Kipi ni bora - Useja au kuoa/kuolewa?

Kwahiyo kwako wewe unachagua ndoa kuliko useja? Mimi Kwangu kuwa mseja ni maisha yaliyo bora sana Kwangu.
 
Kwa hiyo unashauri nini kupitia hizo hadithi za kwenye kitabu cha Biblia ?🤔
 
Useja unachosha jumlisha upweke.
Hapa tu nishachoka upweke sasa sijui kukaa maisha yote kiseja kama nitaweza.
Mi nishajua tu kukaa kiseja siwezi ila ndio hivo sasa bahati mbaya ndoa zinanipitia kushoto.
Sio ndoa zinakupita kushoto, ni nyie mna masharti magumu. Kila mwanamke anayetafuta mume anataka wa kuanzia Miaka 35, in reality Mwanaume wa umri huo kumpata Ni nadra sababu karibu wote wapo kwenye ndoa
Lower your standards, tafuta wa kuanzia Miaka 25
 
Tafuta mdada mpole zaa nae alafu iba mtoto kamlee, mama yake mtafutie kibiashara au kama ana pesa mteme.

Ukishapata mtoto tafta single mother kama wawili wenye maisha, anzisha urafiki kwa ajili ya shoo tu. usiponenepa nitafute unifunge.
 
Kwani Mungu alifanya nini pale Eden?
 

1 Kor 7:1-9​

Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke.
Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake.
Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.
Lakini nasema hayo, kwa kutoa idhini yangu, si kwa amri. Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; walakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi. Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…