Kipindi cha Mzee Kikwete hakuna aliyehitimu ualimu au udaktari akakosa ajira. Wote walikuwa wanapangiwa tena unachagua pa kwenda

Kipindi cha Mzee Kikwete hakuna aliyehitimu ualimu au udaktari akakosa ajira. Wote walikuwa wanapangiwa tena unachagua pa kwenda

Katika utafiti wangu mdogo, nimebaini kwamba Walimu ambao wamekumbwa na tatizo kubwa zaidi la ukosefu wa ajira ni wale ambao waliosomea Masomo ya Sanaa (Arts). Wale waliosomea Masomo ya Sayansi na wamefaulu vizuri katika masomo yao, tatizo hili la ukosefu wa ajira linaonekana kuwa siyo kubwa sana kwao.
Wito: Someni Masomo ya Sayansi, kwani yana uwanja mpana wa kujiajiri au kuajiriwa, hata nje ya mipaka ya Tanzania.

Ila kwa Sasa ni wote.
 
Unamtetea jiwe rais wa ovyo kuwahi kutokea Tanzania, jiwe alikuwa ni WA ovyo na mbaguzi, , alifukuza wafanyakazi hewa na vyeti feki lakini hakufanya replacement , akaajiri watu wa kabila lake , wasukuma wote ambao nimesoma nao, na niliokutana nao katika harakati za kusaka ajira walipata kazi, Mungu ni wa wote akafanya yake.
Watu wajinga tu ndio wanasema JPM alikuwa rais feki

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Ulibanwa ukiwa unafanya nini? Kwasababu mmlikuwa kimya ghafla tu, boss wenu kapita kule Chato na ninyi mmeanza kumtemea mate marehemu.
Ninyi viumbe mnaroho gani? Hamridhiki tu na ukwasi mnaoupata kwa gharama za watanzania maskini?

Kwanini hampendi maskini wawe na amani hata kidogo?

Chama Cha Mapinduzi kimehama kutoka kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi kuwa chama cha 'wafanyabiashara' na 'wezi' lini chama hiki kitarudi katika dhumuni la kumuinua mkulima na mfanyakazi wa taifa hili?

Kwenu ninyi utaifa na maendeleo ni kuwapo kwa uhuru wa kukwapua na mifuko yenu kujawa maburungutu ya wizi?

Baada ya kukwapua na kushindwa kuendesha nchi mnaanza kumlaumu marehemu kwa kushindwa kwenu kutumia vyema hata pato lenu dogo mnalokusanya ndani.
Kwa hiyo unataka hii nchi tuwe maskini milele na milele? Tukitaka kujikwamua from wakulima to wafanyakazi inakukera sana kwa sababu unapenda umaskini tu!!
 
Acheni kupotoshana. Ajira za ualimu zilianza kuwa shida mwaka 2015. Rejeeni ajira za ualimu mwaka 2015 kama arts waliajiriwa wote. Mwaka huo 2015 ndiyo pia ulikuwa mwaka wa kwanza kwa walimu wa arts kuajiriwa s/msingi. Na ilitajwa kuwa walimu wamejaa shule za sekondari.

Ndiyo maana hata Magufuli alipoanza kuajiri 2016 aliajiri wanasayansi na kiingereza pekee.
 
Mtoa maada naye kama hajielewi. Enzi za JK wahitimu walikuwa kiasi gani na sasa hivi wapo kiasi gani?
 
Alichokuwa anafanya JK ni kuhakikisha watu wanaishia dalasa ya saba au wanafeli form 4, sasa hivi wanaohitimu ni wengi mno na serikali haiwezi ajili wote,
ndio maana wanajaa mitaani
 
JK tutamkumbuka sana kwa kweli alifanikwa sana kuifanya elimu iwe na mvuto kiasi wazazi wakawa wanaona fahari kusomesha maana ajira zipo tena na kumwaga ikapelekea mpaka watu wakipangiwa hawaendi mana Kuna uhakika kesho akitaka atapata tena. Nakumbuka pes za kujikimu kabla hujaanza kazi kwa mwl ilikuwa laki sita na unapewa hapohapo.

Mambo yalianzq kuwa magumu kipindi Cha jpm ajira zikawa ni kutafuta kwa tochi na kaanza group kubwa sana la vijana mtaani bila ajira kitu ambacho mama anahangaika kupambana nacho mana limeshakuwa tatizo. Alaaniwe jpm.
Binafsi namshukuru jk kwa kuwa kipindi kile niliweaza kupata ajira ilihali ni mtoto wa kimaskini tu,siku hizi ili uajiriwe ni lazima uwajue watu
 
Uchumi feki nchi ikijengeka kila kona,nagari ikawa kawida kwa watanzania, GDP ikapaa,wakulima wakaishi maisha mazuri,miundombinu ikajengwa,fdi ikamiminika...acha ujinga babu
Sasa mkuu Kama JK alifanya yote haya kwanini watu hawakumpa maua yake? Wakaishia kumtukana matusi na kumdhalilisha kwa maneno ya kejeli.
 
Sasa mkuu Kama JK alifanya yote haya kwanini watu hawakumpa maua yake? Wakaishia kumtukana matusi na kumdhalilisha kwa maneno ya kejeli.
Huwezi pendwa na wote. Sisi tuliomaliza enzi zake ndo tunamjua. Waliokuwa wanamtukana ni vijana wa juzi tu hawamjui vizuri.
 
Hata usalama.wa taifa alianiri wasukuma tu. Mfano ni jamaa anaitwa Florian nzangizyo
Kwahiyo huyo msukuma mmoja ndio sample ya ukabila?Rafiki yangu ni mchaga alipata ajira 2019
 
JK tutamkumbuka sana kwa kweli alifanikwa sana kuifanya elimu iwe na mvuto kiasi wazazi wakawa wanaona fahari kusomesha maana ajira zipo tena na kumwaga ikapelekea mpaka watu wakipangiwa hawaendi mana Kuna uhakika kesho akitaka atapata tena. Nakumbuka pes za kujikimu kabla hujaanza kazi kwa mwl ilikuwa laki sita na unapewa hapohapo.

Mambo yalianzq kuwa magumu kipindi Cha jpm ajira zikawa ni kutafuta kwa tochi na kaanza group kubwa sana la vijana mtaani bila ajira kitu ambacho mama anahangaika kupambana nacho mana limeshakuwa tatizo. Alaaniwe jpm.
Kipindi cha nyerere walikuwa wanatafutwa miezi kabla ya kumaliza shule na wanapangiwa pa kwenda. Hizo nyakati za nyerere, mwinyi, mkapa, kikwete, na magufuli zimepita. Hiyo ilikuwa zamani
 
Lakini haiondoi ukweli kuwa jiwe katengeneza ombwe kubwa sana la ajira huwezi kukaa miaka mitano bila kuajili hali ya kuwa kila mwaka kuna maelfu ya watahiniwa wanamwagwa mitaani.

Na mbaya zaidi yeye kashashindwa kuajili bado akawa muharibifu wa sekta binafisi na zenyewe zikakosa uwezo wa kujiajili kweli wtz tulikuwa tume patikana.

Huyu mama ana kazi kubwa sana ya kuajili watainiwa wa kuanzia mwaka 2015 na wasasa hivi.
Dada zangu wawili walisomea udaktari toka mwaka 2017 wamekuja kuajiliwa mwaka jana duh jiwe alikuwa kiongozi wa hovyo sana.
Ni kweli miaka mitano ya jiwe hakukua na ajira?
 
Kipindi cha nyerere walikuwa wanatafutwa miezi kabla ya kumaliza shule na wanapangiwa pa kwenda. Hizo nyakati za nyerere, mwinyi, mkapa, kikwete, na magufuli zimepita. Hiyo ilikuwa zamani
Mipango tu mdogo wangu. Ukiwa na mipango poor lazima nchi ikushinde kama jpm ambaye jeshi lingempindua soon
 
Back
Top Bottom