Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kati ya hayo ni lipi la ukweli zaidi au ramsi kuliko mengine?
Nimesema matoleo ni tafsiri inayotokana na mahitaji ya wakati na ukuaji wa msamiati na siyo tofauti ya ujumbe. Hivyo, matoleo yote yanalenga kitu kilekile. Ni kama researches mbalimbali za wanasayansi zinatolewa kwanza kwenye lugha zao na kisha zinatafsiriwa katika lugha mbalimbali kutokana na mahitaji. Hii haina maana kwamba kutakapotokea matoleo kadhaa then maudhui na maana ya utafiti fulani unabadilika na kumaanisha kitu tofauti na alivyosema mtafiti mwenyewe.
 
Mkuu kiranga unafahamu vipi kwa mifano yako kuwa square root ya 2 sio 10 na kwamba binti wa miaka mitano hawezi kumzaa bibi wa miaka 70 wakati kila kitu, kwa mujibu wako, kinatokea kwa chance?

Yaani kama huu ulimwengu wote ulitokea kwa mpasuko wa utupu kama mnavyosema atheists, ni namna gani kwa chance hivyohivyo huyo binti asiweze kumzaa huyo bibi?? Ulimwengu wenu nyie hauna consistency kwahiyo chochote kinawezekana.

Mungu yupo na ndio sababu hata wewe unaamini sheria zake za consistency.
 
sayansi haisemi kua imekamilika, na ndio maana inakosolewa.

So chochote ambacho sayansi imejaribu kukielezea na kukaonekana kuna mapungufu bado sio hoja, haikupi uhalali wa wewe kusema jambo hilo hilo kwasababu sayansi imeshindwa kujibu basi kwa namna nyingine ambayo sio ya kiuchunguzi wala uthibitisho jambo hilo ni kweli

Umeongelea maandiko matakatifu ila nimekuuliza swali hujanijibu

Kua maandiko yanayo daiwa kuwa ni matakatifu yako mengi kila dini inayo na kila moja wapo lina tofautiana na maandiko mengine

Islam wana QURA'N na hadiths na vyote hivyo ni maandiko matakatifu

Ukristo una BIBLIA, agano jipya, kale na yenye versions zaidi ya 5

judaism wana TANAKH ambayo ime contain vitabu vingine 24 (TORAH) vyote hivyo vikidaiwa kua ni maandiko matakatifu ambayo yameandikwa na mungu au watu walioongozwa na mungu

Swali langu ni je ni maandiko gani takatifu ambayo ni takatifu zaidi kuliko mengine?

Na kwanini hayo mengine yaitwe matakatifu wakati sio matakatifu?

Kama jibu litasema aina fulani ya maandiko matakatifu sio matakatifu, basi tutagundua kua maandiko kuitwa matakatifu sio kigezo cha kuthibitisha kua maandiko hayo ni matakatifu na yamesema ukweli

Hivyo basi tutarejea hapo kwenye hilo jibu lako ambalo umedai aina fulani ya maandiko ndio ya kweli na ni matakatifu, ututhibitishie kwasababu tushajua kua inawezekana hata hayo maandiko uliyoyachagua yakawa ni potofu kama hayo mengine uliyoyakataa

Kwa hiyo hapo tutakua tume bypass hoja ya kusema mungu yupo kwasababu maandiko matakatifu yamesema yupo, kwasababu tumejua kua maandiko matakatifu hayawezi kua ya kweli kama ambavyo umekataa maandiko kutoka dini zingine
 
Sayansi haijakamilia. Hivyo, unakubali kwamba unapoongelea sayansi unaongelea pia alternative theories to Darwinism such as Lamarckism, orthogenesis, saltationism, catastrophism and creationism?
 
vyanzo ambavyo umevithibitisha vipi?
Wewe ni lini ulithibitisha (kwa vipimo vipi ulivyotumia na ulivitoa wapi) kwamba umri wa dunia ni miaka bilioni 4.543 na the sun's core fuses about 600 million tonnes of hydrogen into helium every second, converting 4 million tonnes of matter into energy every second?
 
Sayansi haijakamilia. Hivyo, unakubali kwamba unapoongelea sayansi unaongelea pia alternative theories to Darwinism such as Lamarckism, orthogenesis, saltationism, catastrophism and creationism?
chochote ambacho sayansi imejaribu kukielezea na kukaonekana kuna mapungufu bado sio hoja, haikupi uhalali wa wewe kusema jambo hilo hilo kwasababu sayansi imeshindwa kujibu basi kwa namna nyingine ambayo sio ya kiuchunguzi wala uthibitisho jambo hilo ni kweli

hujajibu swali hili

Umeongelea maandiko matakatifu ila nimekuuliza swali hujanijibu

Kua maandiko yanayo daiwa kuwa ni matakatifu yako mengi kila dini inayo na kila moja wapo lina tofautiana na maandiko mengine

Islam wana QURA'N na hadiths na vyote hivyo ni maandiko matakatifu

Ukristo una BIBLIA, agano jipya, kale na yenye versions zaidi ya 5

judaism wana TANAKH ambayo ime contain vitabu vingine 24 (TORAH) vyote hivyo vikidaiwa kua ni maandiko matakatifu ambayo yameandikwa na mungu au watu walioongozwa na mungu

Swali langu ni je ni maandiko gani takatifu ambayo ni takatifu zaidi kuliko mengine?

Na kwanini hayo mengine yaitwe matakatifu wakati sio matakatifu?

Kama jibu litasema aina fulani ya maandiko matakatifu sio matakatifu, basi tutagundua kua maandiko kuitwa matakatifu sio kigezo cha kuthibitisha kua maandiko hayo ni matakatifu na yamesema ukweli

Hivyo basi tutarejea hapo kwenye hilo jibu lako ambalo umedai aina fulani ya maandiko ndio ya kweli na ni matakatifu, ututhibitishie kwasababu tushajua kua inawezekana hata hayo maandiko uliyoyachagua yakawa ni potofu kama hayo mengine uliyoyakataa

Kwa hiyo hapo tutakua tume bypass hoja ya kusema mungu yupo kwasababu maandiko matakatifu yamesema yupo, kwasababu tumejua kua maandiko matakatifu hayawezi kua ya kweli kama ambavyo umekataa maandiko kutoka dini zingine
 
irrelevant: hakuna sehemu nimedai dunia ina umri huo (kama ipo nioneshe)

Red herring (igorantio elench): Umeamua kujaribu kubadilisha mjadala kwa ku divert hoja yangu from the real question at issue to some side point.

Ni sawa na dosari iliyokea TRA ikionesha kuna utakatishaji fedha, baada ya ukaguzi wa CAG ikagundulika senetor ndio kataifisha hizo pesa.

Sheria inasema manager wa TRA anapaswa kushikiliwa kwa kosa la utakatishaji fedha. We unakuja kusema hata hivyo kuna ma manager wengi sana kwenye utawala wa mkapa waliofanya ufisadi kuliko huyu manager.

so?

Mafisadi wengine wanaweza wakawepo, but that it is another issue! The questions at hand are
1. Ni kweli manager alitakatisha fedha
2. Sheria inasemaje kwa kosa hilo
 
Nakuuliza hivyo kwa sababu kama wewe ni mwanasayansi au unaikubali sayansi basi utakuwa pia unakubaliana ni hizo 'established findings' kuhusu umri wa dunia au composition ya jua. Au kama hukubaliani nazo, basi sema ili nijue kuwa kumbe hata katika sayansi unayoikubali kuna findings ambazo bado hujajiridhisha nazo. Nakuuliza hivyo kwa sababu ni aina pia ya maswali unayoniuliza na ninataka nione wewe umeshafikia wapi katika kutafiti everything that constitutes science. Kama unasema ni irrelevant, basi hata wewe unaniuliza irrelevant questions. Basi kama ni hivyo, wote tunaulizana irrelevant questions.
 
Sijajibu ulichoniuliza au hujaelewa nilivyokujibu? Awali nilisema huwezi kutumia evidence ya sayansi kuongelea mambo ya Mungu kwa sababu ni kuongelea disciplines 2 tofauti zenye methodolojia tofauti. Mungu hawezi kuwa investigated scientifically na hivyo mambo yote yanayohusu Mungu huwezi kuya'establish' kwa kutumia methodolojia ya sayansi ambayo ndiyo wewe unayotaka nitumie. Haiwezekani.
 
Maswali yako unayoniuliza yako nje na mada (uminihusisha kua nimedai najua umri wa dunia) kimjadala hili ni kosa

Pili jibu lolote nitakalokupa halikupeleki kujua jibu la swali ambalo mimi nimekuuliza.

Kwanini unaizungumzia sayansi kwa kui refer negatively wakati hilo tulilimaliza tangu nilopesema kua sayansi haijatimia, haijui kila kitu na ndio maana inakosolewa?

Kusisitiza kwako kwa ku-point madhaifu ya sayansi kunafanya nione unatumia kama mwanya kuhalalisha habari zisizo thibitishika kua zikubalike tu bila ushahidi, kwasababu sayansi ilishindwa kuthibitisha jambo fulani

Turejee kwenye hoja yako: Maneno ya biblia ni kweli kwa sababu yametoka kwa vyanzo vinavyoaminika.

Swali: vyanzo ambavyo umevithibitisha vipi?
 
Sijui kwanini unajificha kwenye uvungu wa sayansi kitu ambacho mimi sijakutaka ukifanye?

Wapi nimedai unipe uthibitisho wa sayansi?

Mimi nataka uthibitisho wenye kuonesha ukweli usio acha shaka kutokana source ya habari kunadiwa kua imetoka kwa being mwenye amekamilika. Uthibitisho wowote ambao utakua na miscarriage itakya rahisi kwangu kuugundua na kubaini kua ni wauongo.
 
Kingine ambacho hujajibu

Umeongelea maandiko matakatifu ila nimekuuliza swali hujanijibu

Kua maandiko yanayo daiwa kuwa ni matakatifu yako mengi kila dini inayo na kila moja wapo lina tofautiana na maandiko mengine

Islam wana QURA'N na hadiths na vyote hivyo ni maandiko matakatifu

Ukristo una BIBLIA, agano jipya, kale na yenye versions zaidi ya 5. Halikadhalika nayo ni maandiko matakatifu

judaism wana TANAKH ambayo ime contain vitabu vingine 24 (TORAH) vyote hivyo vikidaiwa kua ni maandiko matakatifu ambayo yameandikwa na mungu au watu walioongozwa na mungu

Swali langu ni je ni maandiko gani takatifu ambayo ni takatifu zaidi kuliko mengine?

Kama jibu litasema aina fulani ya maandiko matakatifu sio matakatifu, basi tutagundua kua maandiko kuitwa matakatifu sio kigezo cha kuthibitisha kua maandiko hayo ni matakatifu na yamesema ukweli

Kama moja kati yao ni maandiko matakatifu, kwanini hayo mengine yaitwe matakatifu wakati sio matakatifu?

Hivyo basi tutarejea hapo kwenye hilo jibu lako ambalo umedai aina fulani ya maandiko ndio ya kweli na ni matakatifu, ututhibitishie kwasababu tushajua kua kama yaliyoitwa maandiko matakatifu tumeweza kujua ni uwongo basi inawezekana hata hayo maandiko uliyoyachagua wewe yakawa ni potofu kama hayo mengine uliyoyakataa

Kwa hiyo hapo tutakua tume bypass hoja ya kusema mungu yupo kwasababu maandiko matakatifu yamesema yupo, kwasababu tumejua kua maandiko matakatifu hayawezi kua ya kweli kama ambavyo umekataa maandiko kutoka dini zingine
 
Siyo lazima nithibitishe kila chanzo. Chanzo kinachoamininika sina sababu ya kukithibitisha tena maana hakiwezi kunidanganya. Mfano, naamini kwamba mafundisho ya Yesu kuhusu Mungu, uzima wa milele (salvation), upendo, uaminifu, kusameheana, kuwasaidia wenye shida nk ni ya kweli na sina mashaka yoyote. Na Yesu ni mmoja wa vyanzo vyangu ninavyoviamini hata bila kuthibitisha kauli zao kwa kuzifanyia utafiti upya. Vyanzo vingine ni mababu na manabii, mitume, watu wema na wanasayansi ambao wamefanya kazi yao kwa uaminifu na matunda ya kazi zao tunayafaidi wote hadi leo. Hawa wote nakubaliana na findings au maandiko yao waliyotuachia ya ama mafundisho (kama hao mababu na manabii) au scientific findings (kwa upande wa hao wanasayansi) au ushauri wa aina mbalimbali (watu wote wema wanaotoa ushauri unaweza kuwasaidia wengine). Kwa hawa wote sina sababu ya ku'doubt' kauli zao.
 
umethibitisha mungu yupo?
 
Maandiko yote ya kweli (ambayo ninayomaanisha) ni yale yana ujumbe unaounganisha jamii mbalimbali za watu, unaowafanya watu wawe wema zaidi, wawe karibu zaidi, wazidi kupendana, kusameheana, kusaidiana katika taabu na raha - kuwa ndugu/rafiki wa kweli - hata kama hawakuzaliwa pamoja au hawatoki sehemu/nchi/bara moja.
 
Siyo lazima nithibitishe kila chanzo. Chanzo kinachoamininika sina sababu ya kukithibitisha tena maana hakiwezi kunidanganya.
Nimebaini yafuatayo kwenye hoja yako

Kwamba unajiweka katika angle ya kukubali hata uwongo kwasababu kwako uthibitisho sio kipaumbele

Kwa mantiki hiyo hata kusema kwako kua hajadanganywa nako kutakua ni uwongo.
 
Ndiyo nakubali naweza kukubali wakati mwingine bila kujua hata uwongo na siyo mimi tu hata wewe kwa sababu by our very nature tunaweza kukosea au watu wengine kutukosesha. Lakini kwa upande wangu Mungu ananiongoza kwa mambo mengi na ingawa kuna mambo nimeshawahi kudanganywa na nitaendelea kudanganywa, lakini pia kuna mambo mengi sana ambayo nafanikiwa kuepuka kudanganywa na nitaendelea kufanya vizuri kama nitaendelea kumwamini Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…