Kipindi gani unakikumbuka kutoka Radio Free Africa (RFA) ya wakati huo

Kipindi gani unakikumbuka kutoka Radio Free Africa (RFA) ya wakati huo

Kipindi cha mchezo ambalo kulikuwa na David Azaria, Jackson Nyamsuka, Deokaji Makomba, Hasan Mvula, bila kusahau Steve Moyo Mchongi ambaye alikuwa aninikosha sana pale anapotusomea msimamo wa ligikuu Tanzania bara.

RIP Steve Moyo.
 
Ahmed Ali, Ben mwanantala, mayco Noel, Rebeka Mulesi, sports lady Fatum gafus ambaye NI marehemu, Yusuf magasha, Dickson mpilipili, Maregesi Nyamaka , Gwamaka Francis bila kusahau Nasoro Dimoso.
 
Ahmed Ali, Ben mwanantala, mayco Noel, Rebeka Mulesi, sports lady Fatum gafus ambaye NI marehemu, Yusuf magasha, Dickson mpilipili, Maregesi Nyamaka , Gwamaka Francis bila kusahau Nasoro Dimoso.
Ila hawa wa siku hizi wamechuja sana, huwezi kuwafananisha na akiona Deokaji Makomba mtu mwenye sauti nzito ambaye kwa sasa hivi ni ripota wa DW kutoka Dodoma.
 
●Usiku wa mahaba
●Sintosahau
●Kuna show ya Fredwaa kuna dogo alikua anacheka sana kama jingle nimesahau
●Kulikua na show ya reggae
●Easy Sunday
●The weekend top 40 na kulikua kuna top 100

Hopefully sijachanganya madesa..... good not so old times when radio was a real deal
Icho cha fred kilikua sindano tatu za moto
Hahahaha kile kicheko ni hatari
 
Hizi ndio nyuzi unasoma unasikia raha na kukumbuka zamani.
Fred waaa kiukweli alikuwa mtu na nusu kipindi hicho nikiwa kwetu Morogoro hadi maza alimjua Fredwaa maana aliona kijana wake navodata.

Later pale Moro ikaja Radio Ukweli na Abood!

Nilipoishi Dodoma nikaifamu vizuri Kiss FM aisee kuna ngoma kali sana zilikuwa zinapigwa around saa moja hadi mbili ngoma kama Mbele kwa mbele Dj Yusuf daily.
 
Wazee wa hip hop Mtakumbuka kipindi cha Weekend fever kikiongozwa na Uncle Sam....jamaa alivumbua vipaji vingi vya hip hop hakuna kipindi cha redio cha hip hop kama kile.

Halafu kuna RFA bonanza alikuwa anatangaza huyu jamaa Sky walker wa simulizi na sauti alikuwa anauwa sana.

Vodacom Burudani zaidi
Ndani yake kulikuwa na session ya sindano 5 za moto chini ya Marehem Freduwah.

Sitosahau- hichi kipindi kiliwateka watu wengi sana,mimi ile stori ya jamaa wa Gamboshi pamoja na Rojaz aliyezamia SA lakini hakutoboa akarudi bongo na kufungua Saluni.

Duniani wiki hii-kipindi kilichokuwa kina kusanya matukio yaliyotokea duniani kwa wiki Nzima~ Mtangazaji alikuwa kama Rahab Fred kama sijakosea.

Bolingo time chini ya Marehem u Zuberi Msabaha.
Show time ya kina kidbway Glory Robinson Mtoto wa Mama Sabuni.
Kipindi cha michezo na kina steve Moyo mchonge na Baruani Muhuza.

Nadhani hii ndio redio bora ya miaka ya 2010 kurudi nyuma ilikuwa imesheheni vipaji vya waandishi na watangazaji hodari sana...
Sijui walifeli wapi?
 
●Usiku wa mahaba
●Sintosahau
●Kuna show ya Fredwaa kuna dogo alikua anacheka sana kama jingle nimesahau
●Kulikua na show ya reggae
●Easy Sunday
●The weekend top 40 na kulikua kuna top 100

Hopefully sijachanganya madesa..... good not so old times when radio was a real deal
Hiki cha "sitasahau" watu walikua wanasimama barabarani kusikiliza kama njia moja ya kupumzika maana boda ya zamani ni miguu
 
Show Time, J3,J5 na Ijumaa na Sindano tano za moto na Fred Waah kila Jumamosi asubuhi!
Jumapili tukitoka kanisani tunawahi kusikiliza Sitasahau!
Pia ilikuwepo Search Line!
 
Hao kina malegesi sio wa siku hizi kweli?hata mimi namkumbuka Deokaji Makomba jamaa ana sauti la kipekee.
Maregesi ni wa siku hizi, Deokaji na akiona Jackson pajo nyamsuka, Deokaji makomba pamoja na yusuf magasha ni wa kitambo kidog
 
Back
Top Bottom