Kisa cha Kweli: Mungu alikataa kifo changu mwaka 2018

Kisa cha Kweli: Mungu alikataa kifo changu mwaka 2018

Kelly Allen

Member
Joined
May 7, 2023
Posts
12
Reaction score
20
Hello habari, Mimi ni kijana niliezaliwa mnamo mwaka 1995 katika kanda ya kaskazini hapa nchini.Nimesoma shule mbalimbali hadi kufanikiwa kupata digrii ya kwanza katika chuo cha Taifa cha usafirishaji (NIT).

Leo nimeona kushare na nyie story yangu hii ya kweli ambayo nahisi itakusaidia kupata majibu ya maswali mengi sana. Sitotumia majina yote halisi ili kuficha identity yangu.

Story yangu ipo katika mtiririko ufuatao
1. Mungu alivyokataa kifo changu 2018
2. Nilivyoona kitu cha ajabu juu mawinguni
3. Na mengneyo ya ajabu ajabu mengi
Sitoandika vyote nitafupisha tu lengo ni message basi. Kisa cha kwanza kilinitokea mwaka huo wa 2018 mwezi march. Nakumbuka nilikuwa mwaka wa pili semista ya pili na tulikuwa kwenye mitihani ya kumaliza semista ili tuingie mwaka wa tatu.

Nikiwa nimefanya mtihani mmoja tu na mwngne wa pili nilishindwa kumaliza kwasababu nilipata homa kali na dam kuanza kutoka puani nilimwita msimamizi wa mtihan na kuona hali yangu akaniambia kwa muda uliofanya mtihani sis tunachukulia umeshamaliza so tunakuruhusu utoke. Basi nilitoka nikiwa naumwa sana nilielekea geto langu maeneo ya mabibo.

Geto nilikuwa naishi na mpenz wangu ambae alikuwa mwaka wa kwanza. Baada ya kufika nilala na kuzidiwa hivyo mpenz wangu akafanya juhudi akanipeleka hospitali. Nikafanyiwa vipimo ila ni malaria na typhoid ndo vilionekana nikapewa dawa nikaruhusiwa kuondoka. Kufika geto usiku wake nilizidiwa sana nikarudishwa tena hospital na kulazwa mpaka asubh. Nikaruhusiwa tena kuondoka, mchana wake hali ikawa mbaya nikarudishwa tena hospitali sasa nikafanyiwa uchunguzi vzur ila majib ni yale yale.

Nilikaa pale hospital kama siku mbili nikaruhusiwa kuondoka ile nimefika tu sijakaa sawa hali ikawa tete tena nikabadilishiwa hospital nikapelekwa ya private ni kubwa kdg nikapimwa nikaambiwa habari ile ile. Basi ikabd nirudishwe kwenye ile hospital ya mwanzo ili waendelee kuimonitor hali yangu.

Nakumbuka ilikuwa usiku wa saa nne yan sitokaa nisahau hii siku, wakati nikiwa nimelala na nimezidiwa sana naita hamn anaeniskia ghafla nikajikuta kwenye mazingira ambayo ni strange sanaa, nikaona kitu kama kivuli kimekuja upande wangu wa kushoto ila sikuona sura kikawa kinanishawishi sana kwamba nisiogope kufa mbona wengi wamekufa, nikaanza kuona watu waliokufa muda mrefu yan ananiambia usiogope mbona flan alikufa mbona na flan na huyu na yule yan alinishawishi hadi nikakubali kufa nikaridhika kabisa acha nife sasa basipo kinyongo au kuona nadhulumiwa.

Baada ya kukubali tu kufa nikaanza kuhisi ganzi na baridi kali sana kuanzia kwenye vidole vya miguu ile hali ikaanza kupanda sasa ikafika hadi miguuni naiskia tu inapanda na ikipita nakuwa siskii tena kitu katika sehemu hyo. Ilipokaribia kupita tumboni ile ije kifuani, mm naiskia tu na nilikuwa na huzuni sana kwan nilikuwa namwona mama yangu namwita ata haniskii nikasema atalia sana akiskia nimekufa yan nikawa namuwaza mama yangu tu na kumwonea huruma sana atakapopata taarifa kwamba nimefariki. (Mawazo yote haya yalikuwa within seconds sio ata dakika) basi ile hali ilipokaribia nahis sehem ya moyo kikaja kivuli upande wangu wa kuume kwa haraka sana kikaniambia sema ivi "SITAKUFA NITAISHI MUNGU ALIUMBA MUNGU MTU KUPITIA YEYE SITAKUFA. nikaanza kuwaza before sijasema, kwanza kabsa mm habari ya kanisa au biblia sijui ata ukiniambia nitaje ata verse moja kwa usahihi in the bible siwezi ata quran sijui imendikwa nin uko ndani japo naionaga tu.

Nikasema huyu Mungu mtu atakuwa ni nani? Nikasema hyu huenda akawa ni Yesu maana ndo naskiaga ana contradiction sana mara mungu mara mwana wa Mungu ata sielewi . (kumbuka haya pia yanafanyika within seconds) basi nikawa narudia kwa bidii yote nikiwa namrefer Yesu sasa ila sikuwa na uhakika nikawa nasema sitokufa nitaishi, Mungu aliumba Mungu mtu kupitia yeye nitaishi baada ya kuanza kurudia hayo maneno kweli ile hali ikastop ghafla ikaanza kurudi chini Oh nikawa nasema sasa kwa bidii mpaka ile barid na ganz kali ikaishilia vidoleni ilipoanzia, ghafla nikaanza kusikia sauti za watu, nikaona mwanga, nikamwona daktari anaongea na marafik zangu pale ndan kumbe ningekufa ata wao hawajui.

Nikawa nimerudi kuwa hai tena maana nilikuwa sehem nyingine kabsa nashindwa ata kuielezea. Kuna vitu viwili nilijifunza kupitia hili tukio moja: kabla mtu hajafa lazma makubaliano yafanyike (na malaika mtoa roho) hii nimeconfirm kabsa(Thanks God) Pili kuna uwezekano mkubwa kipindi mtu anakufa ubongo kikawa kiungo cha mwisho kufa na ndio maana ata mm nimeweza kukumbuka kila kitu japo sio vyote.

Baada ya kupata nafuu pale hospital niliamua kwenda home kabsa hvyo nikaenda chuo kuandika barua ya kuomba kufanya special mitihan mitatu ambayo nilikuwa sijafanya kabsa. Nikiwa nyumbani sikumwambia mtu yeyote what happened nikawa nawaza huyu Mungu mtu ni yesu kweli?? Au nikasema potelea mbali mm mambo ya din za wazungu sitaki.

Siku moja ilikuwa jumamosi nikasema kwann leo nisiende ukumbi x kuskiliza habari za Mungu mtu? Nilikuwa na nauli tu ila sadaka sikuwa nayo nikasema acha niende ila nikiwa kwenye gari nikaanza kujilaum uku sasa naenda wapii? Kwanza sina ata sadaka na hawa ni sadaka tu wanatakaga na mm ni mwanaume apa naenda kuaibika watu adi watoto wanatoa alaf mm naonekana kama sijielewi.

Nikawa na hasira sana nikamwambia wew Kama kweli ni Mungu mtu mfanye huyu konda asahau kuchukua hii nauli ili nikaitoe kama sadaka, nilikuwa nimekaa siti ya mbele natazamana na konda yeye amekaa kile kiti cha wanafunzi basi kwel jamaa akaamka akaaza kuchukua nauli cha ajabu akaniruka akachukua kwa niliekuwa nimekaa nae adi akamaliza gari zima akarud kukaa hakuniuliza nauli basi nikashuka na kweli nikaenda kuitoa sadaka.

Nilivyoshuka nikawa bado siamin nikasema ah huenda amejisahau tu. Basi kufika kwenye ule ukumb wa maombi pale getin nikaona wale wapokeaji wagen wameshika mapembe ya Ngombe alafu umo ndan kuna mafuta wanawapaka watu kweny paji la uso then unaingia, kiukwel mm sikupenda ile hali but nilikubali nikazama ndan mle ndani kama kawaida watu walikuwa wanaimba tu mara vitoto vinalialia tu mchungaji alianza mahubir yake kweli yalinilenga mim kabsa ila nikapotezea nikaanza kuwaza nitachomoaje ile sup (matokeo yalitoka na mm lile somo ambalo nilifanya nusu mtihani nilipata sup) sasa mweny hilo somo la sup tunamjua vzur kabsa na alisema ukipata sup somo langu umekwenda na maji mwaka wa tatu utauskia tu.

Nikiwa pale ukumbini nikamwambia kama kweli kweli ni wew naomba ile sup ya yule mwamba nikaifute na masomo mengne pia nifaulu niweze kwenda mwaka wa mwisho. Baada ya maombi nilirud home ile nafika tu nilichukua kidaftari kdg nikaanza kuandika vitu nilivyokuwa navigugo kwenye simu yangu ila vilihusiana na ule mtihan.

Muda wa kwenda kufanya special na sup ulifika nikarud dar ilikuwa mwez wa Tisa mwaka 2018 . But nilivyofika tu nikaanza kuumwa sana sikuweza kabsa kujisomea kwaajili ya sup na zile special, rafika yangu mmoja akaniambia Kelly rudi tu nyumbani hii ngoma hutoboi nenda tena chuo kaandike barua ya kuomba kupostipone mwaka maana unaweza ukashindwa kuchomoa hizo special na sup ya mwamba ukadisko.

Nilikuwa nalala tu kitandani nakula nimelala basi akaniambia kuwa wameweka kambi chuo na wanalala huko hadi na mashuka wanayo nikasema doh!

Siku ya ile sup ikafika nakumbuka ilikuwa ni saa kumi na moja ilipofika saa saba nilibaki peke yangu wengne wakawa wameenda chuo kwaajili ya pepa wakanisih nisiende kufanya huo mtihan, ilipofika saa tisa nikasema hapana! Naenda na mm kufanya pepa, nilipofika chuo kweli niliwaona marafik zangu akiwemo Jamaa yangu nilikuwa namwita Magufuli akaniambia ah Kelly ulikuwa wap muda wote tunalala uku chuo wew huonekan nikamwambia nilikuwa naumwa basi na yy akanisihi nisifanye lile pepa nifanye mpango nipate postpmnt. Nikasema No!

Punde si punde muda wa pepa ulifika tukapangwa kiroho mbaya sana ni ngum kuona ata kama mwenzako ana calculator. Inshort walisup robo tatu ya darasa. Baada ya kusambaziwa mitihan kufungua maswali ivi lah haula! Yale maswali niliyoandika siku nilitoka maombi yale kule kwa ule ukumbi yapo kama yalivyo yan nakumbuka nilindika maswali maane na yote niliyakuta kama yalivyo na yalikuwa na marks 20 kila moja asee nilifurahi sana.

Niliandika kama nilivyoonyeshwa na baada ya kutoka kwa pepa kila mtu alishika njia yake hakuna aliesemeshana na mwenzake.

Baada ya kutoka kweny pepa nilimshukuru sana Mungu Mtu na nikawa siamini kabsa kama ni mimi natokewa na hivi vitu. Basi nikamwambia tena still i don't believe kama kwel ni ww nikamwambia kama kwel ni wew basi hii special moja ni hesabu na hesabu sio mzima sana nikamwambia wew fanya vyovyote huu mtihan niufalu ndo ntaamin kwel ni wew. basi nilivyofika geto nikaskia vijana wanalalama sana na kumtukana yule lecturer matusi mazito mno mm kimyaa! day iliyokuwa inafuata ni hyo ya pepa la hesabu sasa usiku wake nikasikia kitu tu kimeniambia "go through all examples only" sikufanya ajizi nikaendana na maelekezo, kesho naenda kwa pepa lah haula!

Pepa yotee ni examples kuanzia alipoanza mpaka alipoishia na hakubadili ata namba doh nikatusua sana asee. Basi nikamshukuru sana sana Mungu Mtu basi nikasepa. Baada ya kumaliza sup na special nilirudi home kusubiri matokeo na nilifaulu kweli kweli.

Please usikose next part! See you soon
 
kabla mtu hajafa lazma makubaliano yafanyike (na malaika mtoa roho) hii nimeconfirm kabsa
Kabla hujafa Moyo wako unaangalia ulipo na Deni ni wapi ? Kisha huomba ukalipe Deni kwanza baada ya hapo unaachiwa unakua hai Yes kweli kuna makubariano, kumbuka utaelezwa sababu za kuchukuliwa kabla kisha unapewa nafasi ya kujitetea, ukishajitetea km sababu zako ni za moyoni haswa unaachiwa uishi
 
Second year unaishi na binti wa MTU eti mpnz wako?????
Chuo hilo Jambo la kawaida wanatiana hadi mimba Chuo kinajua wanapewa maternity leave eeh na Chuo sio suala la kificho Chuo sio shule ya msingi, wafanye wapi sasa km sio Chuo?
 
unaelewa nini kuhusu Mungu mtu...labda me ndo sielew
Mtu kweli kwa Mtu kweli, Mungu kweli kwa Mungu kweli, aliezaliwa bila kuumbwa mwenye uMungu mmoja na Baba, akazaliwa kwa uwezo Roho Mtakatifu, kwake yeye Bikra Maria, akasuribiwa pia kwa Mamlaka Pioisioi Pilato, akateswa, akafa, akazwa, siku ya tatu akafufuka kutoka katika Wafu, akapaa mbinguni, amekaa kiume kwa Baba, atarudi Tena kuwahukumu wazima na Wafu, nao ufalme wake hautokua na Mwisho

Nasadiki kwa Kanisa moja, Takatifu Katoriki la Mitume, Naungama ubatizo mmoja, kwa maondoleo ya dhambi

Km hapa pia haujaelewa wewe una kichwa kimoja kizito nenda kwa Mwamposa akuwekee mikono kichwani,
 
Hongera sana mtoa mada. Wewe ni kati ya watu wachache wanaopata bahati ya kuona mambo kama haya.

Endelea kuyatafakari yale maneno aliyokuambia uyatamke yule mtu pale hospitali. Endelea kuyatamka kila siku.

Achana na mambo sijui ya kanisa, huko watakupoteza na kukuondolea nguvu zako. Baki jinsi ulivyo huku ukijitafakari.

Na pia achana na hawa MAUCHWARA ya humu yanayotoa kejeli. Hayajui lolote wala hayafahamu ulichokiona. Ni MAZWAZWA yenye SMARTPHONES. Kwanza wengi wao ni WACHAWI na WAGANGA WA KIENYEJI, hawana uwezo wa kukushauri kitu zaidi ya UPUMBAFU.

Hongera sana, umeoneshwa mambo ya ajabu ili uwe jasiri na uzidi kujiamini. Asitokee mtu akakwambia sijui njoo kanisani mara sijui okokaa. KATAAA, mwambie kabla ya dini MUNGU ALIKUWEPO.
 
Mungu yupo na anatenda maajabu kila iitwapo leo, sisi binadamu tukibadili matendo yetu na kumgeukia yeye atakuwa karibu na sisi siku zote, tusiache kumwamini.
 
Anachosema mtoa mada ni kweli kabisa
Mimi Haikua kifo ila Mbingu zilinisaidia sana kipindi niko chuoni.
 
Back
Top Bottom