Kisa cha kweli, mbingu ipo na moto wa jehanamu upo

Kisa cha kweli, mbingu ipo na moto wa jehanamu upo

Haahaaaahaaa acha kamba wewe hizo hadithi na ngano za wayahudi na wayunani wa kale bado unaziamini wewe mmatumbi uliyekulia namtumbo?
Ifike mahari tuseme basi sasa wenzetu huko Yuropa na amerika hizo mambo walishazipuuzia kitambo baada ya kuona hazina uhalisia katika jamii zao kilichobakia ni kuzitumia kupiga pesa kwa kisingizio cha misaada ili wazidi chota mali!
 
Vipi kuhusu dini zingine mkuu tusahau maswala ya mbingu(pepo).

Haswa uarabuni, uchina, na n.k
Yakobo 1:26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Yakobo 1:27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
 
Haahaaaahaaa acha kamba wewe hizo hadithi na ngano za wayahudi na wayunani wa kale bado unaziamini wewe mmatumbi uliyekulia namtumbo?
Ifike mahari tuseme basi sasa wenzetu huko Yuropa na amerika hizo mambo walishazipuuzia kitambo baada ya kuona hazina uhalisia katika jamii zao kilichobakia ni kuzitumia kupiga pesa kwa kisingizio cha misaada ili wazidi chota mali!
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
 
Ni kweli lakini paradiso ndo wanaenda kwa sasa ambapo ni huko huko mbinguni, 2 Wakorintho 5:1 Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. 2 Wakorintho 5:2 Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; baada ya ufufuo au mwisho wa dunia wakati wengine wanaenda kwenye ziwa la moto ( ufunuo 21;8) na watakatifu wanaenda kuishi mji wa Yerusalem mpya
Sasa umeanza kuelewa kidogo maandiko yalivyo. Nakushauri ongeza bidii kusoma maandiko na uzishike Amri za MUNGU naye atakupa "hekima, akili na ufahamu" wa NENO lake.
 
Huwezi kutenganisha mbingu na Yesu, Yesu ni wa mbinguni na mbinguni ni makao ya Yesu
Hayo ni yako na imani yako uliyolishwa, sisi tunauliza kwenye hicho kisa unachodai ni cha kweli na yaliyojiri maana umegusa imani za watu hivyo usilete janja janja ya kujificha kwenye mistari ya Bible kila unapoulizwa huo mkasa.
 
Yakobo 1:26 Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai. Yakobo 1:27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Bado sijapata jibu kiongoz! Tusahau mbingu au inakuwaje ?
 
hivi kwanini tunaamini au tunaminishwa malaika ni viumbe wazuri na wana muonekano wakupendeza?
huku wakiamsemelea shetani akiwa na umbo au sura mabaya na kutisha?
.......malaika hawana muonekana na sura uliyo nayo kichwani mwako kwa sasa.......
 
Hii ndiyo shida ya malokoke, haioi shida kudanganya watu kwa maslahi yao…,,
 
Hayo ni yako na imani yako uliyolishwa, sisi tunauliza kwenye hicho kisa unachodai ni cha kweli na yaliyojiri maana umegusa imani za watu hivyo usilete janja janja ya kujificha kwenye mistari ya Bible kila unapoulizwa huo mkasa.
Mkasa ni wa kweli!! Sasa usipoamini ni wewe mkuu
1 Wakorintho 1:18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
 
Mkasa ni wa kweli!! Sasa usipoamini ni wewe mkuu
1 Wakorintho 1:18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
Mkasa haujataja Yesu wala Wakorintho lakini, na wala haujasema kwamba bila dini hiyo huingii mbinguni...haya nayo umeyapata wapi?
 
hivi kwanini tunaamini au tunaminishwa malaika ni viumbe wazuri na wana muonekano wakupendeza?
huku wakiamsemelea shetani akiwa na umbo au sura mabaya na kutisha?
.......malaika hawana muonekana na sura uliyo nayo kichwani mwako kwa sasa.......
Majini ni kibiblia ni mapepo ni malaika walioasi mbinguni wakatupwa chini pamoja na shetani, wanaitwa mawakala wa shetani, mapepo wachafu!! Hivyo hamna majini wazuri,ni upofu wa kiroho tu
Luka 11:24 Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, Luka 11:25 Nitairudia nyumba yangu niliyotoka. Luka 11:26 Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]

Umemjibu vizuri sana.Eti hawezi kwenda mbinguni bila ubatizo wa maji mengi! Waumini wa Ellen bhn
1 Wakorintho 1:18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
 
Mkasa haujataja Yesu wala Wakorintho lakini, na wala haujasema kwamba bila dini hiyo huingii mbinguni...haya nayo umeyapata wapi?
Mbinguni hamna dini!!!
Isaya 35:8 Na hapo patakuwa na njia kuu, na njia, nayo itaitwa, Njia ya utakatifu; wasio safi hawatapita juu yake; bali itakuwa kwa ajili ya watu hao; wasafirio, wajapokuwa wajinga, hawatapotea katika njia hiyo.
1 Petro 1:15 bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; 1 Petro 1:16 kwa maana imeandikwa, Mtakuwa watakatifu kwa kuwa mimi ni mtakatifu. 1 Petro 1:17 Na ikiwa mnamwita Baba, yeye ahukumuye kila mtu pasipo upendeleo, kwa kadiri ya kazi yake, enendeni kwa hofu katika wakati wenu wa kukaa hapa kama wageni. 1 Petro 1:18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; 1 Petro 1:19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.
 
Sasa umeanza kuelewa kidogo maandiko yalivyo. Nakushauri ongeza bidii kusoma maandiko na uzishike Amri za MUNGU naye atakupa "hekima, akili na ufahamu" wa NENO lake.
2 Yohana 1:9 Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho hayo, huyo ana Baba na Mwana pia.
 
Habari ya asubuhi wakuu!! Hiki ni kisa cha kweli kwa ambaye sio muumini wa Mbinguni na kuzimu hivyi vyitu ni halisi!!!
Miaka kadhaa iliyopita ndugu yangu, aliumwa sana wakati yupo hospitalini tunaamuuguza, alikuwa ameokoka (mlokole), hivyo kwenye ile wodi wachungaji mbalimbali walikuwa wanapishana kuja kumuombea maana aliumwa kipindi kirefu sana, Siku moja jioni alizidiwa na hatimae kufariki dunia( kwa mjibu wa dakitari ) baada ya taratibu za hapa na pale mwili kuandaliwa! Kupelekwa mchowari alipiga chafya na kurejea na kutoka pale akawa mzima mpaka leo, alichokisema ni hiki hapa baada ya kuzinduka
1: kuna maisha baada ya haya, anasema alitoka nje ya mwili wake na akaona jinsi dakitari alivyokuwa anampima pima na jinsi ndugu walivyoanza kulia, baada ya hapo alijikuta yupo dunia nyingine kabisa tofauti na hii!!
2: anaendelea kusema unakuwa na akili zako zote na kumbukumbu zako zote, maana yeye alipofika eneo hilo alikuwa anakumbuka kila kitu kilichopo duniani, na alijua amekufa!
3: matendo yako ndo yataamua uende njia ipi , ya mbinguni au kuzimu, anasema baada ya kufika eneo aliona kwa mbali majitu mawili ya kutisha yanakimbia kuja kumlaki!, lakini ghafula wakashuka watu wawili wamevaa nguo nyeupe wale majitu waliopoona wale watu wawili walirudi nyuma, wale malaika wakamwambia arudi abatizwe kwa maji mengi, maana hawezi kuingia mbinguni, na ndo maana wale majitu yalikuwa yanamfuata!! Baada ya kuambiwa rudi duniani ukabatizwe ndipo akarejea duniani!
Note:
1:Hamna mtu atakayeenda mbinguni bila kumwamini Yesu!!
2: ukitaka kwenda mbinguni fuata yote aliyoyafanya Yesu ikiwemo ubatizo aliobatizwa sio vinginevyo!!!
Huu ushuhuda ni kweli wakuu!! Sio wa kudharau!!!
Magu si ndio anaoomgoza malaika shida ipo wap
 
Hii ndiyo shida ya malokoke, haioi shida kudanganya watu kwa maslahi yao…,,
Marko 16:15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Marko 16:16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Marko 16:17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; Marko 16:18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya. Marko 16:19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. Marko 16:20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.]
 
Back
Top Bottom