Kipi ni bora, kuajiri Kampuni ya Ulinzi au kuajiri mlinzi binafsi?

Umeongea kweli kampuni nyingi zinawanyonya sana wafanyakazi wao na hio ndo sababu wanaibaa!
 
Ajiri walinzi wako wafanyie vettingya kutosha.Makampuni wengi wababaishaji hata likitokea tatizo bado mtasumbuana tu damage ya 2,000,000 tu mtasumbuana sana nina experience ni Hii kitu.Kampuni utailipa 200,000 kwa mwezi mlinzi anapewa 80,000 ikienda sana 100,000.Tafuta head of security mzuri mpe 250,000 walinzi 150,000 (Nssf) utajiongeza ufanyaje na bonas kidogo stori imeisha.
 
Ahsante boss kwa ushauri wako
 
Broo Bora wa linzi was kampuni hao binafsi wanachongaga na majambazi inje kuja kuiba mfano nimeona walinzi was minala ya simu wanavyo waliza makampuni Wana leseni na ukiibiwa wanakulipa na maudhurio au ufanisi was mlinzi wanafuatilia wao ila usi yatafute makampuni mdogo ambayo hayana uwezo
 
ajili mlinzi binafsi anakuwa kama moja ya familia kuliko kukuletea kila siku mlinzi mpya watakuletea wezi wengi wa walinzi ni wezi wametafuta kazi kusoma mazingira kisha waibe.
 
Mkuu kwani akiwa kwenye kampuni hayo matatizo hawayapati mkuu?

Then kwenye issue ya kuibiwa nataka kupata uzoefu kwa walio na walinzi binafsi ila sio hawa wamasai
Kwanini sio wamasai mkuu?

Hao wrote sio kitu tafuta walinzi wachache then weka mbwa hata wanne ..waliopitia mafunzo huko polisi ..

Mbwa hajawahi kuwa na udhuru hata siku moja ..lakini binadam utaskia ooh nina sherehe ,msiba mke Wang kajifungua
 
Kwanini sio wamasai mkuu?

Hao wrote sio kitu tafuta walinzi wachache then weka mbwa hata wanne ..waliopitia mafunzo huko polisi ..

Mbwa hajawahi kuwa na udhuru hata siku moja ..lakini binadam utaskia ooh nina sherehe ,msiba mke Wang kajifungua
Nahitaji walinzi ambao Wana uwezo wa kuandaa report na ufahamu wa lugha ya kiingereza

Ahsante boss kwa ushauri wako
 
Form four awe anajua kingereza plus kuandaa report?? Lakini hujasema report ya aina gani na kwa kutumia mini..computer ama
Mpaka wasiosoma wapo wanajua lugha mkuu tena vizuri tu lugha haijalishi Kama una PHD au la, nadhani utakuwa unachanganya mambo kuona form four hawezi kujua na kutumia hiki kiingereza Cha kawaida.

Hebu tembelea huko makazini, usidhani wanaoandaa report ni wenye masters na PHD, wapo wenye elimu ndogo kulingana na uzoefu wao kwenye fani zao wanaaandaa report nzuri sana
 
tupe kazi sisi walinzi wa kawaida
 
nssf kivipi hapo?
 
Ni rahisi kuvunja mkataba na kampuni ya ulinzi kuliko kuvunja mkataba na mwajiriwa. Fanya "cost benefit analysis" kama wewe ni mlipaji mzuri basi kuajiri ni ghali zaidi kuliko kuweka kampuni kwa maana ya mwajiriwa haweze fanya kazi siku saba, hawezi fanya kazi masaa 12 bila kudai "overtime", kuna kuumwa, kuna dharura na kuna likizo; vyote hivyo ukiviweka kwenye mizani ni bora kuweka mkataba na kampuni ya ulinzi.

Suala la tofauti kati ya utakacholipa na anacholipwa mwajiriwa wa kampuni ya ulinzi ni "non of your business" kwani kampuni ina "overheads" zake kama magari ya doria, supervisors, management, ofisi, leseni, kodi zinazohusiana na mwajiriwa kama SDL, likizo vyote hivyo unachangiwa wewe mteja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…