Kipindi Tunamtafakari Dewji, Naomba atujibu Maswali Haya

Ha ha ha,hayo nayo unayaita mafanikio kulingana na umri wa simba?!!!!

Alafu kipindi tunafurahia mafanikio ya Mnyama.. tujiulize ni Timu gani ilishawahi kufikia au hata kusogelea haya mafanikio ya Mnyama katika ukanda huu wa EAC.
 

Hebu zungumzia mafanikio ya kiuchumi bwana,alafu ulinganishe ukubwa wa timu yenye mtaji wa mashabiki nchi nzima na umri mkubwa ilionao
 
Alafu kipindi tunafurahia mafanikio ya Mnyama.. tujiulize ni Timu gani ilishawahi kufikia au hata kusogelea haya mafanikio ya Mnyama katika ukanda huu wa EAC.

Hayo mafanikio unayoyazungumzia ni kiduchu sana,ni kwaajili ya kuitambia yanga tu,hebu nambie simba ilipata sh.ngapi kwa kufika final cuf na wamenunua nini,isiwe na akili za kizamani bwana uzeni timu ipate mafanikio ya kweli
 
Kasema simba hataki faida sababu ana biashara zaidi ya mia zinampa faida,yeye anataka timu ifanikiwe na mashabiki(akiwemo yeye) wapate raha.
Huyu jamaa ashawahi kuidhamini simba miaka ya 2000 nakumbuka na ilifanya vizuri sana kipindi kile.

Inshu uko hivi.. kama aliweza kuidhamini miaka ya 2000 na Mnyama akataka saaaaana..

1. Kwanini asirudi kuidhamini tena, ili itakate zaidi ya miaka ya 2000?
Kwani ni lazima ainunue?!
2. Kama aliidhamini ikatakata.. kwanini alituacha jangwani?! Je tukimkabidhi Timu hata tutelekeza tena??
 
Hayo mafanikio unayoyazungumzia ni kiduchu sana,ni kwaajili ya kuitambia yanga tu,hebu nambie simba ilipata sh.ngapi kwa kufika final cuf na wamenunua nini,isiwe na akili za kizamani bwana uzeni timu ipate mafanikio ya kweli

Hahaha.. siku zote "adui"yako anakuombea njaa.. sasa nashangaa huyu "adui" anayeniombea mwema!?!

Kipindi unataka kufahamu tulipata sh. ngapi hadi kufika final.. tunatakiwa ujiulize pia tulitumia sh. ngapi hadi kufika hapo.

NB: Kipindi hicho Timu zilikua zinajigharamia kila kitu.. hakukua na wadhamini kama wa sasa.
 
huna lolote nyie ndio mnaowatundikia ma-hirizi wachezaji wetu tutokee kule mbweha wewe mwambie aliyekutuma kuwa huu ni wakati wa kidigitali sio analogi
#MoSimba
 
huna lolote nyie ndio mnaowatundikia ma-hirizi wachezaji wetu tutokee kule mbweha wewe mwambie aliyekutuma kuwa huu ni wakati wa kidigitali sio analogi
#MoSimba

Kidigitali kivipi.. mbona unabwabwaja bila fact? Nakuona umechanganyikiwa na bilioni 20 anazotaka kuwekeza.

Simba S.C ikiiuza jezi 2m kwa 10,000/= tu inapata billion 20... hela anavyotaka kuwekeza huyo Mo.. Kumbuka Simba S.C inawanachama zaidi ya 5m.. na hii ni kwa Tanzania pekee.

Narudia tena kama Mo ana uchungu wa kweli.. tunamkaribisha tena katika Bodi ya wadhamini.. na si kumuuzia Timu.

NB: Thamani ya Simba S.C ni mara 10 ya 20 bilioni.
 
huna lolote nyie ndio mnaowatundikia ma-hirizi wachezaji wetu tutokee kule mbweha wewe mwambie aliyekutuma kuwa huu ni wakati wa kidigitali sio analogi
#MoSimba

Kama inshu ni udigitali.. Simba ya sasa IPO kidigitali zaidi.... Kwanini?
1. Ni Football Club pekee CECAFA, yenye website bora kabisa katika ukanda huu.
2. Ni Timu pekee katika ukanda wa CECAFA inayouza jezi zake online.
3. Ni Timu pekee inayowapatia wanachama wake taarifa kuhusu maendeleo yako kupitia njia ya ujumbe wa Simu a.k.a SMS.
4. Ni Timu pekee katika ukanda wa CECAFA unayoweza kupata uanachama online
5. Ni Timu pekee katika ukanda wa CECAFA inayotoa bima ya maisha kwa wanachama wake.
Mkuu Simba Digitali imefanya mambo mengi sana, ila kwa sasa niishie hapa.
 
Hayo mafanikio unayoyazungumzia ni kiduchu sana,ni kwaajili ya kuitambia yanga tu,hebu nambie simba ilipata sh.ngapi kwa kufika final cuf na wamenunua nini,isiwe na akili za kizamani bwana uzeni timu ipate mafani kio ya kweli
mkuu Gor Mahia ya Kenya umeshachukua kombe la wa washindi na Villa ya Uganda ndio timu ya kwanza kucheza kombe la CAF lilipoanzishwa
 
wakati Simba inafika fainali ya kombe la CAF ilikuwa chini ya ufadhiri wa Azim Dewj akishirikiana na baadhi ya wanachama wa Simba kma Mh. Ahmad Rashid aliyekuwa mbunge wa CUF
 
Kiukweli mimi ni shabk damu wa Simba. Kwa umri wa Simba na fan base kubwa iliyonayo tulipaswa tuwe tunapambana kimafanikio na vilabu kongwe barani afrc kama Tp Mazembw, Al ahl, Zamalek, Mamelody Sundowns El merreikh etc. Ilipaswa tuwe ni kitu cha kawaida kwa klabu yetu kufika level za group stage ktk champions lg ( quarter final).
Lakini pia klabu yetu kwa ukongwe wake ilipaswa iwe na uwanja wake wa kisasa.
Klabu mpya kama Azam zilipaswa zituone kama mfano kutokana maendeleo tuliyopaswa kuwa nayo.
Ila bahati mbaya viongozi karibu wote wanaokuja kwenye klabu yetu wanakuja kwa maslahi yao binafsi ya kibiashara yaani hawana common interests za kuziletea maendeleo klabu yetu na hii yote inatokana na mfumo mbovu wa timu kuwekwa mikononi mwa wanachama kwa njia ambazo haziinufaishi klabu na kupelekea kupata viongozi wasio na malengo hayo niliyoyataja. Na pia mfumo wa umiliki uliopo ndio kila mara unazalisha migogoro na mambo kadha wa kadha yasiyo ya kitaalamu.


Sasa nini kifanyike?; Inapaswa tubadili mfumo wa umiliki wa timu. Timu ijiweke ktk mfumo wa kampuni na iuze hisa zake kwa wanachama na ikiwezekana ombi la MO lifanyiwe kazi na apewe klabu kwa hiyo %ge aliyotaka lakini pia aainishe targets alizonazo kuivusha klabu hapa tulipo.

Mabadiliko MO,,,, MO mabadiliko!!!
 
thamani ya simba ni zaidi ya 40 billion.

brand ya simba ni trillions
 
Binafsi huyu mo dewj alishaniteka mawazo nikamuona mtu wa maana mwenye nia njema na simba..lakini ndugu yangu umenifumbua macho..kumbe hawezi kitu kiufupi anataka kututapeli sisi wanachama wa simba
 
Hivi Mo Dewji na Azim wana uhusiano gani au ni majina tu?
 
Simba Sports Club Haiwezi kuuzwa kwa mtu.
SImba sio Kampuni yenye shares .Imesajiliwa kama Club au association . Haikusajiliwa BRELLA.
Ni club ilosajiliwa na wadhamini , iko chini ya trustees kwa niaba ya wanachama na wapenzi wa timu hio nchini na nje ya nchi.

SUALA : Jee unaweza kuithamini Club ya Simba ? na ukapata thamani yake halisi ili uweze kupata bei ya kuipiga bei ? Jawabu ni Hapana huwezi kui value Timu hii . Simba na Yanga zinakaribia zaidi ya Miaka 100 sasa. Hazijawahi kufa , wala hakuna uwezekano wa kufa ,sana zitashuka daraja na kupanda lakini the brand ipo .

Thamani ya Simba ni priceless .You can?t Value it therefore No body can buy it ?imejengwa miaka mingi ni Zaidi ya Vyama vya siasa amabavyo no body can buy vyama vya siasa,
Unapouza Simba sasa kwa akina Aveva , who are they ? wao ni viongozi tu wenye dhamana ya kuiongoza Simba sio Beneficiary wa Club hii, wanaweza kuondoka na hata kuingia yanga?

Nani beneficiary wa hizo 20 billion ? jee kuinunua yenyewe ni kuingiza kwenye programya Maendelo ? au ndio wanunuzi ni kina Aveva waloikuta Simba juzi ? au ni wajukuua wa waswahili wale waloanzisha hii timu Kutoka Sunderland mpaka ilipo fikia ? nani atafaidika na hizo 20b/ akale nwatoto wake kama jasho la kuwa mwanzilishi na mmiliki halali wa Simba ?
Kwa ufupi Simba hai uziki haina shares inamilikiwa na wanachama chini ya wadhamini wao. washabiki wote wana haki ka club hii.

Jiulize unaweza Kuiuza au kuinunua CUF au CCM ? kama hapana basi Simba ni Hapana mara 100 maana ni zaidi ya CUF na CCM.

Unaweza kuinunua Azam , Muundo wake ni Tofauti ni Kampuni inayomilikiwa kwa share.
Vyenginevyo Unaweza Kujenga MO sports club yako , ukafanya MO Academy , Chamanzi kule viwanja vinapatikana. Aige mfano wa Azam au TP Mazembe au Mtibwa .
lakini ukweli na kisheria No body can buy a club belong to more than 30 million fans ndani na nje ya Tanzania . Simba ipo Tanzania , Ipo Zanzibar , Ipo UK ,UAE,OMAN,USA,SCANDINAVIA nk nk . Simba ni Taifa Kubwa its Big enough for any tycoon to buy it ?Brand yake its worth Trillions of Dollar ni kubwa kuliko any company Tanzania?
Wana simab don?t feel or think too Low ?you have build one the greatest club in Africa.
Simba inahitaji Uongozi imara , wanao penda Football, wenye vision wasio mafisadi pia. Simba ikiwa imara na viongozi madhubuti Company nyingi zitakua tayari kui sponsor kwa mikataba minono ya kuiendesha club hio kwa mafanikio makubwa katika soka..

Viongozi waache hayo mawazo kabisa simba ni kubwa kuliko wao hii club haizuki na hawana uwezo wa kisheria kufanya hivyo. huo,
Wenye Simba haswa Tuliwazika zamani nao walituachia hizi club kama urithi wetu ambao sasa kina Aveva wanafikiria kuuza kwa maslahi binafsi
 
Tatizo simba Ina wapenzi tu ila sio wanachama hai Kama kila mwaka hao unaosema wanachama 5mil wangekuwa wanapilia tu kadi zao za uwanachama kiasi cha elfu tano tu kwa mwaka embu Fikiri wangekuwa wanapata sh ngapi ila tatizo sisi porojo nja porojo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…