Kisa cha kutafakarisha na kufikirisha juu ya Kikwete na Kagame

Kisa cha kutafakarisha na kufikirisha juu ya Kikwete na Kagame

Watanzania kwa ubishi wenu hamtaamini. Aminini jeshi lenu lina uwezo mkubwa sana.
Naam mimi nakuamini kabisa na niseme kuwa binafsi nakuelewa sana. Jeshi letu ndiyo bora sana Afrika nzima kwa kila kitu. Ndiyo maan Raisi alifanya busara sana kuwaachia JWTZ washughulikie swala la korosho. Namshauri kama akiweza alipe jeshi mamlaka liwashugulikie hawa wapinzani wanaotumiwa na mabeberu, najua vijana wetu wakakamavu kutoka TISS na JWTZ wanaweza kuingia hata pale Brussels bila kuonekana na wakaondoka bila hata kuonekana.
 
Halo JF siasa.

Niende madani hapo juu.

Ktk kipindi cha mwaka 2013 hadi 2015 kulikuwa na mgogoro wa kibinafsi na baadae kiinchi kati ya wababe Rais Kikwete na kagame wa Rwanda. Kiini cha mgogoro ni ushauri wa Jk kwa Pk juu ya waasi wa FDLR.

Sasa kutokana na mgogoro wao huo kila moja alipanga kumwonesha mwenzie yeye nani. Kikwete akatuma kikosi maalumu cha makomando kutoka Tz na kuingia Kigali usiku wa manane na kuiteka nyumba anayolala kagame na walifanikiwa kwa asilimia 100% kuingia ktk jiji hilo bila kutambulika.

Baadae kikosi hicho tiifu kilivunja milango na kuingia ndani ambapo walimkamata Rais kagame ambapo aliamua kwa huruma ya kutoweshwa usiku huo kumwomba Jk msamaha kwa njia ya simu huku makomando wa Tz wakisimama chumbani mwake.

Baadae Jk alimwambia mkuu wa operesheni kuwa wamwache na warudi nyumbani na akamwambia kagame kuanzia siku hiyo azibe mdomo wake vinginevyo atajuta.

Nyumba hiyo ya kagame ipo mitaani Kigali na sio Ikulu kwani kagame amegoma kuishi ndani ya Ikulu tangu awe Rais kwa sababu ajuazo yeye. Wakati hayo yakijiri walinzi wote wa nyumba walikuwa washamalizwa na kikosi kazi hicho kabla ya kuingia viunga vya nyumba hiyo ya Rais wa nchi ndogo inayoibuka kiuchumi na kitechnolojia kwa kasi kwa sasa.

Ee Mola tunashukuru kwa Busara zilizotumika kipindi hicho vinginevyo...........
Hivi ni kweli kagame hatumii ikulu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu....Really?!

April mosi bado lakini naona kama umisahau.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Naam mimi nakuamini kabisa na niseme kuwa binafsi nakuelewa sana. Jeshi letu ndiyo bora sana Afrika nzima kwa kila kitu. Ndiyo maan Raisi alifanya busara sana kuwaachia JWTZ washughulikie swala la korosho. Namshauri kama akiweza alipe jeshi mamlaka liwashugulikie hawa wapinzani wanaotumiwa na mabeberu, najua vijana wetu wakakamavu kutoka TISS na JWTZ wanaweza kuingia hata pale Brussels bila kuonekana na wakaondoka bila hata kuonekana.

Hahah umetisha sana mkuu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom