Kipimo cha uhuru wa kiimani ni namna dini yenye waumini wengi inavyoweza kuishi na wanaoamini dini tofauti, ni neema tumezaliwa nchi iliyojaa wakristo

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kipimo cha ubora wa dini ni namna unavyoweza kuishi na wanaoamini dini tofauti na yako. Kama jirani yako anaabudu ng'ombe na hakubagui wala kukunyanyasa wewe unayemuabudu Jehova au Allah hakika huyo ni jirani mwema na bora zaidi ya wale wanaohubiri amani na upendo huku wanalazimisha sheria za dini zao uzifuate, kukuvizia na mapanga, n.k.

NCHI ZILIZOJAA WAKRISTO
Kwa nchi zilizojaa wakristo ni ngumu kukuta nchi inajiita dola ya kikristo kwasababu wanathamini uwepo wa dini zingine tofauti na ukristo, Muislam ataabudu dini yake, wahindi wataabudu dini zao, n.k. Mfano ni hapa Tanzania bara, Ni nchi iliyojaa wakristo kwenye makabila yenye watu wengi na sehemu kubwa ya vijijini ni wakristo lakini ukristo unaishi vizuri kabisa na watu wa imani zingine.

Kwa mifano ya hapa Afrika asilimia kubwa ya nchi zinazoongoza kwa amani zimejaa wakristo mfano Ghana, Zambia, Malawi, Tanzania, Botswana, n.k. ni kwasababu kuna hali ya uvumilivu wa kuweza kuishi na imani zingine

NCHI ZILIZOJAA WAHINDU
Ukienda India kuna ubaguzi wa dini, Wakristo wamekuwa wahanga wakubwa wa mauaji, makanisa kubomolewa, vifungo, ni marufuku kufanya mahubiri ya kuwabadilisha watu imani, n.k. Waislam wana idadi ya waumini milioni 200 nchini India lakini wanapitia unyanyasaji na ubaguzi wa dini, Si sehemu salama kwa wakristo na waislam kuishi.

NCHI ZILIZOJAA WAISLAM
Uhuru wa imani ni muhimu, Kuna nchi kama Dubai U.A.E zimekuwa nchi za kuigwa na zimepiga hatua kubwa kwenye maendeleo kwasababu waliamua kuachana na mirengo ya itikadi kali za kidini. makanisa yanajengwa wakrusto wanaenda kusali, wakristo wanapiga kitimoto kwa uhuru, hakuna kulazimishwa kufunga mfungo wa Ramadan, n.k.

Lakini bado nchi nyingi zilizojaa waislam ni mwiba kwa waumini wa dini zingine, Kuna manyanyaso na ubaguzi wa kidini hasa kwa wakristo, mfano kulazimisha wakristo wasile kipindi cha mfungo, Kutoruhusu ujenzi wa makanisa, kutoruhusu vyakula na vinywaji vya wakristo, Uwepo wa vikundi vinavyowinda wakristo, Kukataza kusoma biblia hadharani, n.k.
 
Sema maskini ndo wanatabia ya kubaguana sana kwenye dini wefatilia matajiri hawanaga sana izo mambo wewe nenda kwenye jamii maskini ndo utasikia kesi za kutoka kujenga kanisa,msikiti.

Kiufupi tuwe na hela zinatupunguzia mambo mengi na kuwa bize bize.
kutokuwa bize mwanzo wa watu kuanza kusumbua.
 
Hii ina ukweli asee. Angalia Dubai wanavyoishi na wa imani nyingine.

Saudi Arabia hadi wakina Lil Wayne wanaenda kutumbuiza fresh tu.
 
Sio suala ya uchumi bali ni dini iliyojaa zaidi eneo flani

Waarabu wana pesa nyingi lakini ukikutwa unasoma biblia hadharani nchi zao unafungwa, ni kesi hio

Nenda hapo Zanzibar kuna matajiri wengi tu lakini ukikutwa unakula hadharani kipindi cha mfungo unashushiwa kipigo
 
Wanakushushia kipigo Zanzibar sio matajiri ni akina Nasoro mpauko pangu pakavu.
 
Hii ina ukweli asee. Angalia Dubai wanavyoishi na wa imani nyingine.

Saudi Arabia hadi wakina Lil Wayne wanaenda kutumbuiza fresh tu.
Saudi Arabia bado wana sheria kali sana za kidini , hawaruhusu kubadili dini, hawaruhusu makanisa, hawaruhusu kusoma biblia hadharani, n.k. lada uende kufanya utalii

Dubai U.A.E waliamua kuachana na mirengo ya itikadi kali za kidini, makanisa yanajengwa mengi, wakristo wanakula kitimoto kwa uhuru, Sio lazima kufunga mfungo wa Ramadan, n.k. Leo hii ni nchi ya kuigwa iliyopiga hatua kubwa
 
Sema maskini ndo wanatabia ya kubaguana sana kwenye dini wefatilia matajiri hawanaga sana izo mambo wewe nenda kwenye jamii maskini ndo utasikia kesi za kutoka kujenga kanisa,msikiti.

Kiufupi tuwe na hela zinatupunguzia mambo mengi na kuwa bize bize.
kutokuwa bize mwanzo wa watu kuanza kusumbua.
Uko sahihi. Mara nyingi sisi matajiri hatuna shida sana na todauti zetu za kidini.
 
Kipimo cha ubora wa dini ni namna unavyoweza kuishi na wanaoamini dini tofauti na yako. Kama jirani yako anaabudu ng'ombe na hakubagui wala kukunyanyasa wewe unayemuabudu Jehova au Allah hakika huyo ni jirani mwema na bora zaidi ya wale wanaohubiri amani na upendo huku wanalazimisha sheria za dini zao uzifuate, kukuvizia na mapanga, n.k.

Kwa nchi zilizojaa wakristo ni ngumu kukuta nchi inajiita dola ya kikristo kwasababu wanathamini uwepo wa dini zingine tofauti na ukristo, Muislam ataabudu dini yake, wahindi wataabudu dini zao, n.k. Mfano ni hapa Tanzania bara, Ni nchi iliyojaa wakristo kwenye makabila yenye watu wengi na sehemu kubwa ya vijijini ni wakristo lakini ukristo unaishi vizuri kabisa na watu wa imani zingine

Lakini hali huwa tofauti kwenye nchi zenye imani kubwa nyingine kama uislam na uhindu

NCHI ZILIZOJAA WAHINDU
Ukienda India kuna ubaguzi wa dini, Wakristo wamekuwa wahanga wakubwa wa mauaji, makanisa kubomolewa, vifungo, ni marufuku kufanya mahubiri ya kuwabadilisha watu imani, n.k. Waislam wana idadi ya waumini milioni 200 nchini India lakini wanapitia unyanyasaji na ubaguzi wa dini, Si sehemu salama kwa wakristo na waislam kuishi.

NCHI ZILIZOJAA WAISLAM
Nchi nyingi zilizojaa waislam ni mwiba kwa waumini wa dini zingine, kuna mifano ya nchi kama Iran, Lebanon, Egypt ziliwahi kuwa nchi zilizojaa wakristo lakini wasilam walipohamia na kujaa ukristo ulififia haraka sana kwasababu ya manyanyaso na ubaguzi wa kidini, mfano kulazimisha wakristo kufuata sheria za kiislam, Kutoruhusu ujenzi wa makanisa, kutoruhusu vyakula na vinywaji vya wakristo, Vikundi vinavyowinda kutokomeza wakristo, n.k.hali hii hupelekea wakristo wengi kuhama dini kwa hofu ya usalama wao.
Wewe ni jweli katija wajinga ndiyo waliwao.

Badala kushukuru Waislam, unaleta upoyoyo.

Ukristo uliukuta Uislam ardhi hii. Na ndiyo leo u meli urudisha nyuma kimaendeleo.
Umekuwa mtumwa wa wazungu kifikra. Ni heri hata usingepewa uhuru wa kisiasa labda ungebaki na uhuru wa fikra.
 
Imani hushinda maarifa, bora Nyerere alituwekea mipaka ya kuzilinda dini na imani zetu zisiathiri wenye dini na imani tofauti.

Laiti kama tusingewekewa mipaka ya kidini na kiimani leo kuna mikoa isingekaliwa na watu wa imani zingine.

Hongera kwa Nyerere baba wa taifa letu, hongera kwa watanzania waelewa👏
 
AMEEEN!NI WAVUMILIVU SANA!NA WALA HAWANA SHIDA NA WATU WASIO WA IMANI YAO!ILA UPANDE WA PILI SASA!TAKATAKA TUPU!HUEZI LAZIMISHA DUNIA NZIMA IWE NA MAWAZO/IMANI/MAONO YANAYOFANANA!BINADAMU LAZIMA TUTOFOUTIANE KATIKA KUFIKIRI NK!!
 
Imani hushinda maarifa, bora Nyerere alituwekea mipaka ya kuzilinda dini na imani zetu zisiathiri wenye dini na imani tofauti.

Laiti kama tusingewekewa mipaka ya kidini na kiimani leo kuna mikoa isingekaliwa na watu wa imani zingine.

Hongera kwa Nyerere baba wa taifa letu, hongera kwa watanzania waelewa👏
Ndivyo ulivyodanganywa.

Unafikiri kwanini au kwa lipi anapigiwa debe na kanisa katoliki apachikwe utakatifu?
 
Wewe ni jweli katija wajinga ndiyo waliwao.

Badala kushukuru Waislam, unaleta upoyoyo.

Ukristo uliukuta Uislam ardhi hii. Na ndiyo leo u meli urudisha nyuma kimaendeleo.
Umekuwa mtumwa wa wazungu kifikra. Ni heri hata usingepewa uhuru wa kisiasa labda ungebaki na uhuru wa fikra.
Katika dini zote mbili hazina jema kwa watanzani hususan watanganyika.

Zanzibar imejaa kizazi mchanganyiko kutoka bara na waarabu, ndy race ya wazanzibar ikatokea.

Waarabu kwa muda mrefu kutekea mashariki ya kati walikuwa ni watu wa biashara na sultan seyid said wa kwanza alikuja kama mkimbizi tu kutokea Oman baada ya kuihasi serikali ya kwao, kaja zanzibar kakuta ardhi kaichukua kaitawala kawageuza watu watumwa kawaweka kwenye mashamba ya nazi na karafuu wengine akawa anawauza kama wafanyakazi wa ndani kwa waarabu wengine matajiri ambao walikuwa wanawahasi waafrika ili wakifika uarabuni wasizae watoto wenye asili ya kiafrika.

Hao ndiyo waislamu waliokuja Zanzibar na Tanganyika wakati huo.
Leo unasema tuwashukuru kwa lipi sasa?

Wakiristo wamekuja na sera ya kukomesha biashara ya utumwa iliyokuwa inafanywa na waarabu baada ya kugundua mashine za viwandani zinazofanya kazi zaidi ya watumwa na wafanyakazi wa bei rahisi.

Baada ya ukiristo kuja ndiyo ukoloni mambo leo ukaanza.
Mashule yakaanza makanisa yakajengwa tukagawanywa katika makundi makuu mawili kwa misingi ya uislam na ukiristo.

Nyerere akaturejesha pamoja tena kama waafrika kama Watanganyika kama watanzania akipiga vita udini.

Je ni nani wa kushukuriwa katika ukombozi wetu?
 
Back
Top Bottom