Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Kirusi kinachotisha kuliko Corona ni uoga/ hofu

Huu ndo ukwel usiofichika watz wengi wetu ni waoga wa kiwango cha dangote cement.

Imagine leo watu wanakufa kona mbalimbali za nchi lakini no media inayotupasha habari zaidi zaidi wanatupasha mambo yasio na msingi,hiki ndo kipindi wananchi wanahitaji habari zaidi kuliko vipindi vyote(endelea kubisha huo ndo ukweli).

Ukifuatilia kiundani utagundua kila media iko busy na vitu vingine kuliko kutafuta data za kinachoendelea ili precautions za kutosha zichukuliwe.

Jana nilipata bahati ya kumsikiliza wakili msomi kuna kitu aliongea kuhusu wanahabari,yaani kuna kitu kinaonekana hakipo sawa juu ya taarifa zinazoletwa na viongozi na uhalisia uliopo mitaani,wengine kwenye media flani wanapinga juu ya maelezo ya msando tena wao wako dar msando yupo Arusha.

Kwa kumalizia nani alitupa uogo na hofu tulizonazo sasa??!!

#coronaisreal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wasipokuwa na hofu ya korona hawatatia maanani maelekezo ya kujikinga, ndiyo madhara yake inasambaa kwa kasi hasa baada ya kuonyesha mfano mbaya wa kwenda kanisani kipindi cha korona. Hofu ndiyo inaweza kukuokoa, tunanawa kwa ajili ya hofu au sio!
Kwenu wamekufa wangapi kwa maambukizi yaliyosababishwa na maombi ya rais Magufuli??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS
 
Kwenu wamekufa wangapi kwa maambukizi yaliyosababishwa na maombi ya rais Magufuli??

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua ujinga ni mbaya kuliko umasikini? Fikiria vyote pamoja nchini kwetu! Unafikiri sie tunaabudu Mungu tofauti na wa Vatican na Makkah? Wao wamefunga kila kitu kwa sababu wana akili na busara na kujua Korona hachagui aina ya mikusanyiko na watu wameambukizwa kwenye mihadhara ya kidini.

We unasikiliza serikali iliyosema Korona haiambukizwi kwa pumzi ghafla wanataka wote tuvae Barakoa wakati kuna kiwanda kimoja tu nchini cha Barakoa na kipo Mbeya?

Kwa taarifa yako Korona ipo zaidi ya serikali inavyosema, na imesambazwa kwenye mikusanyiko yote hata ya kidini, ngoja uone baada ya wiki hii itakavyokuwa mikoani.

Walioanzisha dini wamefunga madhehebu na misikiti, siye tunaoenda kwa waganga wa kienyeji na kujilinda na ndumba na kujifanya kusali ni nani???
 
Tuishinde hofu Watanzania, mabeberu na viongozi wa dini msitutie hofu kwa kuacha vitabu vya dini na kufuata yao. Kwa maana hata shetani anatumia viongozi wa dini kutekeleza yake.
Tuchape kazi...
Mungu Ibariki Tanzania
 
Mimi nitaendelea tu kuchukua tahadhari dhidi ya hili janga, mwanzo mwisho! Sijafarijika wala kushawishika kwa ile hotuba fupi ya Mh. Rais.
 
Back
Top Bottom