Kiranga anatoa sadaka na anaamini stori za majini lakini haamini uwepo wa Mungu

Swali zuri.

Nina vigezo vitatu.

Weka hoja ambayo ina clear and logical evidence, haiwezi kuwa contradicted na haina logical inconsistency kuhusu uwepo wa Mungu tuichambue.

Mpaka sasa, hoja zote kuhusu uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hazina clear and kogical evidence, zina contradiction na logical inconsistencies.

Karibu, nakusubiri.
Vigezo hivyo ni subjective. Nataka objective metrics.
 
The problem of evil contradicts the existence of that God. It proves that God does not exists, by contradiction.

Do you understand that?

Kuwezekana kwa mabaya popote pale, kunathibitisha Mungu huyo hayupo popote pale.
Haujatuhakikishia kuwa hayupo huko tunapoambiwa kuwa yupo, sijui hata kama unaelewa?
 
Wewe unaupenda ujinga kubaki nao.
Ujinga unao wewe unayeamini kuwapo kwa Mungu ambaye huwezi hata kumuelezea.

Nakuuliza kwa nini Mungu kaumba ulimwengu unaowezekana kuwa na mabaya wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, unajibu swali tofauti, eti Mungu ana uhuru wa kuumba vyovyote.

Sawa, tuseme ana uhuru, sijabishia hilo.

Lakini, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana na hakuumba ulimwengu huu uwe hauwezekani mabaya?

Huwezi kujibu.

Unakubali uwepo wa Mungu usiyemuelewa.

Hapo wewe si mjinga kweli?
 
Inshort Kiranga hana fact

Anashindwa kujibu maswali kibao kwasababu atajifunga 😂😂

Kakimbia maswali kibao ya Kadari1
(Mheshimiwa Kadari1 MUNGU akubariki sana )
Kwa mfano
Akili ni nini ?
Na unaweza kuthibitisha akili zipo ?

Inshort watu wote wanamsifia kiranga ni kama wanachama wa sisiemu tu .🤣🤣
Nisameheni jamaa anajipigiaga wajinga wajinga
 
Nimemuuliza Mungu hilo swali lako naye amejibu kuwa ameumba ulimwengu huu jinsi ulivyo kwasababu anatupenda sana na anatupa nafasi ya kumchagua yeye katikati ya changamoto ili kupitia msaada wake basi yeye apate kuwa na utukufu.

Hata hivyo tayari ameshaweka siku atakapokomesha dhambi na uasi wote duniani.

Sasa mimi nakushangaa wewe unayenibishia kwamba Mungu hayupo wakati sasa hivi hapa nilikuwa naongea naye. Ni mfalme mkuu lakini pia ni rafiki wa karibu.
 
Muulize kama anatupenda sana mbona wana wanateseka sana mtaani?

Kwani alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mateso?

Mwambie Kiranga kasema mbona hapo kuna longolongo?

Halafu mwambie mbona ana upendeleo anakutokea wewe tu wengine hatutokei? Huo upendo gani wa kupendelea watu kwa ubaguzi?

Mimi sitaki kuongea naye kupitia kwako mwambie aje ajioneshe kwangu hapa nijue yupo kweli sio wewe unaona yupo kwa ugonjwa wa akili tu.
 
Inshort Kiranga hana fact

Anashindwa kujibu maswali kibao kwasababu atajifunga 😂😂

Kakimbia maswali kibao ya Kadari1
(Mheshimiwa Kadari1 MUNGU akubariki sana )
Kwa mfano
Akili ni nini ?
Na unaweza kuthibitisha akili zipo ?

Inshort watu wote wanamsifia kiranga ni kama wanachama wa sisiemu tu .🤣🤣
Nisameheni jamaa anajipigiaga wajinga wajinga
Mkuu afadhali wewe umeona. Jamaa ni mweupe kichwani japo anajiona anajua.

Katumia maneno: hisia na akili. Namuuliza hisia ni nini? Umewahi kuziona? Akili ni nini? Umewahi kuziona? Anaishia kukimbia maswali.

Anajua akiyajibu hayo amekamatwa kwasababu hivyo vyote vipo ila huwezi kuviona wala kuvishika. Unavithibitisha kwa kuona matendo au results zake.

Vivyo hivyo tunajua Mungu yupo japokuwa hatuwezi kumuona kwa macho na kumshika.
 
Muulize kama anatupenda sana mbona wana wanateseka sana mtaani?

Kwani alishindwa kuumba ulimwengu ambao hauwezekani kuwa na mateso?

Mwambie Kiranga kasema mbona hapo kuna longolongo?

Halafu mwambie mbona ana upendeleo anakutokea wewe tu wengine hatutokei? Huo upendo gani wa kupendelea watu kwa ubaguzi?

Mimi sitaki kuongea naye kupitia kwako mwambie aje ajioneshe kwangu hapa nijue yupo kweli sio wewe unaona yupo kwa ugonjwa wa akili tu.
Watu wanateseka kwasababu ya ujinga wao. Mungu mwenyewe anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Ni jukumu la kila mmoja anayekutana na changamoto mbalimbali kutafuta majibu katika elimu either ya kiroho au hii ya madarasani.

Mungu anazungumza kila siku na mamilioni ya watu ambao wamependa kumfahamu kwa unyenyekevu na uchunguzi. Kwasababu hiyo hachagui wala hapendelei.

Kama ni shauku yako kumfahamu kama ulivyoandika pale kwenye aya ya mwisho basi wala usiwe na wasiwasi. Utatuletea mrejesho siku sio nyingi kwamba umekutana na Mungu pamoja na uzuri wake.

Anakupenda sana na analo kusudi zuri kwa ajili ya maisha yako.
 
Weka hoja ambayo ina clear and logical evidence, haiwezi kuwa contradicted na haina logical inconsistency kuhusu uwepo wa Mungu tuichambue.
Unakubali kwamba "contradiction" pia huwa inasababishwa na ujinga wa mtu husika ? Yaani kulingana na upeo wako kuwa ndogo ukaona hilo jambo lina tatiza ?

Sasa kwa minajili hiyo, usilazimishe sharti (logical evidence) dhafu kuwa kama marejeo. Tunataka uhalisia ndiyo uhukumu baina yetu. Usilete sanaa na mawazo ya watu kama kigezo cha kuhukumu jambo wakati huo uhalisia uko wazi.

Kingine hujawahi kuwa na uwezo wa kuichambua hoja inayo muelezea Mola, sababu unatumia msingi dhaifu kujengea hoja zako.
Mpaka sasa, hoja zote kuhusu uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, hazina clear and kogical evidence, zina contradiction na logical inconsistencies.
Hii siyo kweli, sababu wewe unapinga bila hoja na hukosoi hoja sababu huna uwezo huo.

Nini namaanisha hapa, hapa namaanisha huyo Mola unaye mjadili humjui,vipi upatie katika kumuongelea ?
 
Watu wanateseka kwasababu ya ujinga wao. Mungu mwenyewe anasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Ni jukumu la kila mmoja anayekutana na changamoto mbalimbali kutafuta majibu katika elimu either ya kiroho au hii ya madarasani.

Mungu anazungumza kila siku na mamilioni ya watu ambao wamependa kumfahamu kwa unyenyekevu na uchunguzi. Kwasababu hiyo hachagui wala hapendelei.

Kama ni shauku yako kumfahamu kama ulivyoandika pale kwenye aya ya mwisho basi wala usiwe na wasiwasi. Utatuletea mrejesho siku sio nyingi kwamba umekutana na Mungu pamoja na uzuri wake.

Anakupenda sana na analo kusudi zuri kwa ajili ya maisha yako.
Kwa nini Mungu kaumba ulimwengu ambao ujinga unawezekana kuwapo, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao ujinga hauwezi kuwapo?
 
Nina mazwali mengi, ila hujafuzu kusikia mengine.

Jibu hilo kwanza.

Sasa wewe ni mtu wa kukuuliza maswali ya juu wakati hili la chini kabisa hujaliweza?
Utakaponiambia akili ni nini na wapi umewahi kuziona then hapohapo utapata uthibitisho wa uwepo wa Mungu.

Hata hili la hisia ni nini? Umewahi kuziona? Hujalijibu. Unakimbiakimbia tu.
 
Unakubali kwamba "contradiction" pia huwa inasabaishwa na ujinga wa mtu husika ? Yaani kulingana na upeo wako kuwa ndogo ukaona hilo jambo lina tatiza ?

Sasa kwa minajili hiyo, usilazimishe sharti (logical evidence) dhafu kuwa kama marejeo. Tunataka uhalisia ndiyo uhukumu baina yetu. Usilete sanaa na mawazo ya watu kama kigezo cha kuhukumu jambo wakati huo uhalisia uko wazi.

Kingine hujawahi kuwa na uwezo wa kuichambua hoja inayo muelezea Mola, sababu unatumia msingi dhaifu kujengea hoja zako.

Hii siyo kweli, sababu wewe unapinga bila hoja na hukosoi hoja sababu huna uwezo huo.

Nini namaanisha hapa, hapa namaanisha huyo Mola unaye mjadili humjui,vipi upatie katika kumuongelea ?
Hujalathibitisha Mungu yupo.

Hujachambua hoja yangu yoyote.
 
Back
Top Bottom