Jitu la kienyeji
JF-Expert Member
- Dec 13, 2014
- 4,445
- 7,987
Umeongea kweli kampuni nyingi zinawanyonya sana wafanyakazi wao na hio ndo sababu wanaibaa!Wakuu habari zenu.
Niko kwenye hatua za mwisho za kuanzisha mradi wangu ambao utahitaji huduma ya ulinzi wa walinzi wengi katika maeneo mbalimbali.
Kwa wazoefu wa kuajiri walinzi binafsi lakini wenye mafunzo na weledi na hawa wa kupitia makampuni, wapi wanakuwa na huduma bora?
Binafsi nimejaribu kufanya mawasiliano na kampuni kadhaa za Ulinzi ili nipate huduma zao wamenipa bei zao kwa kila mtu mmoja. Tatizo nilipojaribu kuwadadisi waajiriwa (Walinzi), kiasi wanacholipwa ni kidogo sana kulinganisha na pesa nitakayotoa kwa kichwa, kitu ambacho kinaweza kufanya wakajiingiza kwenye matendo ya wizi au kufanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wizi kuongezeka.
Sasa nikawa nafikiria ni bora niajiri mwenyewe ili niwalipe kiasi ambacho watakuwa na ari ya kufanya kazi kwa kuzingatia kiwango cha elimu angalau kuanzia kidato cha nne.
Kabla sijafanya maamuzi haya, ningependa kupata mawazo yenu wazoefu wa masuala ya ulinzi au wanufaika wa huduma hizi za ulinzi nini faida na hasara za kuajiri kampuni au kuajiri mtu moja kwa moja bila kupitia kampuni?
Karibuni kwa mawazo yenu.