Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Huwa namaliziaga na hii statement kama kuna mungu basi kitu cha karibu kufananisha na mungu ni jua maana bila jua viumbe vingi vitapotea kama sio kuisha vyote. So jua ni kitu kilichongia maisha sana humu duniani
Wewe sema tu unaamini mungu Jua basi,unaogopa nini sasa?
 
ulimwengu usioonekana wewe umeujua vipi, Nani kakwambia? Thibitisha kwanza mungu yupo
Kama wewe ni Atheist unasema hakuna uwepo wa Mungu, ni lazima utakua unajua hivyo vitu vimetokeaje. nimeuliza uniambie hivyo vitu vimetokeaje (formation) nahitaji majibu na sio kuzunguka. Jibu hoja hiyo kwanza.
 
Narudia tena kusema,

Ulimwengu unaoonekana kwa macho, ni huu ulimwengu tunaishi viumbe hai vyote na vitu vyake vyote ambavyo vingine sio viumbe hai, pia unaweza KUVIONA KWA MACHO YA KIBINADAMU (Yaani unaweza kuona mwezi, wanyama, madini, binadamu, ndege, samaki, gari, baiskeli, nyumba, meza n.k)

Katika ulimwengu huu kila unachokiona NI LAZIMA KIWE KIMEUNDWA NA MUUNDAJI, ni kwa sababu vitu vyote katika ulimwengu huu vilivyo hai na visivyo hai vipo limited to time, space and matter.

Kivipi?

Ili kuwe na matter ni lazima kuwe na space and time. Kitu(Matter) chochote ili kiwepo ni lazima kuwe na sehemu/nafasi(Space) ya kukiweka au sehemu kitakapokaa na muda(Time) wa hicho kitu kuundwa ili kiwepo/ ku-exist.

Hivyo, Gari ni Matter na gari lina formation yaani features/ingredients ambazo zimetumika kuliunda, ili gari liwepo ni lazima kuwe na space ya hilo gari kukaa na time ya hilo gari kuundwa, na yupo muundaji wa hilo gari. Hii ni scientifically.

Hivyo basi, HAKUNA CHOCHOTE(MATTER) KINACHOWEZA KUWEPO KATIKA SEHEMU(SPACE) YOYOTE BILA KUWA NA MUDA(TIME) WA HICHO KITU KUUNDWA NA MUUNDAJI.

MUUNDAJI NDIE ANAEUNDA KITU(Matter) KATIKA MUDA(Time) FULANI NA KUKIWEKA SEHEMU(Space) FULANI.

Hivyo, swali nililokuuliza ni vitu vinavyoonekana kwa macho nipo limited to time, space and matter. Haviwezi kuwepo bila kuundwa na muundaji.

NB: Nasubiri unipe majibu ya formation ya hivyo vitu nilivyokuuliza kwasababu unasema hakuna uwepo wa Mungu, basi ni lazima unajua na umejiridhisha hivyo vitu vyote unajua formation yake.
 
Mbona we unanipangia nijibu swali kwa namna ambavyo unataka wewe mi sisemi?

Utata nishakutajia uko wapi rudia kusoma post zangu
Hakuna sehemu niliyokupangia namna ya wewe kujibu, mimi nimeuliza swali nasubiri jibu.
 
Mkuu karibu, kama una majibu ya hilo swali yalete.
 
Swali 1 mpaka 4 imetokana na big bang, then gravitational force to hold things together ongezea some chemicalz reaction/ au physics on atomic fusion and atomic fission(radio activity)
kuanzia 5 kwenda chini evolution ndio imetengeneza hivyo vyote nimekupa kijuu juu nataka ukajisomee mwenyewe.
Ngoja nikupe namna ya kusearcg
1 formation of stars
2 formation of moon
3 formation of elements
4 what is life
5 what is natural selection
6 what is evolution.
Hayo maswali ukiyafanyia research utapata majibu ya maswali yako
 
Wewe sema tu unaamini mungu Jua basi,unaogopa nini sasa?
Nimesema kitu kilicho karibu na sifa za huyo mungu basi ni jua na bila jua maisha hapa duniani yangekuwa hayawezekani. At least jua naliona
 
Akili za Kiranga hazichunguziki mkuu, huyu ni miongoni mwa watu wenye uelewa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kuelezea mambo kwa marefu na mapana, huku yote yakiwa kwa ufasaha.
Kama Mungu mweza yote anachunguzwa, kuchambuliwa na kukosolewa, iweje huyo Kiranga? Kuna geniuses wanachunguzika, kuchambuliwa na kukoselewa pia. Yaani mwanadamu yeyote yule anachunguzika awe na uwezo mdogo sana au uwezo mkubwa sana.
 
Mwezi na wanyama ndio ulimwengu unao onekana?
 
Wewe ndio unijibu na sio mimi nikajisomee sasa itakua ni nini maana ya kuuliza swali?

Unasema 1 mpaka 4 imetokana na big bang, uniambie hiyo big bang ni nini? Imetokeaje? na imeform vipi hivyo vitu?

Uniambie pia hizo gravitational forces, chemical reaction, physics on atomic fusion and atomic fission ni nini? Zimetokeaje? Zilitokea tu kimiujiza na imeform vipi hivyo vitu?
 
hoja ya kwamba mungu yupo na hana chanzo imetumia principle gani?

Mimi sipingi wala sikubali kwasababu sijui, na ndio maana niko hapa kuhoji kwa wanao dai kua kilichopo kinaweza kuwepo bila chanzo, hapo wananipa tafsiri kua chanzo ni unnecessary kumbe hata ulimwengu tunaweza kuulezea vizuri bila chanzo
 
Kama umefikia hitimisho la kusema hakuna uwepo wa Mungu, sisi pia tunataka utujuze hivyo vitu(Hai na visivyo hai) vimetokeaje (formation) maana lazima unajua.
 
Na mimi niambie mungu ametokea wapi. Maana swali lako limeshajibiwa miaka mingi iliyopita ila nyinyi bado hamjaweza jibu mungu ametokea wapi
 
Na mimi niambie mungu ametokea wapi. Maana swali lako limeshajibiwa miaka mingi iliyopita ila nyinyi bado hamjaweza jibu mungu ametokea wapi
Unaponiambia limeshajibiwa miaka mingi bado sikuelewi, nijibu hapa Mkuu. Nijibu kwanza hiyo hoja yangu hivyo vitu vimetokeaje(formation)
 
Mwezi na wanyama ni vitu vilivyopo katika ulimwengu unaoneekana kwa macho, je wewe huwezi kuona wanyama au mwezi? Kwa macho yako.
Ulimwengu unao onekana kwa macho ni nini?

Umetaja wanyama na mwezi kua ndio mfano wa ulimwengu unaoonekana kwa macho, lakini upepo ambao hauonekani kwa macho hautakua sehemu ya huu ulimwengu siyo?

Upepo unaonekana kwa macho?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…