joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
- Thread starter
- #41
Ninarudia tena, Julius Malema, hakutosheka kusikia kwamba South Afrika ina GDP ya $350B. Yeye aliangalia ni nani anayemiliki hiyo GDP, 10% ya watu nchini humo humiliki 85% ya hiyo GDP, hakukubali kufurahia GDP ya kwenye makaratasi wakati wananchi wa kawaida hawana ardhi, hawana ajira, wanaishi katika slums, hawapati huduma bora za Afya, hakuna "security".Kelele nyingi, mwisho wa siku zero content... Kama wewe ndo una akili basi ongea kama mtu mwenye akili, sio kupiga porojo za hewani
Kwa mfano, unaloongekea hapo ni mali ya mtu binafsi
“Wealth” refers to the net assets of a person. It includes all their assets (property, cash, equities,
business interests) less any liabilities.
Hapo bado tunawashinda na mbali sana! next time, ukiamua kujifaya mwenye akili basi tumia ushahidi, si kupiga story tu, e.g ukitaja saratani, toa takwimu za watu walio na saratani na maafa yake TZ vs Ke,,,etc, sio tu kupiga domo ilhali tunajua mwisho wa siku Watz wengi wanakufa kuliko wakenya
EFF ilianzishwa ili kuwarudishia wananchi wa kawaida GDP yao ambayo wabaisikia ipo ktk karatasi lakini haiwasaidii wananchi walio wengi. Huyo huyo Julius Malema ndiye aliteishangaa Kenya kwa kuona kwamba sehemu kubwa ya uchumi wa Kenya unashikiliwa na Wazungu. Jambo la kushangaza ni kuona kwamba wakenya wenyewe hawaoni kama kuna tatizo wanabaki kuimba nyimbo za GDP kubwa.
Kuhusu tiba, Tanzania tunatoa tiba ya " Cancer" bure kwa kila raia kitu ambacho serikali yenu imeshindwa, sasa hiyo GDP inasaidia nini kama hata uwezo wa kuwajengea mabwaya ya maji wafugaji kule Turkana na Samburu hamuwezi?