Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Unasema mimi nimekariri theory.

Wewe unaweza kuthibitisha Mungu yupo kweli tujue habari zake si theory tu, tena ya uongo?
Kama hujakariri weka theory yako au version yako ya special or general relativity, according to Einstein . Mimi naweza kuongelea mambo ya Mungu kwa jinsi alivyonigusa (experience yangu) na kwa kutumia maneno yangu tofauti kabisa na watu wengine. Lakini wewe na wenzako hamwezi. Hamna uhuru wa kujadili kitu, isipokuwa kurudia rudia vitu ambavyo wengine walishavisema hata kama havileti maana au maana yake haieleweki.
 
Pole. Kumbe hata mchango wako huu hujauweka vizuri kwa kutokuwa mwandishi mzuri.
 
Ni kwanini mnahangaika sana kumtetea huyo Mungu? Hivi kama kweli angekuwepo na sifa zote anazopewa si angeshajitokeza japo kidogo tu kuonyesha nguvu zake?
Maana kiuhalisia Mungu kama yupo kweli, kwa jinsi dunia ilivyo basi huyu Mungu nimdhaifu sana ndio maana mnahangaika kutuaminisha kuwa yupo na ana uwezo wote,
 
Wewe wa kiume au wa kike ?
 
Kwa faida yako narudia tena,

NATHITIBISHA MUNGU YUPO NA KWA USHAHIDI WA UUMBAJI WAKE ALIOUFANYA, WA KUUMBA:-
Inafaa kusema kitu fulani kimeumbwa na mungu baada ya kutoa uthibitisho kuonesha mungu yupo, na sio sawa ku point kitu ambacho kipo kinacho thibitishika kua ndio uthibitisho wa kingine kisichothibitishika
1. Ulimwengu usioonekana kwa macho (The unlimited universe from time, space and matter)
Umeujuaje?

Unaweza kuthibitisha upo na sio hallucinations tu?
2. Ulimwengu unaoonekana kwa macho (The limited universe to time, space and matter)
-Hapa Mungu akaumba na kuudesign ulimwengu huu ukae vile alivyotaka yeye,
Cosmological argument

Sio wewe tu, hii hata aquinas ilimshinda
kama:-
. Sayari zote
. Jua, mwezi , vimondo na nyota zote
. Hewa/upepo, mawingu na mifumo mbalimbali ya misimu ya mvua na majira
Vinathibitishaje mungu yupo?
Mungu AKAITEUA SAYARI DUNIA NA KUIWEKEA MARIGHAFI RAFIKI KWA VIUMBE HAI VYOTE ILI WAISHI KATIKA SAYARI DUNIA.
Hapa umehubiri
Uumbaji alioufanya katika sayari dunia ni kama ifuatavyo:-
Uumbaji

hii habari umeipatia wapi?

Unaweza kuthibitisha uumbaji ulifanyika?

Vyote hivyo havithibitishi mungu yupo
. MWISHO MUNGU ALIMUUMBA BINADAMU KWA UPEKEE KULIKO VIUMBE WENGINE
Well, hii inatgemeana na namna unavyo define neno "upekee"

Watu walioumbwa na mungu mwenye uwezo wote tusingetegemea kuona kasoro ambazo zinaondoa sifa nzuri ya upekee.

Vilema, vipofu, viziwi, na wote waliozaliwa na magonjwa ya asili wanathibitisha kua hakuna intelligent being aliyetuumba kwa upekee
Binadamu alituumba kwa kutupa akili/utashi kwenye ubongo akili hii inatambua jema na baya na kusaidia kiumbe BiNADAMU kufanya maamuzi yake kwa kujitegemea.
Maamuzi yake kujitegemea unamaanisha freewill?

Kama ni freewill basi basically itathibitisha hakuna hayo maamuzi ya kujitegemea

Freewill ni hadithi kama ilivyo mungu
Aliumba binadamu waa kila aina e.g mchina, mwafrika, mhindi, mzungu n.k
So kwa mujibu wa source yako na mtazamo binafsi wa mungu, siku ya kwanza mungu aliumba watu wenye race zote?
Bado hujathibitisha mungu yupo
 
Hapa umejibu swali gani kati ya hayo niliyouliza??
😄😄😄
Kwa upeo wako unadhani katika ulicho uliza nastahiki nikujibu ?

Swali langu lina maana sana kuliko kuendelea kujadiliana na wewe.

Nakupa udhuru,nimegundua wewe ni mtoto wa kike,katika jambo gumu kwangu ni kujadiliana na mtoto wa kike juu ya mambo ya kielimu.

Ushauri wangu,endelea kusoma maoni ya wadau,kisha uchague unacho kiona kipo sahihi kwako.

Nipo ....
 
asante sisemi kua kipo kwasababu sina ushahidi kua kipo hivo kwangu ni hakipo, je waweza nithibitishia kipo ili nami nipate mwanga!?.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutokuwa na ushahidi haina maana ya moja kwa moja kuwa hilo jambo si la kweli au halipo, ukisema kabisa kuwa fulani hakipo maana yake una uhakika na sababu, huwezi kudai kitu fulani hakipo kwa sababu et hauna ushahidi wa kuwepo hicho kitu.
 
Wewe kama hujakariri tunga alphabwt yako tujue hujakariri.

Acha maneno ya kipumbavu.

Kitu chenye logic kitabaki kuwa na logic whether kimekaririwa au kimekuwa deducted na anayekisema.

Vivyo hivyo kwenye kitu kisichokuwa na logic.

Kwa hiyo, kukariri au kutokariri ni distraction tu.

Tuangalie logic.

Wewe unayekataa kukariri na kusema unamjua Mungu kwa experience yako, unaweza kuthibitisha yupo na hujamuota tu au hujajifariji kwa kujiaminisha tu?
 
Wewe unayekataa kukariri na kusema unamjua Mungu kwa experience yako, unaweza kuthibitisha yupo na hujamuota tu au hujajifariji kwa kujiaminisha tu?
Ndiyo. Mungu amenigusa na amenisaidia katika nyakati ambazo sikuwa na mtu wa kunisaidia. Nilipokuwa nimeshindwa kusamehe, nimeweza kusamehe, nilipokuwa nakosa upendo nimeweza upendo na hata kutotumia lugha inayoweza kuwaudhi wengine katika michango yangu ni kwa sababu ya Mungu. Nikisoma maandiko matakatifu napata inspiration na naona vitu kwa namna mpya na bora zaidi.
 
mzushi flani kwa kukusaidia kdg,, swali langu linasema hv " Qur'an ni maandiko ya nani ? “

Hapo nahitaji unitajie Mtunzi wa kitabu sio mwandishi... Tofautisha hivo vitu viwili

Kuhusu mwandishi wa Qur'an, hili swali itakuwa nimekuonea, bila shaka utakua hujui ( ndo maana umesema Muhammad SAW)...

“ Qur'an ni maandiko ya nani ? “

kwako ewe ndugu mzushi flani
 
umeuliza Qur an ni maandiko ya nani!? nimekujibu ya Muhammad, umekataaa jibu langu, hivyo wewe unatakiwa unipe jibu sahihi,

pia uniambie ni nani kaandika haya maandishi ya koran? maana umesema mohamedi hakujua kusoma wala kuandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ana matatizo ya macho kuwa naye makini

Nishawahi mpa hii link iliyojibu swali lake tena kwa muumini mwenzake kabla hata mjadala haujaamishwa jukwaa la dini akasema haoni kitu

 
Kweli Mkuu, hawana hoja wanawaamini wanasayansi ambao baadhi yao wamewakaririsha theories za kupinga uwepo wa Mungu kupitia imani ya Atheism. Bahati mbaya hao wanasayansi kuna mambo mengi wao wenyewe hawayajui na hawana majibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…