Kisa cha kweli kilichompata braza akijitafuta kuelekea Msumbiji

Kisa cha kweli kilichompata braza akijitafuta kuelekea Msumbiji

Objective football

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2023
Posts
1,195
Reaction score
2,771
Part:1
Sisi jinsia ya kiume ,tunapitia mengi sana katika harakati za kupata unafuu wa kiuchumi na kusimamia familia bora.

kwa ukanda wetu sisi wakusini age ya 18- 24 unaweza ukawa ndio umri ambao unakumbatia starehe karibia zote ikiwemo pombe na totozi.

lakin 25+ aiseeh vijana wengi huanza kuondoka maskani, kama wameoa basi huaga familia zao na kwenda kutafuta maisha mijini na nchi za watu.

niende kwenye stori moja kwamoja.

mnamo mwaka 2012 kuna mabraza zetu wanne(4) waliondokaga mtaani kwetu wote kwa wakati mmoja.

moja ya chanzo watu wengi kuulizia kuondoka kwao mtaani kwetu ilikua ni vipaji vyao vya soka.alikuepo bro ima(mido) ngasa(striker) shikokoti(striker) na huyu jamaa braza fumo huyu ndio chanzo cha kuleta stori hii hapa na ndie alieleta mrejesho mtaani kuhusu kilicho wasibu katika harakati za kupeleka mzigo huko msumbiji.

its so sad champs, ilikua mida ya sa 12 jionii natoka mashineni kusaga mahindi. nakuta wanafamilia wanalia ,washikaji huku macho ya watu wengi yakimlenga mtu mmoja ambae kadri nilivokua nasogea niliona kama ni mtu ambaye kama namfahamu. ndiyo nikajiridhisha kuwa ni braza fumo !!
je kipi kimemsibu huko alikoenda pamoja na wenzie! hayo yakawa maswali yangu pamoja na wanajamii wote kwa sikuile!
 
Part1 :B
Braza fumo rangi ya mwili wake ilibadilika, weusi wote ulipotea akawa kama wa kijivu huwezi amini kwamba ni yeye.

klabu yetu ya mpira ikajichanga na kuenda kuwaona wazazi wa fumo kwa chochote kitu tulichobarikiwa . basi tukapeleka michango then na kumjulia hali fumo, kwa kipindi kile alikua sio mtu wa mazungumzo marefu na sisi, zaidi ya salamu .

anakusalimu then anaendelea na kupumzika kitandani , hakika wadau mbalimbali ambao fumo alikua akishiriki katika kuchezea klabu zao kwenye ndondo,ngazi ya mkoa na malawi waliweza kujitokeza pale homu kumshika mkono jamaaa na kumjulia hali.

na hata wazazi wa akina shikokoti, ngasa,ima walipatwa na wasiwasi sana ila kwa hali ya braza fumo walishindwa kuambulia dodoso yoyote kuhusu uwepo wao. kwani hali yake hikua sio nzuri
 
Part 2:
ikapita miezi mitatu, fumo akaanza kupata nafuu nakutoa shuhuda kilicho wasibu katika harakati za kupeleka mzigo wa bosi wao msumbiji kupitia bahari ya hindi.

nina mnukuu" tulikua tunapeleka mafuta msumbiji kwa boti ndogo kuelekea mji wa maputo, tulikua watu saba ndani ya boti.

safari ilianza salama,huku bosi wetu akiwa ametulipa advansi ya mzigo huku kiasi kingine akihidi kutulipa baada ya mzigo kufika salama msumbiji!
 
Sema nowdays jf imekumbwa na wasaka attention.
Yale mafunzo dizaini kama yanapotea hivi, na mods hawaunganishi posts za mleta uzi ndo inaua zaidi.

Uzi kama huu mtu akiusoma ile post ya mwanzo, anaupuuza akiamini jamaa haendelei kumbe chini upo, na sio rahisi kuscrow reply zaidi ya 100 ili kupata muendelezo.

Nyie waleta story jitahidi kuleta full story kama kweli mnataka wadau wajifunze ila kama unataka followers basi endeleeni na huo upuuzi wa vipande buku.
Moderator jitahidini kuunganisha muendelezo wa stories zenye mafunzo, waanzisha story(waandishi/wasimuliaji wengi hawjui namna ya kuunganisha).
 
Enhee ikawaje .....? Endelea
nimeifupisha sana, nitaimaliza sehemu ya mwisho watu
Sema nowdays jf imekumbwa na wasaka attention.
Yale mafunzo dizaini kama yanapotea hivi, na mods hawaunganishi posts za mleta uzi ndo inaua zaidi.

Uzi kama huu mtu akiusoma ile post ya mwanzo, anaupuuza akiamini jamaa haendelei kumbe chini upo, na sio rahisi kuscrow reply zaidi ya 100 ili kupata muendelezo.

Nyie waleta story jitahidi kuleta full story kama kweli mnataka wadau wajifunze ila kama unataka followers basi endeleeni na huo upuuzi wa vipande buku.
Moderator jitahidini kuunganisha muendelezo wa stories zenye mafunzo, waanzisha story(waandishi/wasimuliaji wengi hawjui namna ya kuunganisha).
mkuu kimeo kilizima chaji, umeme wa mgao huku niliko
 
part3:

naendelea kumnukuu"'safari ilianza salama mimi na washikaji zangu ,huku tukiamini kuwa tutafikisha mzigo salama msumbiji na hatimae na kupewa kiasi chetu chote cha fedha.

safari ilikua ndefu sana ,baadhi tulipitiwa na usingizi mzito sana,huku boti bado ikiendelea kukata maji marefu kuelekea msumbiji, wengi tuliamini hili dili linaenda kubadili kabisa taswira ya maisha yetu, bado tukaendelea kukata maji salama salimini"

nitaimaliza leo leo wakuu
 
Back
Top Bottom