Kivipi ?
Wapi nimesema amejitengenezea adui ? Mbaya zaid, huyo adui awe na mamlaka sawa Mola ? Wapi nimesema hvo
Huyo ni adui yetu,, Kwanini tusiishi nae ? Ikiwa yeye anatupa majaribio kupitia huyo adui..
Majaribio Allah anatupa kupitia njia nyingi,, ila mojawapo ni iblis ( mnamwita shetani)
Kwa akili yako kweli unaona huu mfano wako unafanana na kuhusu Mola kutuumba sisi ?
Kama ni akili yako imeona hvo,, basi sishangai kuona umefikia hitimisho la kukana uwepo wa Mola
Kwanini tusimchukie wakati ni adui yetu ?
Allah hakumpa maagizo hayo !! İblis mwenyewe ndie aliyeomba kufanya huo ushawishi..
Ngoja nikueleze kitu
Kwenye Uislamu,, Allah alimuumba iblis kutokana na moto,, iblis alikuwa anaishi pamoja na malaika, wote wakiwa wanamwabudu Allah...
Baada ya Allah kumuumba mwanadamu wa kwanza Adam,, aliwaita malaika wote pamoja na iblis kuja kumsujudia Adam... Malaika wote walitii amri ( malaika hawana free will ), isipokuwa iblis ambae alikataa , basi Allah akamfukuza kwenye Arshi yake kwa kosa la kuwa kiburi, na hvo kujikatia tiketi ya motoni moja kwa moja ... Lakini kabla iblis hajaondoka kwenye Arshi ya Allah alikuwa na ombi,, alimuomba Allah amruhusu aweze kuwashawishi viumbe wengine ( binadamu) ili aingie nao huko motoni ( asiingie peke yake) ... Allah akamruhusu... Yaliyofata ikawa historia,, Adam akawa binadamu wa kwanza kushawishiwa na iblis kufanya dhambi