Nimekueleza kwamba sihitaji kujua square root ya 2 ni ipi kujua kwamba 10 si square root ya 2, kama najua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2, na jibu la 10 lina contradict requirement hiyo.
Umeelewa huo mfano?
Unaelewa unachofanya ni kuniambia tutest kama 10 ni square root ya 2 na mimi nakwambia unatafuta jibu upande usiohusika, upande unaohusika ni ule ulio chini ya 2, kwa sababu upande ulio juu ya 2 wote hauwezi kuwa square root ya 2, una contradiction.
Nimekuonesha kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, kwa sababu uwepo wake unakuwa contradicted na dunia tunayoiona, kwa hivyo formation yoyote iliyosababisha jua, nyota, dunia, mito na mazagazaga yote uliyoyataja, ikiwa vyovyote vile, si Mungu huyo.
Kwa sababu Mungu huyo hayupo.
Nimejuaje kuwa hayupo?
Mungu huyo hayupo kama vile ambavyo hakuna binti fictional character wa miaka mitano mwenye mtoto wa kumzaa wa miaka sabini.
Binti wa miaka mitano hawezi kuwa na mtoto wa kumzaa mwenyewe aliye mzee wa miaka sabini.
Hiyo ni contradiction kubwa sana.
Sasa wewe unaniuliza, huyu mzee wa miaka sabini mama yake nani?
Mimi nakwambia hivi, hata nisipomjua mama yake huyo mzee wa miaka sabini, mama yake hawezi kuwa huyo binti wa miaka mitano. Kwa sababu huyo binti kazaliwa miaka 65 baada ya huyo mzee kuzaliwa, hivyo hawezi kuwa mama yake wa kumzaa.
Katika mjadala wa kutazama kama huyo binti wa miaka mitano ni mama wa kumzaa mzee wa miaka sabini, tukisha prove kwamba huyo binti hawezi kuwa mama yake huyo mzee, suala la nani mama yake huyo mzee ni irrelevant, kwa sababu hoja ni kama binti kamzaa huyo mzee, hoja si mama yake mzee ni nani.
Mimi hoja yangu ni Mungu hajauumba ulimwengu huu, kwa sababu hayupo. Hayo mengine ya nani kaumba galaxy au imetokeaje, mpaka leo wanasayansi wanayasoma na mengine hawajapata jibu la kumaliza mjadala.
Lakini hilo halifanyi jibu la Mungu lipewe nafasi ya kuweza kuwa jibu sahihi.
Kwa sababu, unaweza kutojua square root ya 2 ni nini, huna jibu kamili la swali, ukajua square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko mbili, ukajua kwamba jibu la kwamba square root ya 2 ni 10 ni potofu.
Sasa mimi nimeshakuonesha kwamba dhana nzima ya uwepo wa Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ni potofu, kwa sababu ina contradiction. The problem.of evil contradicts the existence of such a God.
Hiyo ndiyo hoja yangu.
Wewe unarudi kwenye kujadili formation of galaxies.
Kama unataka kujua formation ya galazies chukua kozi ya astronomy, jifunze, kuna mengi hayajapata majibu mpaka leo na kila siku wanazuoni wanachapa papers.
Lakini jibu la Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote halipo katika majibu sahihi ya formationnof galaxies.
Kwa sababu ni jibu la aina ya "square root ya 2 ni 10". Liko upande mbaya wa contradiction.
Sasa, tafadhali usiniulize kama square root ya 2 ni 10, wakati tushajadili kwamba square root ya 2 ni lazima iwe ndogo kuliko 2.
Ukiuliza hivyo nitatilia shaka uwezo wako wa kuelewa mambo.