Wazee wa hip hop Mtakumbuka kipindi cha Weekend fever kikiongozwa na Uncle Sam....jamaa alivumbua vipaji vingi vya hip hop hakuna kipindi cha redio cha hip hop kama kile.
Halafu kuna RFA bonanza alikuwa anatangaza huyu jamaa Sky walker wa simulizi na sauti alikuwa anauwa sana.
Vodacom Burudani zaidi
Ndani yake kulikuwa na session ya sindano 5 za moto chini ya Marehem Freduwah.
Sitosahau- hichi kipindi kiliwateka watu wengi sana,mimi ile stori ya jamaa wa Gamboshi pamoja na Rojaz aliyezamia SA lakini hakutoboa akarudi bongo na kufungua Saluni.
Duniani wiki hii-kipindi kilichokuwa kina kusanya matukio yaliyotokea duniani kwa wiki Nzima~ Mtangazaji alikuwa kama Rahab Fred kama sijakosea.
Bolingo time chini ya Marehem u Zuberi Msabaha.
Show time ya kina kidbway Glory Robinson Mtoto wa Mama Sabuni.
Kipindi cha michezo na kina steve Moyo mchonge na Baruani Muhuza.
Nadhani hii ndio redio bora ya miaka ya 2010 kurudi nyuma ilikuwa imesheheni vipaji vya waandishi na watangazaji hodari sana...
Sijui walifeli wapi?