Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Holy texts ndio uthibitisho?
- maandiko matakatifu (scriptures) yanasimlia kuwepo kwake na uumbaji wake na jamii yeyote ya watu inaamini (trust/certainty) kuwepo kwa Mungu ambaye anatajwa kwa majina mbalimbali - Mungu, Allah, Dieu, God, Namalenga, Nyamuanga, Lesa, Ngai, Mulungu etc. Hakuna 'traditional society' duniani ambayo haimini kuwepo kwa Mungu, ambaye kwa nyakati tofauti tofauti amehubiriwa na mababu na manabii mbalimbali (Musa, Ibrahimu, Isaya, Yesu, Mohamed etc) na watu mbalimbali wameshuhudia matendo makuu ya Mungu katika maisha yao tangu enzi na enzi na hadi leo. Haiwezekani wote hawa waseme uwongo as if walisemezana kabla simply kwa sababu sayansi haiwezi kuthibitisha walichoamini au wanachoamini na kukiishi.
Hoja hii au uthibitisho wa namna hiyo haukubaliki na watu wenye fikra huru na wala sio hoja ya kibusara kusimama kama uthibitisho
Hoja hii huanza kwa ku assume kwa kile ambacho inajaribu kukithibitisha, hii ni moja ya hoja dhaifu zilizowahi kutolewa katika kuthibitisha Mungu yupo.
Madai yenu ni kua Mungu lazima aweko kwa sababu maandiko yanasema hivyo. (Bibilia, Korani, Vedas, Avestas, n.k.)
2. Maandiko ni ya kweli kwa sababu yaliandikwa na Mungu au na watu walioongozwa kwa msaada wa mungu
3. Nani aliongoza watu hawa? (Mungu alifanya)
Swali
Kwa hivyo ni andiko lipi takatifu lililo takatifu zaidi au takatifu zaidi au la kweli zaidi: Biblia, Agano Jipya, Korani, Vedas, Avestas ????
Ni matoleo gani ya maandiko haya matakatifu yanayopaswa kuchukuliwa kama RASMI na matoleo ya kweli?
Katika tamaduni zote tatu za Magharibi: Uyahudi, Ukristo na Uislamu, kuna rekodi zinazoonyesha kwamba kulikuwa na tofauti juu ya maandishi hayo matakatifu Katika tamaduni zote tatu
Je wakati ukifika wakati jamii ikihitaji kuamua toleo rasmi itakuwa nini?