plumber hydrogen
JF-Expert Member
- Feb 17, 2022
- 881
- 1,537
Noma
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamna mchango hapa, sometimes majukumu yanatubana ila hapa ni mwanzo mwisho.Mchango buku 3
Tunasubiri mkuuHamna mchango hapa, sometimes majukumu yanatubana ila hapa ni mwanzo mwisho.
Naachia kitu sio muda.
Mkuu kuna ile story ya dada aliyekua anafanya kazi za ndani akaopoa mfanya biashara masaki akazaa ane twins, nikumbushe ule uzi please. Yeyote anaekumbuka naomba anipe details.
MnoooDah
Kwenye upande wa ulimwengu huo hakuna kuoneana huruma
Hilo neno zito sana
Leo endelea murisya.Tunaendelea sehemu ya nane.
Tulianza kumfuata yule ndege tukiwa tunatembea kwa miguu. Hii dunia ina maajabu sana! Kwa kasi aliyokuwa anatembea yule ndege mdogo ili tufanya tutembee kwa kasi sana ili kwenda nae sawa au niseme alikuwa kama anakimbia.
Tulitembea kwa muda sasa tukawa tunaelekea usawa wa mti mmoja aina ya mkuyu mkubwa sana. Mti huu ulikuwa unapatikana mpakani mwa kijiji chetu na kijiji jirani upande wa magharibi. Ni mti ambao ulikuwa upo katikati ya uwanda ambapo ulikuwa peke yake hakukuwa na mti mwingine mdogo wala mkubwa. Yule ndege alivyoanza kwenda usawa ule nilianza kuhisi ataenda sehemu ile.
Licha ya kwamba matukio mengi niliyokuwa nimeyashuhudia yalikuwa ya kuogofya, lakini kwenda kwenye huu mti naweza sema kile kiwango cha uoga kilikuwa kimepanda hadi kikafika mwisho. Hii ilitokana na simulizi za kutisha ambazo tumekuwa tukisimuliwa kuhusu eneo hilo miaka na miaka. Ni eneo lenye maajabu ni kawaida kusikia watu hapo wamepotezwa kwa muda wa siku kadhaa, au kupotea njia na kujikuta wametokea mbali sana, kusikia kelele za watu na vigoma bila kuwaona hasa nyakati za usiku, au watu kukutana na watu waliokufa. Nilisikia kuna pia kuna mtu mgeni akiwa anachunga ng'ombe aliwahi kwenda kukaa pale akiwa hana habari akashangaa anapewa sahani ya wali na nyama, usiniulize kama alikula au la! Ukitaka kujua niambie nikupeleke ukatembelee siku moja!
Mojawapo ya simulizi ambayo nadhani kila mtu wa eneo lile aliijua, ilisemekana kwenye mti ule kulikuwa na nyumba nzuri sana, ambapo wafu walikuwa wanaishi. Ilikuwa ni kawaida pale kijijini mtu akifa kifo ambacho walimwengu wanaona si cha kawaida basi baada ya siku chache utasikia kaonekana anatembea kwenye mti ule au karibu na mti ule.
Ndio sehemu ambayo nilihisi tulikuwa tunaenda Sasa, japo akilini mwangu nilitamani ndege yule aende sehemu nyingine.
Mawazo yangu hayakuwa nje ya ukweli, ndege yule alikata kona kuelekea kwenye ule mti. Tulipokata kona tukapiga kama hatua mbili, huwezi kuamini tulichokiona!
it was a house!!!
Yes pembeni ya ule mti mkubwa tuliona nyumba kubwa sana na ya kupendeza. Tulitembea hadi sehemu kuliyokuwa na mlango wa ile nyumba. Ndege yule kufika kwenye ile nyumba alisimama kidogo ghafla ule mlango ulifunguka!
Mzee Masele alininong'oneza nitangulie mimi kwanza mlangoni, halafu nikifika ninyanyue fimbo juu. Hakukuwa na nafasi ya kuuliza maswali zaidi ya kutekeleza nilichoamriwa. Mzee Masele nilimuona akitokomea nyuma ya ule mti mkubwa, sikujua alikuwa anafanya nini.
Nilienda moja kwa moja hadi kwenye mlango wa ile nyumba, niliona ile nyumba haikuwa na chumba ilikuwa ni kama ukumbi wa moja kwa moja. Katikati ya chumba kulikuwa na wanaume na wanawake wapatao ishirini walikuwa wamekaa kama kundi likiwa kwenye kikao niliwasikia walichokuwa wanakizungumza lakini sioni sababu ya kusimulia. Wachache kati yao niliwatambua. Nilivyotazama mwisho kabisa wa ile nyumba au tuseme ukumbi nilimuona yule ndege amesimama kwenye kama ka meza kalikozibwa Pande zote na kutengenezewa ka mlango kadogo. Au niseme kalikuwa kametengenezwa kama ka chumba kadogo na kafupi kenye mlango mdogo na kalitengezwa kwa matope kabisa. Juu ya ile meza kulikwa na makorokoro ya ajabu ajabu vichwa vya wanyama, mifupa, mizizi vingine sikuweza kuvijua.
Pamoja na kwamba nilikuwa nimesimama mlangoni na ndani ya ile nyumba kulikuwa na mwanga uliotoakana na myoto iliyokuwa imewashwa mle kwa kuni na nyasi lakini ni kama walikuwa hawaoni chochote. Wengine walikuwa wanatazama kabisa mlangoni lakini hawakuona chochote. Niliendelea kusimama hadi mzee Masele alivyokuja na kunipita kwa nyuma bila kuiniongelesha. Alikuwa anahema sana alionekana kama ametoka kupigana au kufanya kazi ya kutumia nguvu nyingi sana. Alitembea moja kwa moja hadi alipokuwa yule ndege na kuchukua ka kopo fulani, alipokachukua tu yule ndege akaanza kupiga hatua kutoka nje. Wakati Mzee Masele anaingia na kutoka bila woga alipita karibu sana na lile kundi la waliokaa, lakini hawakuhisi chochote. Wakati mwingine nilihisi kama ananichora ili nimuone alivyo mtaalamu wa hayo mambo, ndiyo nilikuwa sahihi kwa nini apite karibu vile wakati nafasi ya kupita ni kubwa tu angewadondokea je? Mzee Masele alikuwa anapiga hatua akifata Kwa nyuma ya ndege huku mimi nikiendelea kusimamisha fimbo juu. Walivyotoka na mimi nikatoka tukaanza kuondoka eneo lile kwa kasi. Cha ajabu tulivyofika mbali kidogo mzee Nkelebe aliniomba ile fimbo akampiga Yule ndege akafa palepale.
Sikuuliza chochote! Mambo ya ngoswe muachie ngoswe mwenyewe.
Sisi tulitembea hadi nyumbani kwa mzee masele, tulivyofika tu aliniingiza kwenye kijumba chake. Alifungua kile kikopo akaniambia hii ndiyo damu yako, alimwagia dawa fulani ya unga ndani ya kopo. Kisha akanitengenezea dawa nikaenda kuoga, halafu akaniambia niende nikaichimbie ile damu.
Baada ya kumaliza akaniambia
"Una bahati sana! Sasa hawana nguvu tena kwako! sasa kesho tutawatengeneza waliokufanyia ubaya. Kwenye huu upande wa ulimwengu huwa hakuna kuoneana huruma maana hakuna kinachotokea kwa bahati mbaya. Mtu akikuumiza ujue kadhamiria usipommaliza ataendelea kukutafuta mpaka pale atakaponyoosha mikono"
Tulipata chakula, akamaliza akaniamuru niende kulala.
Itaendelea, ndio ndio