Kipindi hiki cha mvua Tandika siyo sehemu ya kwenda kabisa

Kipindi hiki cha mvua Tandika siyo sehemu ya kwenda kabisa

2019

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2018
Posts
3,130
Reaction score
4,735
Wilaya masikini kabisa kwa mkoa wa Dar es Salaam ni Temeke, wilaya yenye watu duni kabisa ni Temeke, wilaya iliyochelewa kabisa kimaendeleo ni Temeke.

Hata mipango na miundombinu duni kabisa ni Temeke. Inaongoza kwa uchafu pia.

Jambo la kushangaza nimepita soko Tandika kuna mitaa imepangwa mingi ni michafu sana ni michache ina lami lakini hakuna mitaro ya maji hata m1.

Hata barabara inayokatiza kwenda Buza japo ni njia kuu lakini hakina mitaro. Kukosekana kwa mitaro kumefanya maji yatuame sehemu moja na kuchimba hapo na kukaa muda mrefu kutoa harufu mbaya na kuaribu barabara yenyewe.

Ukitoa soko la Kariakoo linafuata la Tandika lakini hakuvutii kabisa. Sehemu pekee unayoweza kukaa kwenye wilaya hii ni Mtoni Kijichi tu lakini Tandika na Mbagala zimechelewa sana kuendelea.

Serikali inapaswa kuangalia maeneo haya kwa mbele zaidi kwani ni miji na masoko yanayokuwa kwa kasi sana lakini miundombinu inaweza kuwakatisha tamaa wawekezaji wanaotaka kuwekeza maeneo hayo.
 
Kuna siku nilipitia K/koo stand ya magari ya mbagara,aisee nilitamani kutapika Mana kuna chemba ya mavi ilikuwa inatema kama chemchem hatari...na ile mvua daaah.

Na si apo tu,kwa kifupi miundo mbinu yetu ya kupitisha maji taka haipo vzuri kabsa.

Kule kwa Azizi Ali kuna barabara ya mtaa inajengwa,mtaro wa maji taka upo upande mmoja na hauna slope yaani upo kama swimming pool tu,maji yamejazana hayana pakwenda. Sometime maji humwaga,ni shida tupu,wachina sometime wanazingua.
 
Dar ni wilaya ya Kinondoni na Ilala tu huko kwingine hauna tofauti na mtu alieko Namtumbo tu sema wanajiita wako Dar.

Njoo uishi zako Tegeta, Bunju, Goba, Mbezi , Madale , Makongo juu , Chuo kikuu ( changanyikeni) n.k

Huwa nashangaa mtu anaenda kununua kiwanja Mbagala hahaha.
 
Dar ni wilaya ya kinondoni na ilala tu huko kwingine hauna tofauti na mtu alieko Namtumbo tu sema wanajiita wako Dar...
Kweli kabisa mkuu lakini utadhani Temeke haiko Dar kabisa ilivyosahaulika
 
Kweli kabisa mkuu lakini utadhani Temeke haiko Dar kabisa ilivyosahaulika
Ndio ndio mkuu wilaya ambazo zinatoa picha ya Dar ni kinondoni na ilala huko kwingine ni Upuuzi tu.

Mtu Yuko Tandika, Buza, Mbagala nk anajiita Yuko dar. Wewe uko Somalia maana hata mikoani Hakuna sehemu za ajabu Kama Tandika au Mbagala.

Jichanganye wilaya ya kinondoni au ilala mkuu kwanza Temeke hata kuweka familia huko inakuwa ya kiswahili. Unakaa na waswahili waswahili tu
 
Nimecheka sana baada ya kusoma hii posti na nikasema moyoni aliyepost atakuwa haijui Dar es Salaam. Bandari ya Dar es salaam ipo Temeke, Tazara ipo Temeke, Uwanja wa Taifa upo Temeke, CBE ipo Temeke, Veta ipo Temeke, Daraja la kigamboni lipo Temeke. Kumbuka tu kila sehemu wapo Matajiri na maskini na maskini ndiyo hufa zaidi.

Mvua ya octoba kinondoni 8 ilala 4.Maeneo athirika vingunguti, kigogo na kinondoni, Mwananyamala ,Kinondoni. Hata kikija kipindupindu jibu Ilala na Kinondoni hupigwa zaidi. Fikiri tena njoo upost
 
Nimecheka sana baada ya kusoma hii posti na nikasema moyoni aliyepost atakuwa haijui Dar es Salaam. Bandari ya Dar es salaam ipo Temeke,Tazara ipo Temeke,Uwanja wa Taifa upo Temeke,CBE ipo Temeke,Veta ipo Temeke, Daraja la kigamboni lipo Temeke. Kumbuka tu kila sehemu wapo Matajiri na maskini na maskini ndiyo hufa zaidi .Mvua ya octoba kinondoni 8 ilala 4.Maeneo athirika vingunguti, kigogo na kinondoni, MWananyamala ,kinondoni. Hate kikija kipindupindu jibu ilala na Kinondoni hupigwa zaidi. Fikiri tena njoo upost
Kwahiyo watu wanaishi humo bandarini , Veta , uwanja wa taifa na CBE?

Mtu anakuja kuzungumzia maeneo wanayoishi watu wewe unaleta uwepo wa bandari na uwanja wa taifa. Una akili za kijinga sana.

Hivi unaweza kulinganisha Mbagala na Tegeta. Au Ununio na Tandika.

Nyie ndio mnajenga madaraja na matreni mnaacha watu hawana hata madawati darasani.
 
Dar ni wilaya ya kinondoni na ilala tu huko kwingine hauna tofauti na mtu alieko Namtumbo tu sema wanajiita wako Dar.

Njoo uishi zako tegeta, Bunju, Goba, mbezi , Madale , Makongo juu , Chuo kikuu ( changanyikeni) n.k

Huwa nashangaa mtu anaenda kununua kiwanja Mbagala hahaha.
Huwa siwaelewi watu wanaoishi wilaya ya temeje[emoji2][emoji2]
 
Dar ni wilaya ya kinondoni na ilala tu huko kwingine hauna tofauti na mtu alieko Namtumbo tu sema wanajiita wako Dar.

Njoo uishi zako tegeta, Bunju, Goba, mbezi , Madale , Makongo juu , Chuo kikuu ( changanyikeni) n.k

Huwa nashangaa mtu anaenda kununua kiwanja Mbagala hahaha.
Hayo maeneo uliyotaji ili watu waje kuishi,miaka ya nyuma ilikuwa ni machaka na mapori ya kufa mtu,usingeweza hata kuwaza kuwa angeweza kuishi binadamu,shida ya hayo maeneo ya Tandika, Mbagala, Kariakoo, Ilala n.k yako chini na pia yako level kwahiyo kutuama kwa maji sio jambo la kushangaza,ingawa serikali inatakiwa itafute njia mbadala ili kuweza kuyanusuru kwani miaka hiyo ndio yalikuwa maeneo ya wajanja ukitoa Mbagala ambayo nayo ilikuwa maporini.
 
Sure kabisa Mimi hata nijie fulia namna gani sikai eneo lolote ndani ya wilaya ya temeje[emoji1787][emoji1787][emoji3577]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Yaani mtu unatoka mkoani kwenye Hali ya hewa nzuri unakuja kuishi Tandika , Mbagala au Buza, matumizi mabaya ya nauli.


Njoo uishi Mbezi , Tegeta, Makongo juu, Bunju n.k sio huko uswekeni.


Siwez ishi wilaya ya temeke Mimi Bora nirudi mkoani Kuna Hali ya hewa nzuri.
 
Hayo maeneo uliyotaji ili watu waje kuishi,miaka ya nyuma ilikuwa ni machaka na mapori ya kufa mtu,usingeweza hata kuwaza kuwa angeweza kuishi binadamu,shida ya hayo maeneo ya Tandika,Mbagala,Kariakoo,Ilala n.k yako chini na pia yako level kwahiyo kutuama kwa maji sio jambo la kushangaza,ingawa serikali inatakiwa itafute njia mbadala ili kuweza kuyanusuru kwani miaka hiyo ndio yalikuwa maeneo ya wajanja ukitoa Mbagala ambayo nayo ilikuwa maporini....
Kwani huko Tandika unakosema kulikuwa ndio maeneo ya wajanja hakukuanza kuwa Pori?

Kuna mji ambao haukuanza na pori. Tokeni huko uswekeni [emoji16]
 
Halafu wanajiona wajanja balaaa kuwa ndio wenye jiji wakati wako kwenye mkoa wao [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Sijui mkuu ujanja unaouzungumzia wewe ni upi,Ujanja wa watu wa Dar huko ndiko ulikoanzia,Kariakoo,Temeke,Tandika,Ilala yote ndio kulikuwa na viwanja vya kujirusha vya hatari...
 
Yaani mtu unatoka mkoani kwenye Hali ya hewa nzuri unakuja kuishi Tandika , Mbagala au Buza, matumizi mabaya ya nauli.


Njoo uishi Mbezi , Tegeta, Makongo juu, Bunju n.k sio huko uswekeni.


Siwez ishi wilaya ya temeke Mimi Bora nirudi mkoani Kuna Hali ya hewa nzuri.
Kila mtu ana maamuzi yke na akae sehemu aipendayo msitufos kuishi huko mbopo
 
Back
Top Bottom