Ghost MVP
JF-Expert Member
- May 19, 2022
- 439
- 736
Habari wana jukuwaa. Ni matumaini yangu unaendelea salama wewe kama mdau!
Leo niwape Tips kadhaa zitakazokusaidia Kujiupusha na Ajali unapoendesha chombo cha Moto Barabarani. Ajali nyingi zinaweza kutokea kipindi cha mvua nyingi kwasababu ya uoni hafifu wa madereva na vyombo vingine hivyo zingatia yafuatayo
Leo niwape Tips kadhaa zitakazokusaidia Kujiupusha na Ajali unapoendesha chombo cha Moto Barabarani. Ajali nyingi zinaweza kutokea kipindi cha mvua nyingi kwasababu ya uoni hafifu wa madereva na vyombo vingine hivyo zingatia yafuatayo
- Tumia Fog-Lights: Hizi ni taa ndogo zinaokaa Chini ya bamper nyingi hufanana kama mduara, ila huwa zinajitenga, Fatilia Manual ya namna ya kuwasha Fog light kwenye Chombo chako, lakini gari nyingi hii inawasha sehemu unayowasha Taa za kawaida kuna kiringi kidogo cha kuzungusha. Unapowasha hizi na za nyuma zitawaka Hivyo anayekuja mbele atakuona kwa kupitia mwanga wa FogLights zako na anayetokea Nyuma atakuona pia kupitia Parking Lights zako.
- Bana Upande Wa Kushoto: Kwa sisi tunaendesha gari za Mkono wa kulia tunapaswa kubana karibu na mshari wa kushoto kwa7bu dereva wengi kipindi cha mvua wanataka kupita katikati ya barabara lakini unapofanya hivyo chukua tahadhari pia usitoke nje sana na kuvuka au kukanyaga Mstaari.
- Tembea Polepole: Speed yako kubwa iwe 60 Kph kwa speed hii inaweza kukupa adverntage kuchukua maamuzi pale inapotokea Emergency na kusaidia gari isiteleze ushikapo Break.
- Zingatia Break: Hakikisha Break pads zako ziko kwenye hali nzuri na jazitaleta shida kwenye maji, Lakini pia unaposhika break basi fanya polepole ili kuepusha gari kuteleza na taharaki kwa anayekuja nyuma yako.
- Hali ya Taa: hakikisha taa zako za nyumba zote zinawaka na hakuna iliyoungua, na za mbele pian na pia jitahidi kutumia Endicator unapotaka kukunja.
- Epuka Madimbi ya Maji: Mengine yanaweza kuwa Marefu na yakaleta Shida katika chombo chako hivyo chukua Tahadhari unapovuka madimbwi ya maji.
- Epuka Maji yanayoTembea: usidharau kasi ya maji wala wingi chukua tahadhari ili kuepusha gari yako kuzidiwa na maji na kusombwa hivyo weka akili kichwani sio mguuni ndugu.