Narudia tena kusema,
Ulimwengu unaoonekana kwa macho, ni huu ulimwengu tunaishi viumbe hai vyote na vitu vyake vyote ambavyo vingine sio viumbe hai, pia unaweza KUVIONA KWA MACHO YA KIBINADAMU (Yaani unaweza kuona mwezi, wanyama, madini, binadamu, ndege, samaki, gari, baiskeli, nyumba, meza n.k)
Katika ulimwengu huu kila unachokiona NI LAZIMA KIWE KIMEUNDWA NA MUUNDAJI, ni kwa sababu vitu vyote katika ulimwengu huu vilivyo hai na visivyo hai vipo limited to time, space and matter.
Kivipi?
Ili kuwe na matter ni lazima kuwe na space and time. Kitu(Matter) chochote ili kiwepo ni lazima kuwe na sehemu/nafasi(Space) ya kukiweka au sehemu kitakapokaa na muda(Time) wa hicho kitu kuundwa ili kiwepo/ ku-exist.
Hivyo, Gari ni Matter na gari lina formation yaani features/ingredients ambazo zimetumika kuliunda, ili gari liwepo ni lazima kuwe na space ya hilo gari kukaa na time ya hilo gari kuundwa, na yupo muundaji wa hilo gari. Hii ni scientifically.
Hivyo basi, HAKUNA CHOCHOTE(MATTER) KINACHOWEZA KUWEPO KATIKA SEHEMU(SPACE) YOYOTE BILA KUWA NA MUDA(TIME) WA HICHO KITU KUUNDWA NA MUUNDAJI.
MUUNDAJI NDIE ANAEUNDA KITU(Matter) KATIKA MUDA(Time) FULANI NA KUKIWEKA SEHEMU(Space) FULANI.
Hivyo, swali nililokuuliza ni vitu vinavyoonekana kwa macho nipo limited to time, space and matter. Haviwezi kuwepo bila kuundwa na muundaji.
NB: Nasubiri unipe majibu ya formation ya hivyo vitu nilivyokuuliza kwasababu unasema hakuna uwepo wa Mungu, basi ni lazima unajua na umejiridhisha hivyo vitu vyote unajua formation yake.