Kiporo kipi kitamu zaidi?

Kiporo kipi kitamu zaidi?

Habari ya leo wapenda kula mapocho pocho wenzangu.

Hivi kati ya kiporo cha wali na maharage/ wali ndondo na kiporo cha wali kisamvu (cha nazi au karanga) kipi kitamu?

Yaani nimeona niulize wala viporo wenzangu kwa sababu hapa namalizia kunywa chai na kiporo cha kisamvu yaani nimekaa chini kabisaa kwa utamu nikimaliza kupost uzi huu nashushia na juice ya embe, lol.

Nitapungua mwakani jamani[emoji38][emoji38]

Hebu nambie kiboko yako ya kiporo ni ipi mwenzetu.

~MC~
Mawazo yangu yalinipeleka mbaaali sana aisee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wali maharage mixer chai imekolea sukari ebwanaaaa wachaaaaa kingine ni kiporo cha ugali wabaridiii na chai ya motoooo afu imekolea sukari hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We dada utakuwa na kitambi kikubwa kama mimba (nahisi tu) maana viporo na kitambi ni kama uji na mgonjwa
 
Kiporo cha maharage na kiporo cha kisamvu.
Lakini wali usiwe kiporo.
Kikweli mimi kiporo cha wali mhhhhhh.
Pia napenda sana kisamvu nilie na maharage.
Woiiiii vyote viporo utamu kunoga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwangu kiporo cha wali na maharage hakina mpinzani japo cha kisamvu nacho nakipenda ila kwa sasa kukipata ni tabu sana naishia kukisikia tu.
 
Hakuna cha kuzidi wali maharage wewe... halafu kwanza kanuni yetu sisi ni kwamba wali siyo kiporo

Kiporo nambari wani ni mbungu aka ngamunya aka dongo aka nguna aka bondo aka dona aka... taja jina lolote ulijualo lakini tutakutana pamoja tu kwenye UGALI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari ya leo wapenda kula mapocho pocho wenzangu.

Hivi kati ya kiporo cha wali na maharage/ wali ndondo na kiporo cha wali kisamvu (cha nazi au karanga) kipi kitamu?

Yaani nimeona niulize wala viporo wenzangu kwa sababu hapa namalizia kunywa chai na kiporo cha kisamvu yaani nimekaa chini kabisaa kwa utamu nikimaliza kupost uzi huu nashushia na juice ya embe, lol.

Nitapungua mwakani jamani😆😆

Hebu nambie kiboko yako ya kiporo ni ipi mwenzetu.

~MC~

Wali Maharage + Samaki wa Nazi + Chai ya Maziwa
 
Unajua unawatesa watu mtu mwingine mlo wake wa siku tu kuupata ni shida,mtu kama kiduku lilo ana siku ya tatu hajala,halafu unamuambia mambo ya viporo unadhani anakuonaje
 
Back
Top Bottom