Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Akili za Kiranga hazichunguziki mkuu, huyu ni miongoni mwa watu wenye uelewa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kuelezea mambo kwa marefu na mapana, huku yote yakiwa kwa ufasaha.
Nimemfatilia kwenye hu uzi, kilanga ni wa kawaida sana kumbe, anaweza kua mjuzi wa mambo mengine but kuhusu IMANI yake hi mpya hana majibu ya kuvutia kiviile kama ambavyo watu wengi wamemkweza, nimemsoma akibishana na jamaa mmoja, naona anaruka ruka tu. I am sorry, nilikua nadhania ni mjuvi sana haya mambo but bado sana, sema tu ana msimamo sana wa anacho kiamini but hawezi kukitetea ili kumshawishi mtu aamini anavyo amini yeye.
 

I lose interest really fast when debating people who seem to emrace ignorance.

Kwa nini unauliza "aliyeiumba" Milky Way?

Huoni swali lako limelenga kwenye jibu unalotaka?

Badalq ya kuuliza hela zinepoteaje, unaukuza Mchaga gani kaiba hela!

Unajuaje hela zimeibiwa? Na kamq zimeibuwa, unajuajw aliyeibq ni Mchaga?

Swali lako lenyewe linaonesha umeshajiaminisha kwamba hela zineibiwa na Mchaga, unataka kumjua Mchaga gani tu!

Kuhusu maswali yako ya post nqmba 584,
Nikishakuonesha kwamba Mungu wako hayupo, sitahitaji kukuonesha nani kaumba mto, kwa sababu, katika muktadha wa mjadala wa ku prove kuwepo kwa Mungu, njia nyingine yoyote ile ambayo mto utakuwa umetikea, njai hiyo si huyo Mungu ambaye hayupo.

Natumia namba kukueleza kwa uwazi zaidi.

Nikishakuonesha kwamba square root ya 2 ni kazima iwe ndogo kuliko 2, ni ujinga kuanza kuangqlia kama 3,4,5,6,7,8,9 na 10 zinaweza kuwa square roots za 2.

Unachofanya hapa ni kuniambia niangalie kama 3,4,5,6,7,8,9 na 10 ninsquare roots za 2.

Wakati nimeshakuonesha kwamba, square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko mbili, sehemu ya kutafuta jibu ni namba ndogo kuliko 2, si namba kubwa kuliko 2.

Wewe unalazimisha kutafuta square root ya 2 kwenye namba zilizo kubwa kuliko 2.

Hutapata jibu huko.
 
Sijawahi kusema mimi si kawaida.Na wala sihitaji unione wa kawaida.

Sina nia ya kupendwa, ningekuwa na nia hiyo nisingeweka such an unpopular worldview such as atheism here.

Mimi najali kujieleza.

Wewe umeshindwa ku spell "Kiranga" umeandika "Kilanga".

Mpaka hapo naona una matatizo ya kusoma na kufanya correct spelling, sasa siwezi kushangaa usiponielewa.

Mpaka sasa.

1. Hujathibitisha Mungu yupo.

2. Hujaeleza imekuwaje Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya mengi yanawezekana.
 
Following Hell and Heaven definitions ; and according to the Bible and religion, ninety-nine percent of the people that God created are going to hell. Only a few are going to be in heaven.

Why would an all powerful God of love burns people in hell forever ?

I would not want to be with someone that burns a cat, let alone someone that burns millions of people forever, [emoji3166].

No decent person would love such a God. It is either hizi dini zimekuwa metaphorically misunderstood au something is missing.

Dini yangu kama ya Uislam , asilimia 90 ni mafundisho ya kutishana na adhabu ya Kaburi, sijui moto wa Jahanam. Imepelekea watu wengi washindwe kuishi maisha na ku explore their inner secrets. It is sad but true.

I believe dini ni Mind Control tool or device to manipulate the human race. It takes a touch of genius and efforts to understand and see the ultimate truth.
-
Malheureusement and the worst part; dini nyingi zimejengwa katika mfumo wa violence and bloodshed......But still they can argue and justify the violence and bloodshed.... it is really sad to see such a thing.

Thanks to the civilization, otherwise hizi dini zinge create the hell on earth.

Two things are infinity ; The Universe and Man’s Stupidity .
 
It is interesting that Zeus and Isis sound a lot like Jesus. Just a coincidence?
 
Inafaa kunukuu aya za maandiko kama msingi unaojaribu kuthibitisha. Haifai kuinukuu kama ushahidi wa madai (kwa sababu ni madai).

Unaweza kuthibitisha hayo maandishi yamesema ukweli?
Ukweli unaoutaka ukoje na according to who?
 
1. Maandiko matakatifu ni chanzo muhimu cha ufunuo wa Mungu.
2. Watu wenye "fikira huru" ni watu gani hao na wamechaguliwa na nani ili wawe more credible kuliko watu wengine au fikira zao ndiyo zionekane zina uzito zaidi ya za wngine na kwa ground ipi?
3. 'Maandiko matakatifu' ni yale yanayohusu 'revealed truth about God'. Siwezi kusemea dini zingine, lakini mimi kama Mkristo Mkatoliki nasema Biblia ni chanzo muhimu cha ufunuo wa Mungu.
4. Matoleo ya biblia yako mengi kulingana na mahitaji ya watu na ukuaji wa msamiati wa mahali. Mfano, zamani kulikuwa na matoleo machache ya biblia kwa sababu lugha zilizotumika kutasfiri biblia zilikuwa chache na sasa ni mengi kulingana na lugha na watumiaji kuwa wengi pia. Kimsingi, biblia ni neno la Mungu lililoandikwa kwa lugha ya kibinadamu kwa kutumia misemo mbalimbali. Baada ya muda fulani lugha hubadilika - baadhi ya maneno na misemo huongezeka na mengine matumizi yake hupungua na hata wakati fulani kutoweka. Inapotokea kuna toleo jipya la biblia ina maana mabadiliko kama haya huzingatiwa, lengo likiwa kuwawezesha 'addressees' kupata ujumbe uliokusudiwa kwa kutumia lugha inayofahamika kwao au wanayoitumia kwa wakati huo.
5. Toleo la biblia halina maana nyingine nje ya tafsiri inayoendana na matumizi ya lugha inayotumiwa na 'addressees' (wale wanaoamini ujumbe wake).
 
Siyo to who

Kulingana na uhalisia wa hicho kitu

Unajuaje hayo maneno yamesema ukweli?
Maneno ya biblia ni kweli kwa sababu yametoka kwa vyanzo vinavyoaminika. Ni kama wewe unavyoamini scientific investigation fulani kutokana na kwamba inatoka kwenye chanzo unachokiamini na hivyo huna haja ya wewe kuanza investigation upya as if nothing has not been done in that area. We all take for granted certain truths to be true because we believe the sources are credible by established standards. For instance, if the earth rotates once in about 24 hours with respect to the sun, but once every 23 hours, 56 minutes, and 4 seconds with respect to other, distant, stars, I don't have to re-investigate it. I just trust the source and take it for granted that it is true. If each of the things has to be re-investigated over and over again life would been impossible. Imagine if each human being would have re-investigated to prove if the 'sun formed about 4.6 billion years ago from the gravitational collapse of matter within a region of a large molecular cloud' or 'that its core fuses about 600 million tonnes of hydrogen into helium every second, converting 4 million tonnes of matter into energy every second as a result'! So, we have to trust credible sources, but, of course, we shouldn't trust unreliable sources for any reason.
 
Unajuaje kua vimeumbwa na mungu na sio kitu kingine au vikawa havina muumbaji wala chanzo?

Pia kuna maelfu ya miungu inayoabudiwa na dini mbalimbali, kwanini mungu wako tu ndio awe muumbaji wa ulimwengu?
Kuna Mungu mmoja tu - transcendent being, the unmoved mover, the uncaused cause, the source of life and all existence. Maelfu ya hao miungu siyo Mungu ninayemwongelea. Hiyo miungu unayozungumzia haijaumba kitu na wala siyo source of life and existence na unaweza kuithibitisha wewe unayeiongelea siyo mimi.
 
1. Maandiko matakatifu ni chanzo muhimu cha ufunuo wa Mungu.
andiko lipi takatifu lililo takatifu zaidi au takatifu zaidi au la kweli zaidi: Biblia, Agano Jipya, Korani, Vedas, Avestas ????
 
2. Watu wenye "fikira huru" ni watu gani hao na wamechaguliwa na nani ili wawe more credible kuliko watu wengine au fikira zao ndiyo zionekane zina uzito zaidi ya za wngine na kwa ground ipi?
Mwenye fikra huru ni mtu asiye fungwa na mipaka kwenye kuhoji.

Mathalani kuna maswali ambayo mtu wa dini kafundishwa kua ni kufru kuhoji na ni dhambi itakayokupelekea uchomwe moto
 
3. 'Maandiko matakatifu' ni yale yanayohusu 'revealed truth about God'. Siwezi kusemea dini zingine, lakini mimi kama Mkristo Mkatoliki nasema Biblia ni chanzo muhimu cha ufunuo wa Mungu.
Kumbuka hapa tunazungumzia kitu kinachoitwa "maandiko matakatifu"

Na umedai kua maandiko matakatifu ni ujumbe moja kwa moja toka kwa mungu na huongea yaliyo kweli

Sasa Kila dini ina maandiko matakatifu

Kama kweli maandiko matakatifu husema kweli kwanini maandiko matakatifu ya dini yako yatofautiane na dini nyingine kwa kupingana wakati yote ni maandiko matakatifu?

Kwanini uone maandiko yako tu ndio yawe ya kweli na mengine siyo wakati nayo yanatambulika kama matakatifu?
 
Bado naona unakimbia kujibu swali, kama neno aliyeumba limekukwaza naliondoka naweka neno formation. Haya nipe formation ya hivyo nilivyokuuliza.

NB: Wajulishe pia na Atheist mwenzio Scars naona amepotelea hewani. Mtoe majibu hayo. Mnipe formation ya swali kwenye post #584
 
Umempa hoja nzuri sana...

Kwa msingi wa hoja yake, ina maana hata vitabu vilivyoandikwa na hao wanasayansi pamoja na kanuni ( formulars) zao, sio za kuziamini....
Hoja yake ni ya uongo.
Mkuu ndo maana nawaambia Atheism ni imani kama imani zingine, wao wanawaamini hao wanasayansi na vitabu vyao, vipi wamewahi kuwaona hao waliondika vitabu? vipi kama ni vya uongo?

Cha kuchekesha hao wanasayansi waliowapotosha waliondika hivyo vitabu, wamebase katika kuyaandika yale yote yaliyo katika time, space and matter ambayo muasisi na muumbaji ni Mungu ila wao wanajaribu kupotosha kwa kufuata imani yao Atheism ya kumkana Mungu na kusema kwamba ulimwengu haukuumba na Mungu na wanashindwa kuthibitisha kisayansi.
 
Naomba kurudia tena kutoa angalizo mnaojijua kuwa nyie ni Atheist na mnakana uwepo wa MUNGU muumba mbingu na nchi, msikimbie kujibu maswali. Tafadhali sana tunaomba mjibu maswali katika hoja tunazowapa kama na sisi tunavyojibu hoja zenu.

NB: Nahitaji majibu ya swali katika post #584, kutoka kwenu Atheist. Kama mnakana hakuna uwepo wa Mungu lazima mtakua mnajua chanzo cha vyote kama nilivyoanisha katika post #584.
 
Nimekueleza kwamba sihitaji kujua square root ya 2 ni ipi kujua kwamba 10 si square root ya 2, kama najua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na jibu la 10 lina contradict requirement hiyo.

Umeelewa huo mfano?

Unaelewa unachofanya ni kuniambia tutest kama 10 ni square root ya 2 na mimi nakwambia unatafuta jibu upande usiohusika, upande unaohusika ni ule ulio chini ya 2, kwa sababu upande ulio juu ya 2 wote hauwezi kuwa square root ya 2, una contradiction.

Nimekuonesha kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, kwa sababu uwepo wake unakuwa contradicted na dunia tunayoiona, kwa hivyo formation yoyote iliyosababisha jua, nyota, dunia, mito na mazagazaga yote uliyoyataja, ikiwa vyovyote vile, si Mungu huyo.

Kwa sababu Mungu huyo hayupo.

Nimejuaje kuwa hayupo?

Mungu huyo hayupo kama vile ambavyo hakuna binti fictional character wa miaka mitano mwenye mtoto wa kumzaa wa miaka sabini.

Binti wa miaka mitano hawezi kuwa na mtoto wa kumzaa mwenyewe aliye mzee wa miaka sabini.

Hiyo ni contradiction kubwa sana.

Sasa wewe unaniuliza, huyu mzee wa miaka sabini mama yake nani?

Mimi nakwambia hivi, hata nisipomjua mama yake huyo mzee wa miaka sabini, mama yake hawezi kuwa huyo binti wa miaka mitano. Kwa sababu huyo binti kazaliwa miaka 65 baada ya huyo mzee kuzaliwa, hivyo hawezi kuwa mama yake wa kumzaa.

Katika mjadala wa kutazama kama huyo binti wa miaka mitano ni mama wa kumzaa mzee wa miaka sabini, tukisha prove kwamba huyo binti hawezi kuwa mama yake huyo mzee, suala la nani mama yake huyo mzee ni irrelevant, kwa sababu hoja ni kama binti kamzaa huyo mzee, hoja si mama yake mzee ni nani.

Mimi hoja yangu ni Mungu hajauumba ulimwengu huu, kwa sababu hayupo. Hayo mengine ya nani kaumba galaxy au imetokeaje, mpaka leo wanasayansi wanayasoma na mengine hawajapata jibu la kumaliza mjadala.

Lakini hilo halifanyi jibu la Mungu lipewe nafasi ya kuweza kuwa jibu sahihi.

Kwa sababu, unaweza kutojua square root ya 2 ni nini, huna jibu kamili la swali, ukajua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko mbili, ukajua kwamba jibu la kwamba square root ya 2 ni 10 ni potofu.

Sasa mimi nimeshakuonesha kwamba dhana nzima ya uwepo wa Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ni potofu, kwa sababu ina contradiction. The problem.of evil contradicts the existence of such a God.

Hiyo ndiyo hoja yangu.

Wewe unarudi kwenye kujadili formation of galaxies.

Kama unataka kujua formation ya galazies chukua kozi ya astronomy, jifunze, kuna mengi hayajapata majibu mpaka leo na kila siku wanazuoni wanachapa papers.

Lakini jibu la Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote halipo katika majibu sahihi ya formationnof galaxies.

Kwa sababu ni jibu la aina ya "square root ya 2 ni 10". Liko upande mbaya wa contradiction.

Sasa, tafadhali usiniulize kama square root ya 2 ni 10, wakati tushajadili kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.

Ukiuliza hivyo nitatilia shaka uwezo wako wa kuelewa mambo.
 
Unathibitishaje kua yupo?

Wewe umejuaje na unahakika gani ya hicho unachokijua kua kipo sahihi na sio umepotoka tu?

Hata wewe unazungumzia sayansi inayosema 'jua liko stationary na dunia ndiyo inayozunguka' na naamini unazungumzia pia sayansi inayokubaliana na evolution, according to Darwin. Je, tuseme unapozungumzia saysnsi una'include' hata alternative theories to Darwinism such as Lamarckism, orthogenesis, saltationism, catastrophism and creationism? Ninapoongelea maandiko matakatifu naongelea maandiko yote matakatifu yanayoendana na revealed truths (according to the Bible) au yasiyopingana na biblical message. Hayo ya miungu wengine sina na wala sijawahi kuyaona na wala sina literature inayoonyesha hao miungu walivyoumba ulimwengu na how ni sources of life and existence.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…