Kipindi gani unakikumbuka kutoka Radio Free Africa (RFA) ya wakati huo

Kipindi gani unakikumbuka kutoka Radio Free Africa (RFA) ya wakati huo

Wakuu nimekaa nikakumbuka miaka hiyo kipindi cha SITOSAHAU cha RFA. Ilikuwa ikifika hiyo mida ni kukaa karibu na redio mfano wakati wa simulizi ya Gamboshi 😂 asee?

Wahenga kipindi kipi mnakumbuka? Au ulikuwa ukikipenda?
Wandugu. Msisahau na RTD yetu club raha leo na Marehemu Julius Nyaisanga. Japo Uzi ni kuhusu RFA. Hapo RFA lilikuwa na mwamba mmoja Zuberi Msabaha akijiita volts laki moja,, na kipindi chake cha miziki ya Zaire-DRC.
 
Hahah ndio huyo huyo Laki Sita Volt Zuberi Msabaha.

Anapiga kikongo kuliko wakongo wenydwe
 
Kipo, kuna siku nilikisikiliza kinaendeshwa na jamaa mmoja anajiita mlevi mwenye busara.
Sasa hivi hakuna mtu anayesikiliza hicho kipindi zaidi a ya mtangazaji anakiendesha mwenyewe (anajisikiliza)

Bogus kweli kweli.
Duu jamani, sijui nitakumbuka siku moja nikiwepo nyumbani huwa saangapi! 😀😀😀
 
●Usiku wa mahaba
●Sintosahau
●Kuna show ya Fredwaa kuna dogo alikua anacheka sana kama jingle nimesahau
●Kulikua na show ya reggae
●Easy Sunday
●The weekend top 40 na kulikua kuna top 100

Hopefully sijachanganya madesa..... good not so old times when radio was a real deal
Kumbe mimi ni mzee sana aisee nitoke nyumbani sasa. Legend habari za mchana
 
Wakuu nimekaa nikakumbuka miaka hiyo kipindi cha SITOSAHAU cha RFA. Ilikuwa ikifika hiyo mida ni kukaa karibu na redio mfano wakati wa simulizi ya Gamboshi 😂 asee?

Wahenga kipindi kipi mnakumbuka? Au ulikuwa ukikipenda?
Bolingo time,
Msabaha akigonga lingala hatari!
 
Kumbe mimi ni mzee sana aisee nitoke nyumbani sasa. Legend habari za mchana
Hahahahaha usiogope..... wengine tumeanza sikiliza vitu toka tukiwa primary huko.... 35 yenyewe bado sana ingawa tayari 3rd floor
 
Hizi ndio nyuzi unasoma unasikia raha na kukumbuka zamani.
Fred waaa kiukweli alikuwa mtu na nusu kipindi hicho nikiwa kwetu Morogoro hadi maza alimjua Fredwaa maana aliona kijana wake navodata.

Later pale Moro ikaja Radio Ukweli na Abood!

Nilipoishi Dodoma nikaifamu vizuri Kiss FM aisee kuna ngoma kali sana zilikuwa zinapigwa around saa moja hadi mbili ngoma kama Mbele kwa mbele Dj Yusuf daily.
Bila shaka ilikuwa ni African Beats hiyo.​
 
Back
Top Bottom