Sikuwahi kujua kua huu mjadala una kamisaa, we uko humu kama jaji au kama mshiriki?
Huu mjadala tunaufanya ki fact, ni lazima utaona tofauti sana pale ambapo unataka kuufananisha na mabishano ya vilinge. Huku tunajua logical fallacy ni nini katika arguments
Mdau kauliza swali ambalo kajisetia jibu, kwamba ionekane kila kilichopo kina chanzo at the same time kuna dhana anayoishikiria na kudai haina chanzo
Sasa mimi sio mkurupukaji naelewa hiyo ni fallacy ya contradictory of special pleading, naelewa vyema opponent anatumia kwa lengo lipi na naelewa weakness yake ni ipi na ndio maana humuoni kujibu hoja ambazo zimelenga kuuliza swali lake hilo hilo.
Hiyo ni attempt anayoitengeneza opponent kwa kuset universal principle (kila kilichopo lazima kiwe na chanzo)
Ukisema kila kilichopo kina chanzo, hautafika mwisho kwamba kitu fulani ndio chanzo cha vyote, sasa weakness ya hoja hii ni pale ambapo anataka ku force ionekane kua kipo kitu ambacho ndio chanzo cha vyote na hicho kitu hakina chanzo.
Hapo tayari kaisha toka nje ya kanuni yake aliyoanza nayo (kila kilichopo lazima kwe kina chanzo)
Ni sawa na mimi niseme kila mtu aliyechangia kwenye huu mjadala ni mwizi, at the same time mimi najitoa kwenye list, kisha naanza kuwaita nyinyi wezi wakati na mimi nimechangia huu mjadala.
Kwa hiyo wewe utakubali kuitwa nwizi, kwasababu mimi nimetoa kanuni ambayo inaonesha watu wote humu ni wezi isipokua mimi?
Sasa wewe ulitaka nikurupuke kujibu kibubusa kwenye fallacy kama hiyo?