Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kama umefikia hitimisho la kusema hakuna uwepo wa Mungu, sisi pia tunataka utujuze hivyo vitu(Hai na visivyo hai) vimetokeaje (formation) maana lazima unajua.
Wewe ulipofikia hitimisho kua mungu yupo ulitupa chanzo cha huyo mungu ni kipi?
 
Hivi mnavyotaka mthibitishiwe Mungu, huwa mnataraji nini katika huo uthibitisho yani mnataka muoneshwe huyo Mungu au ni kipi hasa ambacho mnakikusudia?
tumepewa akili na ufaham, sihitaj kukaririshwa eti sabab tu vitabu vimesema.
 
tumepewa akili na ufaham, sihitaj kukaririshwa eti sabab tu vitabu vimesema.
Nani tena aliyekupa akili na ufahamu?

Nachouliza ni kwamba tunamthibitishaje huyo Mungu yani tukakuoneshe huko aliko umuone mwenyewe au vp hasa huko kumthibitisha Mungu kunapaswa kuwa?
 
Wanaodai hivyo nadhani wanaona ni jambo ambalo kwa kutumia akili wanaona haliingi akilini kwamba kuweze kutokea na kitu pasina chanzo.
 
Ulimwengu unao onekana kwa macho ni nini?

Umetaja wanyama na mwezi kua ndio mfano wa ulimwengu unaoonekana kwa macho, lakini upepo ambao hauonekani kwa macho hautakua sehemu ya huu ulimwengu siyo?

Upepo unaonekana kwa macho?
Kama neno ulimwengu unaoonekana kwa macho linakuchanganya, ibakie neno Ulimwengu. Haya nipe majibu mkuu
 
swali gani?
Kwenu mnaojiita Atheist.
Nyie mnasema hakuna uwepo wa Mungu.

Kama hakuna uwepo wa Mungu lazima mtakua mnajua formation of the universe (ulimwengu) Formation ya vitu vyote hivi vifiatavyo:-

1. Sayari zote
2. Jua, mwezi na nyota zote
3. Bahari, mito na maziwa yote katika sayari dunia.
4. Gesi, mafuta na madini ardhini katika sayari dunia.
5. Samaki wa aina zote na viumbe vyote katika bahari, mito na maziwa.
6. Ndege wa aina zote
7. Wanyama wa aina zote
8. Binadamu
9. Miti ya aina zote, mimea na mbogamboga za aina zote

NB: Mtuambie hivyo vitu vimetokeaje, msikimbie hili swali.
 
Sasa hili swali nimelijibu labda kama unataka nilijibu tena na hapa

Formation ya vitu vyote vimeasisiwa na ulimwengu, ulimwengu ndio chanzo cha vilivyomo, ulimwengu hauna chanzo

Umenisoma?
 
Sasa hili swali nimelijibu labda kama unataka nilijibu tena na hapa

Formation ya vitu vyote vimeasisiwa na ulimwengu, ulimwengu ndio chanzo cha vilivyomo, ulimwengu hauna chanzo

Umenisoma?
Mkuu nimekuuliza unipe formation ya hivyo vitu vyote ambavyo vipo katika ulimwengu tunaoishi.

Unaniambia hivyo vitu vimeasisiwa na ulimwengu, huniambii ulimwengu umeasisi vipi na kuform hivyo vitu? Hivyo vitu vyote nilivyokuuliza ni Matter. Unipe facts how they formed scientifically.

Kwanini unipe facts scientifically kwasababu wewe hauamini katika miujiza, yaan ukisema ulimwengu umeasisi ni sawa na kusema hivyo vitu vimetokea tu kimiujiza without proof

Uniambie Ulimwengu umewezaje ku-form/kuunda vitu vyote hivi vifuatavyo:-

1. Sayari zote
2. Jua, mwezi na nyota zote
3. Bahari, mito na maziwa yote katika sayari dunia.
4. Gesi, mafuta na madini ardhini katika sayari dunia.
5. Samaki wa aina zote katika bahari, mito na maziwa.
6. Ndege wa aina zote
7. Wanyama wa aina zote
8. Binadamu
9. Miti, mimea na mbogamboga za aina zote
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Wewe ulishawahi kufa ukathibitisha kwamba ukifa ndipo unaona?
 
Sasa unajuaje kwamba huwezi wewe kwa ujinga wako tu, na kiukweli yupo, au huwezi kwa sababu hayupo?
Kama huwezi kitu siyo lazima kujua kama huwezi. Kwa mfano, ninapokuwa nimelala usingizi nyumbani usiku siwezi kwenda kufanya kazi ofisini wakati niko usingizini. Lakini sijui kama nikiwa nimelala usingizini huwa naenda kufanya kazi usiku ofisini.
 
Sasa unajuaje kwamba huwezi wewe kwa ujinga wako tu, na kiukweli yupo, au huwezi kwa sababu hayupo?
Kama huwezi kitu siyo lazima kujua kama huwezi. Kwa mfano, ninapokuwa nimelala usingizi nyumbani usiku siwezi kwenda kufanya kazi ofisini wakati niko usingizini. After all sijawahi kwenda kufanya kazi ofisini usiku. Lakini sijui kama nikiwa nimelala usingizini huwa naenda kufanya kazi usiku ofisini.
 
Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Wewe ulishawahi kufa ukathibitisha kwamba ukifa ndipo unaona?
Mtu kutoweza kuthibitisha au kushindwa kuthibitisha kuwa Mungu yupo siyo ushahidi kwamba hayupo. Mfano, wewe ukishindwa kuthibitisha kuwa nimeoa siyo ushahidi kuwa sijaoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…