Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

TAMKO RASMI

Kwenu mnaojiita Atheist.
Nyie mnasema hakuna uwepo wa Mungu.

Kama hakuna uwepo wa Mungu lazima mtakua mnajua formation of the universe (ulimwengu) ulivyoanza na formation ya vitu vyote hivi vifiatavyo:-
Unasema uwepo wa mungu Ila hujafafanua Ni mungu yupi hapa. Wa wakristo, wa Islams, Buddha, Krishna, Jua, nk
Weka wazi kwanza hapa.

Halafu hayo yote yanathibitishaje uwepo wa mungu ? unaweza kuthibitisha?
 
unasema uwepo wa mungu Ila hujafafanua Ni mungu yupi hapa. Wa wakristo, wa Islams, Buddha, Krishna, Jua, nk
Weka wazi kwanza hapa.
Halafu hayo yote yanathibitishaje uwepo wa mungu ? unaweza kuthibitisha?
Namaanisha Mungu alieumba ulimwengu usioonekana kwa macho na ulimwengu huu unaoonekana kwa macho ambao tunaishi viumbe hai vyote katika sayari hii dunia na vyote vilivyomo kama wanyama, samaki, miti, jua, mwezi, nyota, binadamu n.k
 
Hujaona jibu kua ulimwengu hauna chanzi hapo?

Au ulijipanga na majibu yako ambayo yapo mfukoni?
Nimekuuliza hivyo vitu vimetokeaje(formation) maana vipo katika ulimwengu unaoonekana kwa macho (ulimwengu ambao chochote unachokiona lazima kiwe kimeundwa na muundaji) Ukisema ulimwengu hauna chanzo huo utakua ni muujiza, kitu ambacho nyie mnaojiita Atheist hamkubaliani nacho.

So bado nahitaji unipe majibu.
 
Hapana, kuna errors kwenye swali lako

Unaposema ulimwengu unao onekana una maanisha nini?

Hapo huoni kwamba unafanya comparison kwa vitu viwili ila kimoja hujakitaja?

Unaposema ulimwengu unao onekana unakua umefanya comparison na ulimwengu upi kujua utofauti kua huu unaonekana?

Ukisema ulimwengu unao onekana, tafsiri yake ni kwamba kuna ulimwengu mingine ambayo ipo na haionekani .

Sasa unapotaka swali lako lijibike kwa namna ambayo unataka wewe wakati mimi naona bado ni paradox kwasababu ya mjengeko wake hauko proper, utakua una feli
 
Haya kitu kingine kwenye hoja yako ambacho umekifanya kionekane cha lazima bila kufafanua huo ulazima kwanini uwepo

Umejenga hoja kwamba chochote kinacho onekana ni lazima kiwe kimeundwa, lakini hoja hii haijapitia facts haijapitia vipimo kuonesha umuhimu wa muundaji kwanini iwe ni lazima

Pia fact ya muundaji bado hujaielezea ipo katika state gani, visible au invisible, kwasababu kama naye muundaji ni visible tafsiri yake ni kwamba atahitaji muumbaji

Na kama sio invisible, hapimiki kwa kipomo chochote, hachukui nafasi (non matter) tutajuaje kua muundaji huyo yupo?

Tutathibitisha vipi kua formation ya vitu vimetokana na kitu ambacho huwezi kuthibitisha kipo?
 
Ulimwengu unaoonekana kwa macho namaanisha, unaweza kuona kwa macho yako wewe kama binadamu yaan unaweza kuona huyu ni samaki, haya ni matunda, ule ni mwezi, zile ni nyota n.k

Haya, naendelea kusubiri majibu.
 
Namaanisha Mungu alieumba ulimwengu usioonekana kwa macho na ulimwengu huu unaoonekana kwa macho ambao tunaishi viumbe hai vyote katika sayari hii dunia na vyote vilivyomo kama wanyama, samaki, miti, jua, mwezi, nyota, binadamu n.k
Uthibitisho unao?
 
Ulimwengu unaoonekana kwa macho namaanisha, unaweza kuona kwa macho yako wewe kama binadamu yaan unaweza kuona huyu ni samaki, haya ni matunda, ule ni mwezi, zile ni nyota n.k

Haya, naendelea kusubiri majibu.
Sasa huo sio ulimwengu, hivyo ni vitu vilivyomo ndani ya ulimwengu

Afu ina maana oxygen ambayo huiona unaiweka kwenye category gani hapo?
 
Mkuu, unaweza kunijuza kuna chochote katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho kinachoweza kuwepo bila kuwa na formation yake? /Muundaji
 
Sasa huo sio ulimwengu, hivyo ni vitu vilivyomo ndani ya ulimwengu

Afu ina maana oxygen ambayo huiona unaiweka kwenye category gani hapo?
Ndio ni vitu vilivyomo katika ulimwengu unaoonekana kwa macho

Wewe Scars ni kiumbe binadamu unaishi katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho lakini ndani ya mwili wako una hisia, hasira, upendo, stress je unaweza kuziona kwa mcho stress, hisia, upendo?
 
Nimefatilia arguments zenu nimeona kabisa mshikaji amekuzidi kete.

Maswali yake sensible lakin huyajibu, unaruka ruka tu.
Sikuwahi kujua kua huu mjadala una kamisaa, we uko humu kama jaji au kama mshiriki?

Huu mjadala tunaufanya ki fact, ni lazima utaona tofauti sana pale ambapo unataka kuufananisha na mabishano ya vilinge. Huku tunajua logical fallacy ni nini katika arguments

Mdau kauliza swali ambalo kajisetia jibu, kwamba ionekane kila kilichopo kina chanzo at the same time kuna dhana anayoishikiria na kudai haina chanzo

Sasa mimi sio mkurupukaji naelewa hiyo ni fallacy ya contradictory of special pleading, naelewa vyema opponent anatumia kwa lengo lipi na naelewa weakness yake ni ipi na ndio maana humuoni kujibu hoja ambazo zimelenga kuuliza swali lake hilo hilo.

Hiyo ni attempt anayoitengeneza opponent kwa kuset universal principle (kila kilichopo lazima kiwe na chanzo)

Ukisema kila kilichopo kina chanzo, hautafika mwisho kwamba kitu fulani ndio chanzo cha vyote, sasa weakness ya hoja hii ni pale ambapo anataka ku force ionekane kua kipo kitu ambacho ndio chanzo cha vyote na hicho kitu hakina chanzo.

Hapo tayari kaisha toka nje ya kanuni yake aliyoanza nayo (kila kilichopo lazima kwe kina chanzo)

Ni sawa na mimi niseme kila mtu aliyechangia kwenye huu mjadala ni mwizi, at the same time mimi najitoa kwenye list, kisha naanza kuwaita nyinyi wezi wakati na mimi nimechangia huu mjadala.

Kwa hiyo wewe utakubali kuitwa nwizi, kwasababu mimi nimetoa kanuni ambayo inaonesha watu wote humu ni wezi isipokua mimi?

Sasa wewe ulitaka nikurupuke kujibu kibubusa kwenye fallacy kama hiyo?
 
Kuna ulimwengu ambao hauonekani kwa macho?

Ndani mwangu sehemu gani ambapo stress zina kaa?
 
Wewe jamaa bana.

Unajidai kumix misamiati ya kiingereza kishenz. Kila maneno mawili, la tatu lazima uweke English vocabulary eti uonekane una the "highest reasoning capacity".

Pengine lengo lako ni umchanganye mshikaji umtoe kwenye reli.

Na yeye kumbe ni mjanja. Kila ukiruka ruka yeye hababaiki, anakazia urudi kujibu swali lake la msingi.

By the way, mimi ni mchangiaji kama wewe.
 
Ningependa unipe majibu ya swali nililokuuliza kwanza.
Mimi ndio nina kiu kali sana ya kutaka kujibu swali lako na ndio maana nakusisitiza hapa uondoe kwanza hiyo paradox ili swali lako liwe proper nilijibu ipasavyo kwasababu swali lako halijakamilika

Naomba ufafanue swali lako vyema, kama huelewi pakuanzia nitakuambia wapi ambapo swali lako halija kaa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…