Watu hawajui maana ya branding, dunia ilishahama kutoka kwenye Oligopolistic market business na sasa ipo kwenye Multilateral market business, hakuna kampuni inapeleka bidhaa sokoni ili ikae muda mfupi, brands kama Samsung, LG, Hisense, Sony na Panasonic ni za muda mrefu, ndio mana zinaa minika.
Zinaaminikaje?
Imagine brands zilitengeneza TV miaka zaidi ya 15 iliyopita, si lazima itakuwa na mtumba wake? Maana yake lazima uje sokoni, watu wataamini zinadumu kuliko zilizokuja sasa hivi.
Kinachotokea ni nini?
Zitaendelea kununulika, halafu kuna Brands zimeingia hivi karibuni, na hazina miaka hata 7, yaani hakuna mitumba yake. Vole vile, hazijajitangaza sana, hawawezi kuuza kwa bei kubwa.
Mimi mpaka sasa, nimebadilisha TV kama nne, kutoka mwaka 2021, haziharibiki, hapana, ila ni shida tu, ila kuna jirani yangu hapa ana Star X tangu Juni 2018, alinunua mpya, mpaka leo ipo vile vile, hajabadili hata stendi, na nina dada yangu alinunua Hisense mwaka 2021, mwaka jana wakati wa Sensa anahangaikia suala la wino sijui ulianza mstari.
Ni vile tu, watu hawaelewi. Mambo yamebadilika, hayo Matv wanayochukulia Simple yatakuja kuwa ghali siku za usoni.
Ila tu. Usinunue Mtumba. Wanauzia jina, sio ubora.