Kisa cha kweli, mbingu ipo na moto wa jehanamu upo

Ili story yako ikamilike Kwanza ungetupa jina la. Huyo mtu. Hospital aliyofufukia. Daktari aliye confirm kuwa kafariki ili na sisi tukaverify hii taarifa. Mwisho kabisa muhusika inabidi aje na Yeye maana Ishuhuda huu ni mkubwa so haitakiwi aje ahadithie mtu mwingine.
Halafu hao malaika walitaka arudi tu abatizwe. Sasa mbona hajafa maana shida yao ilikuwa abatizwe tu.... Au bado hamjambatiza???.
Halafu unasema jamaa mlokole kaokoka then hajui msingi wa Ubatizo maisha yake yote?? Mpk akakumbushwa na malaika baada ya kufa[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849] sorry msabato hapo umetuacha.
 
Warumi 10:9 Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Warumi 10:10 Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
 
Mheshimiwa hapo unatangaza dini hunaa lolote! Ulivyoongea vyote hiyo ni filamu uliyoiangalia sasa unatuhadithia
 
Mkuu inabidi uamini tu hata nikikupa hizo document zote hutaamini (!! 2 Timotheo 4:3 Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti); Yesu wapo ambao hawamwamini lakini kazi zake zinaonekana mpaka leo, na swala la mbinguni huwezi kumlinganisha Mungu na wewe, mawazo ya Mungu sio mawazo yako
Isaya 48:6 Umesikia haya; tazama haya yote; nanyi, je! Hamtayahubiri? Nimekuonyesha mambo mapya tangu wakati huu, naam, mambo yaliyofichwa, usiyoyajua.
 
Mheshimiwa hapo unatangaza dini hunaa lolote! Ulivyoongea vyote hiyo ni filamu uliyoiangalia sasa unatuhadithia
1 Wakorintho 2:14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
 
Naona umeukazia ule uongo wa kwenye picha mliokaririshwa wa malaika kuvaa mavazi meupe.Halafu huyo jamaa na ulokole wake wote aliambiwa hawezi kuongia mbinguni mpaka akabatizwe je kubatizwa kunahusiana nini na kuingia mbinguni.Tumedanganywa sana au nasema uongo ndugi zangu
 
Naona umeukazia ule uongo wa kwenye picha mliokaririshwa wa malaika kuvaa mavazi meupe.
1 Wakorintho 1:18 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.
 
Mkuu hii ni fursa kwa washonaji na wauzaji wa nguo nyeupe. Malaika wananunua sana tena kwa bei nzuri. Tuchangamkie fursa wakuu
 
Unapata kiu ya haki ukiwa wapi hapa duniani ?
Yohana 4:13 Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; Yohana 4:14 walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. Yohana 4:15 Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka.
 
Hayo mavazi meupe ya malaika huwa anayashona nani?
Isaya 55:8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Isaya 55:9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
 
Tufungue kanisa tupige pesa kupitia huu mkasa
 
Mkuu hii ni fursa kwa washonaji na wauzaji wa nguo nyeupe. Malaika wananunua sana tena kwa bei nzuri. Tuchangamkie fursa wakuu
Isaya 55:8 Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema BWANA. Isaya 55:9 Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
 
Anaefikiria kuna maisha baada ya kifo, ni kupoteza mda, tumia huo mda kufikiria kuwa maisha ni haya tu yakiondoka yameondoka.
 
Tufungue kanisa tupige pesa kupitia huu mkasa
Yohana 10:12 Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yohana 10:13 Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Yohana 10:14 Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…