Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Mdau 1: hivi unajua kama kuna kuku mwenye miguu 4?
Mdau 2: Ahhh wapi haiwezekani kukawa na kuku mwenye miguu 4
Mdau 1: me ndo nakwambia sasa
Mdau 2: Thibitisha
Mdau 1: we amini Tu hivo mkuu
Mdau 2: anyway source ya habari yako?
Mdau 1: Trust me brother

Huo ni mfano wa watu ambao wanamtetea Mungu kuwa yupo, majibu Yao yamekaa kihisia Sana na sio uhalisia, cha ajabu Mungu hajawahi kujitetea mwenyewe juu ya uwepo wake Ila ajabu aliowaacha wamtetee majibu Yao ni mepesi sana

Binadamu tumekuwa na kasumba ya kutoa credits Kwa watengenezaji wa vitu vyote vizuri katika uso wa dunia, tunaangalia uumbaji wa dunia tunatoa sifa Kwa Mungu

Ukiangalia wajenzi wa majengo,magari,madaraja,vifaa vya umeme nk unaishia kutoa sifa Kwa mjenzi wa kitu husika, ata kama hujawahi kumuona utasema dahh huyu jamaa ni Noma Sana

Ila cha ajabu linapokuja swala la Mungu tunatoa Tu points kwake bila kutoa credits Kwa aliefanikisha uwepo wake, kama unaamini hakuna ambacho kinaweza kutokea Tu from no where na credits zote anapewa Mungu inakuwaje unaamini Mungu hajatokana na kitu?

Kama unaamini kuwa Mungu hajatokana na chochote iweje ushindwe kuamini kuwa wanyama,sayari,nyota,vyanzo vya maji,mimea kuwa vimetokea Tu from no where kama ambavyo Mungu ametokea?

Ni nani alietuaminisha kuwa dunia imeumbwa na Mungu Ila Mungu hajaumbwa na chochote? Ni sababu zipi za msingi ambazo ukimwambia mtu mwenye Akili timamu anaweza kukuelewa kuwa vitu vyooote vimeumbwa ila muumbaji ye ametokea Tu
 
Hujathibitisha hata mara moja.

Kama unabisha, weka link umethibitisha wapi.
Hili kwangu rahisi sana, nakuthibitishia tena, hapa. Kisha tuuchambue huu uthibitisho ninao kuwekea hapa.

Anasema Allah aliye juu, akiwajibu watu wa mfano wako :

34. Basi nawalete masimulizi kama haya ikiwa wao wanasema kweli.

35. Au wao wameumbwa pasipo kutokana na kitu chochote, au ni wao ndio waumbaji?

36. Au wao wameziumba mbingu na ardhi? Bali hawana na yakini. (at-Tur : 34 - 36)
 
Ila cha ajabu linapokuja swala la Mungu tunatoa Tu points kwake bila kutoa credits Kwa aliefanikisha uwepo wake, kama unaamini hakuna ambacho kinaweza kutokea Tu from no where na credits zote anapewa Mungu inakuwaje unaamini Mungu hajatokana na kitu?
Ngoja nionyeshe ujinga wako ulipo.

Naomba unipe sababu tano zinazo onyesha ulazima wa Mola awe ana chanzo.

Kisha uniambie je kuna infinity series ?
Ni nani alietuaminisha kuwa dunia imeumbwa na Mungu Ila Mungu hajaumbwa na chochote? Ni sababu zipi za msingi ambazo ukimwambia mtu mwenye Akili timamu anaweza kukuelewa kuwa vitu vyooote vimeumbwa ila muumbaji ye ametokea Tu
Hakuna mtu mwenye akili timamu mwenye kupinga uwepo wa Mola muumba, ukijiona unapinga hilo ujue huna akili timamu au unafikiria kitoto sana.

Kwanini nasema hivi ? Mola alivyo tuumba akatuwekea Fitrah (Innate disposition) hali wezekano ya kumkubali na kujua ya kuwa huu ulimwengu umeumbwa na unaendeshwa.

Mola muumba wa mbingu na ardhi na vilivyo yeye yupo wala hakuna kitu kabla yake wala hakuna kitu baada yake, hii ndiyo sifa ya muumbaji,hatakiwi kutanguliwa na wakati, bali yeye ndiye amumba wakati.
Mfano wako huu wa uongo, sababu mimi naamini juu ya uwepo wa Mola, ila siwezi kujenga hoja kijinga namna hii. Huu mfano unaingia kwa wakana Mungu wote, mfano wa mkana Mungu huyu aliyeanzishiwa hii mada, ukimuuliza kwanini unasema Mungu hayupo, anakujibu "Kwa sababu hayupo". Hili si jibu bali ni uoga wakujibu maswali.
 
Jana niliwaambia huku Kiranga Hakubaligi kushindwa,
Leo tena msilale hadi muonyeshe Mungu alipo
Usijali yeye atamaliza utata kwa kutuhakikishia kabisa kuwa Mungu hayupo huko panapoaminiwa kuwa ndio yupo huyo Mungu, tatizo anapoteza muda kuelezea kwamba Mungu hajaumba huu ulimwengu badala ya kutuhakikishia kuwa huyo Mungu hayupo.
 
Mungu hayupo au hajaumba huu ulimwengu? Maana umejikita kwenye issue ya Mungu kuumba huu ulimwengu tu na si kuumba binaadamu au vitu vyengine.
 
Unapowaza kwamba kila kitu kina mwanzo na mwisho unathibitisha kwamba nguvu inayoumba huo mwanzo na mwisho unatakiwa kuwa nje yake.

Mtengenezaji wa kitu chochote hakai ndani yake kama sehemu ya material za uundaji.

Vivyo hivyo Mungu yupo nje ya mfumo huu wa mwanzo na mwisho. Yeye yupo tangu milele hata milele.
 
Mkuu Bahati mbaya sijaandika comment/mawazo yangu ili kubishana na mtu na ndomana sija quote mtu yoyote Yule

Na bahati mbaya zaidi ata nikisema nianze kubishana na wewe utanisumbua Tu bure huna facts, kuna baadhi ya wenzio at least waga wanajenga hoja

Kwa kuangalia vile unajenga hoja na kujibu maswali ya wadau we ni mweupe sana kichwani, kwahiyo itahitaji niwe mweupe zaidi yako Kichwani ili kuendana na uelewa wako. Endelea Tu na kiranga me nilikuwa napita Tu
 
Mkuu umemaliza Ngoja Sasa waamini Mungu wakija na hoja Zao
Ooooh swala la Mungu ni Imani!
 
Shukrani.

Hivi ndivyo nilivyo mimi.
 
Hii ni nini? [emoji23]
 

Ungekuwa unafahamu nadharia za origin of universe na life usingejenga hoja duni hivyo

Ungekuwa unajua sifa za SPIRITUAL BEING pia usingejenga hoja duni hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…