Liutenant
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 590
- 899
- Thread starter
- #341
Hapa twende kwenye baselines. Mimi Mungu simwamini kinadharia tu, nimemwona kwenye maisha yangu mara nyingi sana.Unajuaje Mungu hajaweka wazi na si kwamba Mungu hayupo?
Kama Mungu hayupo, halafu mtu akaamua tu kujudanganya akakwambia Mungu hajulikani wazi kwa sababu kaamua kutojiweka wazi kwa sababu zake, ukaamini hilo, utajuaje ukweli kwamba Mungu hayupo wakati umetanguliza imani potofu?
Unajuaje hatujui sababu za Mungu kuumba ulimwengu unaoruhusu dhambi kwa sababu Mungu kaamua kutoziweka wazi, na si kwa sababu Mungu hayupo?
Kama unaamini uwepo wa Mungu usiyemuelewa vizuri, unajuaje kwamba huyo Mungu yupo kweli na habari za uwepo wake si hadithi za watu tu tumedanganyana kwa sababu zetu za kidunia hii tu?
Kimsingi Mungu anaeleweka kirahisi sana mara baada ya kumwamini. Zamani nilikuwa napata changamoto maswali ya namna hii yanapoulizwa na yale ya waislamu kuhusu Yesu. Ilikuwa doubtful moment.
Lakini nikaamua kumuomba Mungu anipe ufahamu kuhusu yeye. Nilifanya study ya dini hizi mbili kubwa hapa Tanzania. Nikapata ufahamu wa kuelewa namna ambavyo Yesu ni Mungu, nikaelewa kuhusu the trinity of God, nikaelewa kuhusu the righteousness of God, the love of God, ukuu wa Mungu, msamaha wa dhambi na hata uzima wa milele.
Mimi ninakuunga mkono kuhoji na kujiuliza maswali haya na mengine mengi. Ni watu wachache sana wanapata nafasi ya namna hii. Actually hata waislamu wanapohoji na ku doubt ninawaelewa.
Ila kwa uzoefu wangu, utapata majibu ikiwa moyoni unayodhamira ya dhati kupata majibu. Unyenyekevu utawezesha kupata ufahamu. Unaweza kuomba sincerely from your mind kwamba kama Mungu yupo basi ajidhihirishe kwako.
Nina uhakika atakupa ufahamu kumjua kama kweli unapenda kumjua.