Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kwanini unasema anacheza na akili zetu ?

Kwenye Uislamu,, Allah alisema kwamba atatupa majaribio ( test) ... Na shetani ni mojawapo ya njia Allah anatupa majaribio ya kiimani sisi waja wake
Kwenye akili yako hiyo ina make sense eti baba yako akuwekee nyoka aseme anakupa majaribio?

Hebu jiulize kiutu uzima
 
Huyo baba ananipa majaribio ya kitu gani ?

Tayari. Kwangu ina make sense
Kwani shetani nyie mnamchukuliaje? Kama rafiki anayetimiza majukumu yake aliyopewa na Mungu au mnamchukulia adui ambaye inatakiwa upambane naye?
 
Ni adui ambae tunapambana nae,, ambao huo uadui wetu ni kutokana na mpango wa Mungu...

Tukiwa tunaendelea na mjadala,, na mm nakuuliza huku...
Umeisoma Qur'an ? Unaijuaje Qur'an.? Ushaifuatilia ?
Yaani mkuu mimi nawaona hamjielewi.

Yaani unavyosema wewe ni kuwa Mungu alijitengenezea ufalme na akajitengenezea adui mwenye mamlaka sawa na yeye. Alafu anawahukumu kwa yeye kumruhusu huyo adui aishi na nyinyi.

Yaani hapa ni vichekesho. Ni sawa na wewe uoe mke wako alafu uanze kufanya majaribio ya kumtongoza. Akikukataa unamuacha kweli. Yaani ni utoto mtupu ambao nikijiuliza nakosa majibu kwanini hamshtuki...

Nimekuuliza swali ukajibu pasipo kufikiria. Unasema uwepo wa shetani kwenye ufalme wa Mungu ni mpango wa Mungu. Kwa jibu hili maana yake shetani sio muovu wala hastahili kuchukiwa kwakua anatekeleza majukumu aliyopewa na Mungu. Hivyo hana adhabu atakayopewa kwakua anatii maagizo
 
Bado hujanijibu,, huyo baba anataka kunipa majaribio ya kitu gani ?

Kule juu nilikwambia kuwa Allah anatupa waja wake majaribio ya kiimani.

Tusiache kitu,,
Majaribio ya wewe kung'atwa. Tena anakufungia kwenye chumba wewe na hilo joka lenye sumu kali
 
Hivi uwepo wa shetani kwenye ufalme wa Mungu ni mpango wa Mungu mwenyewe au ni kufeli kwa Mungu?
Ni mpango wa Mola muumba.

Umeulizwa zuri sana,kwamba umejuaje kama habari za Mungu ni hadithi za kutungwa,unetoa maelezo mengi mno ambayo hayakujibu swali hilo rahisi.

Ulitakiwa uambatanishe na ushahidi na utuambie ilikuwaje habari hizo zikatungwa na nani ni wa kwanza katika utunzi huo,maswali haya yalitakiwa tuyaone majibu yake katika ulicho eleza. Kusema ukagundua tu pasi na viambatanisho wewe ni haki yako kuitwa muongo na usiye jua kitu juu ya Mola muumba.
 
Yaani unavyosema wewe ni kuwa Mungu alijitengenezea ufalme na akajitengenezea adui mwenye mamlaka sawa na yeye. Alafu anawahukumu kwa yeye kumruhusu huyo adui aishi na nyinyi.
Hayo mamlaka sawa na yeye,yako wapi ? Jaribu kuhoji mambo kulingana na unachoandikiwa wala usizue. Yaani uwepo wa Shetani uwe katika mamlaka ya Allah,kisha kwa ujinga wako na upotoshaji udai adui huyo ana mamlaka sawa na Allah,hili umelipata wapi ?

Au hujui kama Allah amemlaani Shetani na atamchoma moto na ataishi humo milele ?
 
Ni mpango wa Mola muumba.

Umeulizwa zuri sana,kwamba umejuaje kama habari za Mungu ni hadithi za kutungwa,unetoa maelezo mengi mno ambayo hayakujibu swali hilo rahisi.

Ulitakiwa uambatanishe na ushahidi na utuambie ilikuwaje habari hizo zikatungwa na nani ni wa kwanza katika utunzi huo,maswali haya yalitakiwa tuyaone majibu yake katika ulicho eleza. Kusema ukagundua tu pasi na viambatanisho wewe ni haki yako kuitwa muongo na usiye jua kitu juu ya Mola muumba.
Nilitangulia kusema kwenye uandishi siko vizuri. Hivyo utanisamehe kama ujumbe au majibu yangu hayatakua ya kuridhisha
 
Mkuu umesema uwepo wa shetani ni mpango wa Mungu. Maana yake shetani anatimiza wajibu aliopewa na Mungu. Sasa amemlaani kwa kosa lipi.?
Kutimiza aliyoagizwa au kosa la shetani hapo ni lipi kama uwepo wake ulikua ni mpango wa Mungu?
 
Ni mpango wa Mola muumba.

Umeulizwa zuri sana,kwamba umejuaje kama habari za Mungu ni hadithi za kutungwa,unetoa maelezo mengi mno ambayo hayakujibu swali hilo rahisi.

Ulitakiwa uambatanishe na ushahidi na utuambie ilikuwaje habari hizo zikatungwa na nani ni wa kwanza katika utunzi huo,maswali haya yalitakiwa tuyaone majibu yake katika ulicho eleza. Kusema ukagundua tu pasi na viambatanisho wewe ni haki yako kuitwa muongo na usiye jua kitu juu ya Mola muumba.
Ni hadithi za kutungwa kwakua hazina uthibitisho. Zaidi ninachokiona kwenye vitabu vyenu vya dini ni vitisho vya maana.

Yaani huyo Mungu wenu yeye anatangaza adhabu tu tena kali ambazo ukifikiria kiundani unaona kabisa kuwa hapa unalazimishwa kuamini la sivyo utakutana na moto. Yaani ni vitisho mwanzo mwisho.

Tena vitabu vyenyewe vinasema adhabu ni baada ya kifo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Hapo pana mtego mdogo sana. Mwandishi aliwaza mbali akaona akisema ukiwa hai, haitawahi tokea. Akaona aseme baada ya kifo kwakua yeye au wao walikua wanajua maana ya kifo hivyo ukifa huwezi rudi kwenye uzima ukaja kutoa ushuha

Ni hadithi ambazo zilikua na lengo maalum ambalo mpaka sasa wamefanikiwa pakubwa sana
 
Bado hujanijibu,, huyo baba anataka kunipa majaribio ya kitu gani ?

Kule juu nilikwambia kuwa Allah anatupa waja wake majaribio ya kiimani.

Tusiache kitu,,
Alafu unasema Allah amewapa waja wake majaribio ya kiimani.
Sasa utasema huyo Mungu ni muweza wa yote kama imani yako tu mpaka aijaribu?!! Ina maana alikuumba pasipo na uhakika?

Kama alikua na uhakika na alichokiumba, majaribio ya kiimani ni ya kazi gani? Hapa wenye kutumia akili zao na sio za kushikiwa ndipo wanapohoji huo uwezo wa huyo Mungu wenu
 
Kivipi ?

Wapi nimesema amejitengenezea adui ? Mbaya zaid, huyo adui awe na mamlaka sawa Mola ? Wapi nimesema hvo

Huyo ni adui yetu,, Kwanini tusiishi nae ? Ikiwa yeye anatupa majaribio kupitia huyo adui..
Majaribio Allah anatupa kupitia njia nyingi,, ila mojawapo ni iblis ( mnamwita shetani)

Kwa akili yako kweli unaona huu mfano wako unafanana na kuhusu Mola kutuumba sisi ?
Kama ni akili yako imeona hvo,, basi sishangai kuona umefikia hitimisho la kukana uwepo wa Mola

Kwanini tusimchukie wakati ni adui yetu ?

Allah hakumpa maagizo hayo !! İblis mwenyewe ndie aliyeomba kufanya huo ushawishi..

Ngoja nikueleze kitu
Kwenye Uislamu,, Allah alimuumba iblis kutokana na moto,, iblis alikuwa anaishi pamoja na malaika, wote wakiwa wanamwabudu Allah...
Baada ya Allah kumuumba mwanadamu wa kwanza Adam,, aliwaita malaika wote pamoja na iblis kuja kumsujudia Adam... Malaika wote walitii amri ( malaika hawana free will ), isipokuwa iblis ambae alikataa , basi Allah akamfukuza kwenye Arshi yake kwa kosa la kuwa kiburi, na hvo kujikatia tiketi ya motoni moja kwa moja ... Lakini kabla iblis hajaondoka kwenye Arshi ya Allah alikuwa na ombi,, alimuomba Allah amruhusu aweze kuwashawishi viumbe wengine ( binadamu) ili aingie nao huko motoni ( asiingie peke yake) ... Allah akamruhusu... Yaliyofata ikawa historia,, Adam akawa binadamu wa kwanza kushawishiwa na iblis kufanya dhambi
Kwahiyo hii hadithi wewe inakuingia akili. Eti muasi akasema naomba nikawashawishi watu wa kuingia nao motoni?[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]. Dunia ya leo kweli na elimu zenu unadanganywa hivi? Zamani sawa....lakini mpaka karne ya sasa.? Mkuu kwa hadithi hii mimi naishia hapa
 
Ndio,, hakuna kitu ambacho kitatokea ila yeye ndo kakikadiria.

Wapi kasema Mungu amempa hayo maagizo huyo shetani ?

Hivi kuPlan kitu lazima uwe umetoa maagizo ?

Nimekuwekea kosa alofanya kwenye comment ya juu.

Kosa lake nimekuonesha kwenye comment ya juu
Samahani mkuu labda hukuelewa swali.

Nimeuliza hivi "uwepo wa shetani kwenye ufalme wa Mungu ni mpango wa Mungu au ni kufeli kwa Mungu"?

Yaani mpaka ile hatua shetani anaasi yaani hataki kutii maagizo ya Mungu mpaka akatolewa kwenye umalaika ilikua Mungu ndiye aliyepanga shetani afanye vile au Mungu alifeli kuumba kitu ambacho hakujua kitakuja kumuasi?

Labda hapa swali langu utakua umelielewa. Nijibu hapa alafu tutaendelea
 
Mkuu si tulikubaliana tokea mwanzo kuwa tunaenda kwa hoja...
Kanusha kwa hoja mkuu ( twende kama wasomi )....
Lete hoja, sio kuchekacheka

Halafu mbona kuna maswali yangu hujibu ?
Hoja gani mkuu naona unanifurahisha. Hivi mtu akuasi alafu akuombe achukue wanao uliohangaika kuwatengeneza na unakubali?

Hivi hii ni hoja kweli au ni utoto? Yaani unaona kabisa ni uongo uliojaa ujinga ndani yake. Huu mimi naita ni uvivu wa kufikiria
 
Wapi Mola amesema AMEHANGAIKA kututengeneza ?
Ndo maana Nilikuuliza, unajua lengo la kuumbwa mwanadamu ? Nijibu hili swali twende sambamba.
Mkuu umeshindwa kujibu swali langu ambalo ndio mwongozo wa kufunguliwa.

Kwakua umekosa jibu basi maana yake hapo hakuna Mungu. Kama angekuwepo na jibu lingepatikana.

Labda nikwambie tu kwa ufupi. Lengo la waliotuletea hofu ya maisha baada ya kufa lilikua ni kupoteza maana ya haya maisha halisi tunayoishi.

Walitutengenezea mfumo ambao walitaka tuone hakuna umuhimu wa kuwa hai bali kuna umuhimu baada ya kifo. Wakati huo wao walikua wanaandaa mifumo ya kuitawala dunia vizazi na vizazi.

Mimi sio mzuri kiundashi ila utanivumilia.

Leo hii nikikuambia ni kitu gani tunaweza tukawa tunajivunia huko duniani? Huwezi kunijibu. Zaidi zaidi utasema maisha ya hapa duniani hayana thamani. Hili ndilo lililokua lengo lao. Kuyatoa thamani maisha uliyonayo.

Hebu angalia nchi ambazo hizo dini zenu zilianzia. Si unaona kuwa ndio vinara wa utajiri na teknolojia ufanyaji biashara? Si unaona hata hali za kiuchumi za mataifa yao? Je, sisi???

Tumevumbua nini? Si wametutawala kimawazo na kimataduni? Si tumekua soko sisi..???

Kuna mengi sana ambayo huyajui..

Hatua niliyofikia mimi sio ya kujiuliza eti kuwa Mungu yupo au hayupo? Kwakua ninafahamu hakuna Mungu, basi hatua niliyofikia mimi ni kujiuliza umuhimu wa hizi dini kwenye mfumo wa maisha tulionao sasa.

Maana tumebaki kuulizana maswali ya kitoto
 
Nilitangulia kusema kwenye uandishi siko vizuri. Hivyo utanisamehe kama ujumbe au majibu yangu hayatakua ya kuridhisha
Ulitakiwa ujibu hoja hata kama uandishi siyo mzuri.
 
Mkuu umesema uwepo wa shetani ni mpango wa Mungu. Maana yake shetani anatimiza wajibu aliopewa na Mungu
Wajibu gani shetani amepewa na Allah ?

Kama hujaelewa jambo bora uulize kwanza. Shetani alikuwa ni katika viumbe wenye kufanya ibada sana,mpaka akapewa ofa na Mola wake na kuwekwa katika kundi moja na Malaika. Ila baadae akaja kuleta kiburi. Kwahiyo ulitakiwa ujue ilikiwake Shetani akalaaniwa ? Kwahiyo kujiona kwake yeye ni bora kuliko Adamu kulimponza.
Sasa amemlaani kwa kosa lipi.?
Kutimiza aliyoagizwa au kosa la shetani hapo ni lipi kama uwepo wake ulikua ni mpango wa Mungu?
Amalaaniwa kwa sababu alifanya kiburi na kukataa amri ya Allah.

Nikuulize wewe sasa,maana naona unairudia sana kauli ya "....aliagizwa.." aliagizwa na nani na umepata wapi habari hizi ?
 
Ni hadithi za kutungwa kwakua hazina uthibitisho. Zaidi ninachokiona kwenye vitabu vyenu vya dini ni vitisho vya maana.
Unajua kama huja hoja ? Thibitisha kwamba ni hadithi za kutungwa,una sema kwamba hazina uthibitisho ? Unaelewa unacho kiandika ?

Nithibitishie kwamba kweli hazina uthibitisho,na ili uthibitisho uwe uthbitisho kwako wewe unabidi ukidhi vigezo gani ?

Nani alikwambia kwamba hazina uthibitisho ?

Ushawahi kuisoma Qur'aan ? Thibitisha ukweli wa maneno yako kwa kutolea mfano kwenye Qur'aan.

Hadithi ni nini hasa ?
Yaani huyo Mungu wenu yeye anatangaza adhabu tu tena kali ambazo ukifikiria kiundani unaona kabisa kuwa hapa unalazimishwa kuamini la sivyo utakutana na moto. Yaani ni vitisho mwanzo mwisho.
Kwanza huwezi kufikiri kiundani juu ya maandiko ukaandika maneno haya,bali umefikiria juu juu.

Kitabu chetu ni muongozo,na kimeelezea njia ya ufaulu na kufeli. Hakuna kulazimishwa kuamini,ndiyo maana unaambiwa ukifanya mema unalipwa pepo na ukifanya uovu unalipwa moto,kwahiyo ni juu yako katika kuchagua.
 
Ina maana hujaliona jibu... Au ni kwamba jibu lipo tofauti na matakwa yako ?

Okay,, tufanye nimekosa jibu,, sasa kuna uhusiano gani kati ya Mm kukosa jibu na kutokuwepo Mungu ?

Nani hao waliotuletea hofu ya maisha ?
Jibu hili swali .... Kwanini unanishutumu mm kujibu maswali yako ingawa ww hujibu maswali yangu ?
Si unasema unatumia akili vzr,, Kwanini hujibu maswali? ,, hii inathibitisha kuwa akili mnayotumia haijitoshelezi

Akina nani hao ?
Mifumo ipi hio walitengeneza ?

Mm Nakuelewa vzr tu.

Umejuaje kuwa siwezi kukujibu ?

Hilo sio jibu langu...

Kama hilo ndo jibu lako kuhusiana na swali uliouliza mwenyewe, Basi napata mashaka sana na huko ulikosoma!!

Kwani walitukataza sisi kufanya hzo teknolojia na biashara.?
Kwahiyo watu wa hzo nchi wanajali sana maisha ya dunia kuliko huku ?

Inahusiana vp na dini na Mola ?
Kwani umekatazwa kuvumbua ?

Mpaka sasa hujathibitisha Kuwa Mungu hayupo...
Mbaya zaid hujajibu maswali yangu..

Kama umefikia majibu yake,, basi Jitafakari sana

Unakimbia maswali mkuu,, hujibu kabisa
Hivi unathibitishaje kuwa kitu hakipo wakati hakipo kweli?

Ingekua mimba tungechukua mkojo wa mwanamke tunayebishania alafu tukanunua kipimo tukapima.

Sasa Mungu nakuthibitishiaje wakati hayupo kweli?

Wewe ndiye uliyepaswa kunithibitishia. Sio kwa maneno bali kwa kutumia milango hii mitano ya fahamu.

Alafu kweli unaniuliza swali la sisi tumekatazwa na nani kuvumbua? Kweli hili ni la kuuliza?
Hii mifumo na tamaduni za maisha ya sasa ni athari ya wazee wetu kupokea tamaduni na mifumo waliyoletewa na wakoloni ambao hawakua na lengo la kutukomboa bali kututawala.
Hapa maana yake kuanzia mifumo ya kula mpaka kulala ni mifumo tegemezi ambayo haikupi wewe mwanya wa kuvumbua.

Hata mifumo ya elimu hailengi kukufanya uwe huru bali uwe mtumishi.

Ukiongezea na dini, basi muda tunaoupoteza kwenye kusali na kuabudu tunaona kawaida na tumapata thawabu wakati wenzetu wanafanya tafiti kila siku.

Wanatuletea mpaka virusi ambavyo tunabaki kuhangaika. Yote hiyo ni kuhakikisha wanaendelea kututawala.

Huwezi kuona haya kwakua umefungwa. Na ndilo lengo lao
 
Unajua kama huja hoja ? Thibitisha kwamba ni hadithi za kutungwa,una sema kwamba hazina uthibitisho ? Unaelewa unacho kiandika ?

Nithibitishie kwamba kweli hazina uthibitisho,na ili uthibitisho uwe uthbitisho kwako wewe unabidi ukidhi vigezo gani ?

Nani alikwambia kwamba hazina uthibitisho ?

Ushawahi kuisoma Qur'aan ? Thibitisha ukweli wa maneno yako kwa kutolea mfano kwenye Qur'aan.

Hadithi ni nini hasa ?

Kwanza huwezi kufikiri kiundani juu ya maandiko ukaandika maneno haya,bali umefikiria juu juu.

Kitabu chetu ni muongozo,na kimeelezea njia ya ufaulu na kufeli. Hakuna kulazimishwa kuamini,ndiyo maana unaambiwa ukifanya mema unalipwa pepo na ukifanya uovu unalipwa moto,kwahiyo ni juu yako katika kuchagua.
Wewe unaona hulazimishwi kwakua hujafikiria kiundani.
Hebu jiulize ukiwa mdogo, ulilazimishwa kusoma madrat au ulisoma kwa kupenda? Lengo la wewe kusoma madrsat lilikua ni nini?
Ulilishwa vitu ambavyo leo hii unaona ni kawaida kuwa navyo wakati hukustahili
 
Back
Top Bottom