Kipi ni bora, kuajiri Kampuni ya Ulinzi au kuajiri mlinzi binafsi?

Kipi ni bora, kuajiri Kampuni ya Ulinzi au kuajiri mlinzi binafsi?

Requal

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2020
Posts
1,025
Reaction score
1,923
Wakuu habari zenu.

Niko kwenye hatua za mwisho za kuanzisha mradi wangu ambao utahitaji huduma ya ulinzi wa walinzi wengi katika maeneo mbalimbali.

Kwa wazoefu wa kuajiri walinzi binafsi lakini wenye mafunzo na weledi na hawa wa kupitia makampuni, wapi wanakuwa na huduma bora?

Binafsi nimejaribu kufanya mawasiliano na kampuni kadhaa za Ulinzi ili nipate huduma zao wamenipa bei zao kwa kila mtu mmoja. Tatizo nilipojaribu kuwadadisi waajiriwa (Walinzi), kiasi wanacholipwa ni kidogo sana kulinganisha na pesa nitakayotoa kwa kichwa, kitu ambacho kinaweza kufanya wakajiingiza kwenye matendo ya wizi au kufanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wizi kuongezeka.

Sasa nikawa nafikiria ni bora niajiri mwenyewe ili niwalipe kiasi ambacho watakuwa na ari ya kufanya kazi kwa kuzingatia kiwango cha elimu angalau kuanzia kidato cha nne.

Kabla sijafanya maamuzi haya, ningependa kupata mawazo yenu wazoefu wa masuala ya ulinzi au wanufaika wa huduma hizi za ulinzi nini faida na hasara za kuajiri kampuni au kuajiri mtu moja kwa moja bila kupitia kampuni?

Karibuni kwa mawazo yenu.
 
Walinzi wako watahitaji usimamizi toka kwako.

Walinzi wa makampuni usimamizi haukuhusu.

Kama unaweza kusimamia shughuli zako na kuwajibika ipasavyo katika kusimamia ulinzi nakushauri Linda mwenyewe.
 
Walinzi wako watahitaji usimamizi toka kwako.

Walinzi wa makampuni usimamizi haukuhusu.

Kama unaweza kusimamia shughuli zako na kuwajibika ipasavyo katika kusimamia ulinzi nakushauri Linda mwenyewe.
Kutakuwa na Chief Security kaka, na huyo nafikiri ndio atakuwa anawajibika kwangu
 
Kutakuwa na Chief Security kaka, na huyo nafikiri ndio atakuwa anawajibika kwangu
Ikitokea umeibiwaa na ikaonekana ni uzembee wa Kampuni nasikia wanahusika kukulipa mali iliyoibiwaa...!! Kama linzi binafsi imekulaa kwakoo
 
Nianze na walinzi wa kampuni: hawa wanafaa kwa kuwa jambo lolote la hujuma litakalofanywa na mlinzi huyo, pa kuanzia kufuatilia panakuwepo, kuliko mlinzi binafsi akisepa ndiyo imetoka.

Halafu kufuatilia huyo mlinzi wa kampuni analipwaje, wewe siyo suala lako.

Tukija walinzi binafsi, kabla haujamwajiri hakikisha yafuatayo: awe amepitia mafunzo ya awali ya mgambo, upafahamu anakoishi, awe na wadhamini, awe kijana ama umri wa makamo asiwe mzee, awe na uzoefu na mambo ya ulinzi.

Sasa wewe mwenyewe utapiga hesabu zako uone wapi anskufaa.
 
Ulinzi ni kitengo nyeti sana, hatuwezi tukaajiri mtu kutoka barabarani kama nikiona ulinzi binafsi unafaa basi Vetting ya uhakika itafanyika kipindi cha kuajiri

Na kingine kwa vile wananifanyia kazi, maslahi yao ni muhimu niyajue kwa nature ya mradi ninaoanzisha haiwezekani niwe na mlinzi asiye na uhakika wa kushiba
 
Uzuri wa third part, wewe huhusiki na ishu yoyote ya mambo ya likizo, uzazi, posho etc etc. Sheria ya mahusiano kazini
Pamoja na hapo gharama za kulipa kampuni zinakuwa kubwa na walinzi wanalipwa kidogo hivyo badala ya kufanya kazi kwa ufanisi kinyume na matarajio wanakuwa na misongo ya mawazo hali inayopelekea kufanya kazi chini ya kiwango
 
Ukitaka kazi zako zifanywe kwa ustadi ajiri binafsi lakini hakikisha unawajua vizuri hao unaowaajiri, wafanyie screening ya hali ya juu ikiwemo kujiridhirisha kwa serikali za mitaa wanakoishi hata mabalozi wa nyumba kumi huko wanakotokea na wazamini wawe ndugu wa damu wenye makazi yasiyohamishika na wasaini kutoa ushirikiano au kuwajibika pale ndugu yao atakapofanya mambo ya tofauti yenye uvunjifu wa sheria then walipe vizuri na wape kazi.

Makampuni yanawanyonya sana na mlinzi anatakiwa awe strong na mweye afya na utimamu wa akili njema ikiwa na haya yanatokana na anacholipwa vinginevyo tegemea kuwa na mlinzi pambo tu, mzee kaajiri binafsi na wanapiga kazi kwa weledi sana tena sana..
 
Ukitaka kazi zako zifanywe kwa ustadi ajiri binafsi lakini hakikisha unawajua vizuri hao unaowaajiri, wafanyie screening ya hali ya juu ikiwemo kujiridhirisha kwa serikali za mitaa wanakoishi hata mabalozi wa nyumba kumi huko wanakotokea na wazamini wawe ndugu wa damu wenye makazi yasiyohamishika na wasaini kutoa ushirikiano au kuwajibika pale ndugu yao atakapofanya mambo ya tofauti yenye uvunjifu wa sheria then walipe vizuri na wape kazi.

Makampuni yananyonya sana, mzee kaajiri binafsi na wanapiga kazi kwa weledi sana tena sana..
Mkuu nakuomba PM

Ahsante sana kusikia hivi
 
Kibiashara, Kimaslahi na Kiusalama Kuajiri Makampuni ni SAHIHI.

Kimaslahi (Kwa Walinzi ) Ni Ndio na Hapana.

Je, Uajiri mwenyewe: Ndio na Hapana.

Chaguo ni Lako.
 
Uzuri wa kampuni ya ulinzi ukiibiwa, wao wanakuwa responsible. Sasa mlinzi binafsi utamdai nini alafu siku nyingine anaweza asiwepo kwa matatizo mmbakimbali ya kijamii
 
Kutakuwa na Chief Security kaka, na huyo nafikiri ndio atakuwa anawajibika kwangu
Ndo hivyo ambavyo mfumo mzima wa sekta ya ulinzi ilivyo.

Kumbuka, uniform , mishahara, vitendea kazi, marupurupu makusanyo ya mifuko ya jamii nk.

Yaani sasa kampuni yako itakuwa na watumishi zaidi.
 
Uzuri wa kampuni ya ulinzi ukiibiwa, wao wanakuwa responsible. Sasa mlinzi binafsi utamdai nini alafu siku nyingine anaweza asiwepo kwa matatizo mmbakimbali ya kijamii
Mkuu kwani akiwa kwenye kampuni hayo matatizo hawayapati mkuu?

Then kwenye issue ya kuibiwa nataka kupata uzoefu kwa walio na walinzi binafsi ila sio hawa wamasai
 
Back
Top Bottom