Kisa cha kweli kilichompata braza akijitafuta kuelekea Msumbiji

Kisa cha kweli kilichompata braza akijitafuta kuelekea Msumbiji

Sema nowdays jf imekumbwa na wasaka attention.
Yale mafunzo dizaini kama yanapotea hivi, na mods hawaunganishi posts za mleta uzi ndo inaua zaidi.

Uzi kama huu mtu akiusoma ile post ya mwanzo, anaupuuza akiamini jamaa haendelei kumbe chini upo, na sio rahisi kuscrow reply zaidi ya 100 ili kupata muendelezo.

Nyie waleta story jitahidi kuleta full story kama kweli mnataka wadau wajifunze ila kama unataka followers basi endeleeni na huo upuuzi wa vipande buku.
Moderator jitahidini kuunganisha muendelezo wa stories zenye mafunzo, waanzisha story(waandishi/wasimuliaji wengi hawjui namna ya kuunganisha).
Wamekuwa ma dj afro
 
Part:1
Sisi jinsia ya kiume ,tunapitia mengi sana katika harakati za kupata unafuu wa kiuchumi na kusimamia familia bora.

kwa ukanda wetu sisi wakusini age ya 18- 24 unaweza ukawa ndio umri ambao unakumbatia starehe karibia zote ikiwemo pombe na totozi.

lakin 25+ aiseeh vijana wengi huanza kuondoka maskani, kama wameoa basi huaga familia zao na kwenda kutafuta maisha mijini na nchi za watu.

niende kwenye stori moja kwamoja.

mnamo mwaka 2012 kuna mabraza zetu wanne(4) waliondokaga mtaani kwetu wote kwa wakati mmoja.

moja ya chanzo watu wengi kuulizia kuondoka kwao mtaani kwetu ilikua ni vipaji vyao vya soka.alikuepo bro ima(mido) ngasa(striker) shikokoti(striker) na huyu jamaa braza fumo huyu ndio chanzo cha kuleta stori hii hapa na ndie alieleta mrejesho mtaani kuhusu kilicho wasibu katika harakati za kupeleka mzigo huko msumbiji.

its so sad champs, ilikua mida ya sa 12 jionii natoka mashineni kusaga mahindi. nakuta wanafamilia wanalia ,washikaji huku macho ya watu wengi yakimlenga mtu mmoja ambae kadri nilivokua nasogea niliona kama ni mtu ambaye kama namfahamu. ndiyo nikajiridhisha kuwa ni braza fumo !!
je kipi kimemsibu huko alikoenda pamoja na wenzie! hayo yakawa maswali yangu pamoja na wanajamii wote kwa sikuile!
Nitarudi
 
Hivi mtu.haweza andika akamaliza akaweka uzi mmoja akaendelea na mambo yake?!

Sioni sababu ya mabandiko mengi ya hadithi/visa vya maisha kuwa na vipengele viiingi.
 
Shusha Vitu....Story nzuri ila uwasilishaji wako sasa unapunguza utamu maana inabidi mtu atulie ndoo ataelewa kuna sehemu unataka kutufikisha na kutufunza
mkuu mm niko mnadani muda huu, watu wa dsm mnakuja kununua kila aina ya mifugo huku site aka kanda ya kati
 
Part:4

Braza fumo akiwa mtu aliyepoteza nuru kabisa akaendelea na simulizi yake iliyojaa kusudi la kufanikiwa na mateso makubwa waliyo kumbana nayo .

Namnukuu "' Safari ilikua ndefu sana , nikamwamsha shikokoti achukue kiroba tulichohifadhia vyakula vyetu ndani ya safari hii ya kuusaka utajiri ndani ya boti hii inayokata mawimbi kuelekea msumbiji. shikokoti ,kokoti mwanangu amka tuishi! basi shiko akaamka akiwa katika mudi ya usingizi mzito , akachukua kiroba cha menyu tukaaanza kula ndani ya safari hii, huku kaubaridi kakianza kukolea katika mwili wangu.

nikavaa sweta jingine la pili, angalau hapa nikapata nafuu ya baridi hii ndani ya bahari ya hindi.
wakati tunakula msosi dogo ngasa alikua kalala fofofo huku akiweweseka usiku ule akimtaja mama ake kwa kilugha kwa lugha yetu ya kiswahili alikua akisema hivii " mama yangu najua nikombali nawewe ,ila nitarudi na mali kubadili hio hali ya nyumbani naomba uwasalimu wadogo zangu na yule mkamwana wako emmy".

nitaimalizia leoleo wakuu.
 
Back
Top Bottom