Sehemu ya 15.
Nilifika nyumbani lakini nikiwa na mawazo mengi sana, sikuwa sawa. Baadaye niliingia geto la pale home kulala, geto tulikuwa tunalala wawili mimi na kaka yangu. Wakati huo kimawazo nilikuwa mbali sana. Niliifikiria kauli ya Vumilia ambayo alitoka kuniambia siku hiyo kwamba, kuna kitu hakufikiria kunifanyia lakini kwa sababu nilionyesha nampenda Sara na sio yeye basi hakuwa na jinsi zaidi ya kunifanyia hicho kitu. Niliwaza ni kitu gani hicho sasa?
Niliamini hiyo kauli aliyoniambia ilikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mimi kukabwa ili nile nyama kwa lazima. Licha ya kuamini hivyo swali lilibaki palepale
"Je kitendo nilichofanyiwa lengo lake ni nini?"
Wakati nikiwaza hivyo nikapata wazo fulani akilini, naweza sema lilikuwa la kipuuzi lakini kwa wakati huo lili-make sense sana. Sio wazo niseme ni tukio ambalo liliaminika kutokea.
Kuna jamaa mmoja pale kijijini alinunua mti ambao ulikuwa umepakana na nyumba ya bibi mmoja aliyeaminika ni mwanga au mchawi sana. Aliununua ule mti kwa lengo la kuukata ili achome mkaa, akaukata. Siku hiyo alipoukata usiku alivamiwa na watu wenye nywele ndefu usiku wakamkaba sana (usiniulize hizo nywele walizionaje hata mimi sijui). Kesho yake aliamka anaumwa yuko mahututi kufikia jioni, alikuwa ameaga dunia. Ilisemekana alikata mti wa mmliki feki wa huo mti lakini mbabe. Na huyo mmiliki feki alikuwa ameshaweka vitu vyake kwenye huo mti, hivyo alipoukata aliharibu vitu vya mbabe huyo. Na malipo yake yakawa kuondolewa kwenye uso wa dunia.
Ilisemekana lakini!
Nilipokumbuka hiyo scandal niliogopa sana. Nikasema inawezekana na mimi nilivyokabwa hivi kesho inaweza kuwa kwa heri, nitaumwa ghafla na kuondoka ndani ya muda mfupi. Nilizidi kuogopa sana nilipofikiria hilo.Nikaanza kuwaza nifanye nini, nilikosa jibu hasa nikikumbuka aliyeniokoa kwenye msala wa kwanza ndiye huyu anayenitafuta kuninasa kwenye mtego wake kwa sasa. Nilichanganyikiwa!
Baada ya kutafakari sana,niliona njia salama pekee ilyokuwa imebaki ni kutafuta suluhu na Vumilia haraka iwezekanavyo. La sivyo lolote linaweza kutokea. Haraka niliamka nikamuambia bro wangu, natoka naenda kwa John kuna t-shirt yangu ya shule nilimpa nataka nikaichukue kesho nataka kufua asubuhi sana (john alikuwa anakaa maeneo ya karibu na kwetu). Bro wangu alikuwa sio mtu wa kujali sana, hivyo nikatoka. Nilivyotoka nilianza mbio kuelekea kwao Vumilia nikiwa na Lengo la kutafuta suluhu. Kulikuwa kuna umbali fulani, lakini muda si kitambo nikawa nimeshafika. Nilikifahamu chumba alichokuwa analala, na uzuri nilifahamu huwa analala peke yake. Nilianza kugonga dirishani huku nikimuita kwa sauti ya chini lakini sikusikia mtu akinijibu. Niligonga dirisha hadi nikachoka!
Nikaamua sasa bora nirudi nyumbani, nilianza kurudi nyumbani. Lakini ghafla kwa mbele nikamuona mtu amesimama katikati ya barabara. Mawazo ya wachawi yakiwa tayari yameshaitawala akili yangu. Niliogopa nikataka kutokomea vichakani, lakini akawa ananifuata kwa nyuma!
Aisee! Nilitimua mbio kama Hussein "Bolt". Lakini cha ajabu nikigeuka nyuma namuona yupo anakuja tena yeye hakimbii anatembea tu. Wakati nikiendelea kukimbia nilisikia sauti!
"Mr the dragon kwa nini unamkimbia unayemtafuta! "
Ilikuwa ni sauti ya Vumilia!
Nilishangaa sana lakini nikaamua kusimama, mahali pale kwenye pori pori sio barabarani. Nikamsubiri ninayemtafuta aje!
Alipofika swali la kwanza kuniuliza lilikuwa
"Yaani wewe pamoja na yote uliyoyaona bado unaogopa hivyo"
Sikupendezwa na hilo swali maana nililiona , halikuhusu jambo lililonileta nikapuuzia kujibu ili kuokoa muda. Alivyoniona sijajibu akaongea tena!
"nimekufatilia toka tulipokwambia uende kwenu hadi ulipomuaga kaka yako, unaenda kwa John. Lakini pia ulivyoenda kwetu badala ya kwao John, vilevile nimekuona ulivyokuwa unagonga kwenye chumba changu. Haya nambie kwa una shida gani na mimi kikaragosi, wewe si unampenda Sara!"
Nilimuangalia kwa macho ya huruma halafu nikamuambia.
"Naomba tusameheane kwa yote yaliyotokea, nilikuwa mjinga kusahau wema wako kwangu. Naomba kama kuna kitu kibaya unataka kunifanyia basi nisamehe, sitarudia tena" niliamua kuomba msamaha!
"Hakuna chochote kibaya tulichokufanyia" alijibu kwa dharau za mbali
"Unajua Vumilia tokea mlivyonilazimisha kula manyama yale, najihisi niko hatarini sana yaani nimechanganyikiwa"
"Hatari ipi"
"Sasa yale manyama mmenilisha ya kazi gani"
"Ili uwe wa kwangu peke yangu"
"Kivipi"
"Utaona mwenyewe! Wewe nenda kalale kwa amani! Sitakufanyia kibaya kabisa, lakini angalau kwa sasa naamini nitakuwa chaguo lako la mwisho. Kwa heri"
Baada ya kusema hivyo alipiga hatua na kuondoka maeneo yale, nikamuona anatokomea gizani.
Niliondoka na kurudi nyumbani kidogo nilikuwa na amani. Sijui ni kwa nini nilipata amani moyoni, lakini kuna muda nilikuwa namuamini sana Vumilia vitu alivyokuwa ananiambia. Hivyo alivyoniambia hakuna jambo baya litakalotokea, nilimuamini!
Ingawa kuna swali jipya ambalo lilihitaji majibu lilitokea. Swali lenyewe ni hili, Vumilia anaposema nitakuwa wa kwake peke yake, ama yeye ndio atakuwa chaguo langu la mwisho anamaanisha nini?
Ni jibu ambalo mpaka leo sijawahi kujua jibu lake haswa. Maana mhusika hakuwahi kunipa majibu kamili. Lakini kuna mambo yalianza kutokea kwenye maisha yangu ambayo nilihisi ndio yalikuwa majibu ya swali hilo.
Kwanza Sara alinikataa siku chache baada ya tukio hilo, akawa hataki hata kuiona sura yangu. Yaani msichana niliyefahamu kwamba ananipenda tokea akiwa bado binti mdogo, alinikataa pasipo sababu ya kueleweka. Msichana ambaye siku chache zilizopita tuliwekeana ahadi za kupendana mpaka mwisho wa uhai wetu. Kingine ikawa kila msichana niliyekuwa nikirusha ndoano angalau nimvue chupi ili nipunguze ashki aliruka mita mia nane. Namaanisha kila msichana niliyekuwa nikimtongoza alinikataa. Hali hii ilinishangaza kidogo inakuwaje kijana barobaro wa kijiji, ninakataliwa halafu wanakubaliwa washamba wengine ambao ninawazidi vigezo na sifa, wanakubaliwa na wasichana walewale ambao mimi wamenikataa!
Nilikataliwa hadi na wasichana wengine ambao, ungeonekana unawatongoza ungechekwa na washikaji. Ama ungeonekana umewaonea huruma! Lakini walinikataa!
Nilikuwa nimepewa mkosi au"kimavi" kama wasemavyo vijana wa mjini. Hakukuwa na njia kuelezea hilo tofauti na kuamini nimepewa mkosi.
Na kweli Vumilia aliposema yeye ndio atakuwa chaguo la mwisho hakukosea. Maana kila hamu ya kuvunja amri ya sita au ya saba iliponishika ikawa ni lazima nirudi kwa Vumilia. Vumilia akawa ni kama mke wangu sasa, na mimi nikawa mme bora nisiyeweza kuchepuka au labda mme bwege! Sijui!
Kwa hiyo kila nilipopata ashki ilibidi nikatulize kwa Vumilia. Na kila akizingua kunipa tunda ilibidi nimbebeleze hadi atakpokubali. Sikuwa na option nyingine!
Mpaka wakati huo mimi nilidhani nimepewa mkosi pekee wa kukataliwa na wanawake! Kumbe nilijidanganya! Ndio nilijidanganya kabisa! Kuna kitu kibaya zaidi nilikuwa nimefanyiwa pasipo kujua.
Nakumbuka mwaka huo ulikuwa unaelekea mwishoni. Ilikuwa mwezi wa 12 mwaka 2012 tukiusubiri 2013 mwaka ambao ningeingia kidato cha nne sasa!
Mzee wangu akanipeleka mjini Mwanza kusoma Tution shule moja ya serikali iko maeneo ya Nyegezi. Sasa nilipokuwa nakaa ni kwa ndugu yangu, binamu yangu wa kiume mtoto wa shangazi yangu. Jirani na pale kulikuwa na demu mmoja mzuri sana, anavaa miwani alikuwa anasoma shule moja ya private huko pasiansi. Yule demu alikuwa mzuri sana,tena mjanja mjanja wa mjini achana na waporipori wa kule kwetu. Alikuwa na ngozi laini, msuko mzuri na wowowo si haba. Sasa tukawa tunasoma wote Tution! Asubuhi tunaenda pamoja, tunarudi pamoja.
There is time for everyone, no matter what!
Ndio naweza kusema hivyo, nikawa nimeshazoeana na huyo demu. Sasa kuna siku nikasema ngoja nijaribu bahati yangu. Au ngoja nipime kina cha maji! Nikarusha mistari kwa yule demu, akanikubalia!
Siku hiyo nilifurahi sana, pamoja na kwamba nilijawa na mshangao sana. Maana niliamini Vumilia alishafanya yake, lakini cha kushangaza zilidunda kwa yule mtoto wa kihaya!
Niliona kabisa yaani nimekataliwa na mademu wabovu (sorry if it is offensive) . Lakini nakuja kukubaliwa na demu ambae kiuhalisia kwa wakati ule mimi sikuwa type au class yake.
Sasa bwana tukawa tumeelewana siku ya Christmass tukachakatane. Siku hiyo alidai ndio siku ambayo angepata uhuru wa kutoka. Kulikuwa na dogo tunakaa nae pale kwa binamu yangu alikuwa mwenyeji wa yale maeneo akawa amenifanyia mpango wa geto la kwenda kumchakata yule mtoto. Siku ya siku ikafika nikiwa na hamu ya kuibabua papuchi ya kimjinimjini
Tukutane kesho.