Kisa cha ''magaidi'' wawili: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege

Kisa cha ''magaidi'' wawili: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege

Hatukatai😂😂huenda uko sahihi kwenye hayo ya TANU maana hakukuwa na CCTV. Ila tunaoneshwa footage za magaidi siku hizi. Na zingine wanajirekodi wenyewe kabla ya kwenda kuua watu wasiohusika kwa kisingizio kuwa wanafanya kazi ya allah.

Alafu wewe unakuja kuwatetea hapa. Maswali magumu yakianza unakimbilia kumsingizia Nyerere.

Kubali kuwa magaidi wanatengenezwa na masheikh na viongozi wa dini wenye misimamo mikali.

Usituambie hao wamesingiziwa eti kisa ulikuwa unafahamiana nao. Kuna watu mchana ni wastaarabu na heshima zao lakini usiku ni majambazi wenye roho za kinyama.

Unakamatwa kama unaviashiria vya ugaidi sio kwa vile wewe ni muislamu

sheria yenyewe ya ugaidi imewekwa na wakristo
 
Miaka ya utotoni shuleni , alikuwa akituhubiria dini mwanafunzi mwenzetu aliyetutangulia darasa. Ye form six si form three enzi hizo. Nilikua nikienda humo kusali na baada ya Sala akitoa nasaha Hapa na pale basi mwenzetu Yule alikua charismatic Sana. Akiongea Yale ayaongeayo watamani kuyatekeleza kwa uharaka.
Katika siku flani akaanza katika hotba zake kuchomekea chuki dhidi ya wengine. Na Kwamba sisi tunaonewa Sana. Ohh huko niliendaga kusoma maza alinikataza kujihusisha na makundi yoyote hasa hata Yale ya kutetea maslahi yetu kibabe.
Basi sikukuu flani ya idi Yule bwana akatuwekea katika screen ( sikumbuki Ni ya tv au PC) video moja ya shekh kavaa kibarghashia, half combat ya kitopu Cha bakabaka flani hivi Cha mtumba, kanzu, pamoja na Smg pembeni yake.
Yule shekhe kideoni alikua akiongea kiswahili Cha Kikenya flani hivi akihamasisha hiki na kile juu ya uonevu dhidi ya dini na hasa akituomba kiushawishi tuchukue hatua dhidi ya Mambo kadha wa kadha aliyosema.
Ah Mimi isitoshe kwetu Ni mbali Sana na niliposomea ikawa mi nasali na kusikiliza kama redio na kutembea. Nikasoma nikafanya mtihani nikatembea.
Baada ya kuona Hili nikakumbuka stori hii
Ni miaka 22 Sasa tokA Jambo hili litokee.
Uliona uwe tu kunguru mwoga kuepusha mbawa. Watu wa aina yake huwa smart sana. Hakuingizi kwenye mtego haraka. Anakujenga taratibu
 
Uliona uwe tu kunguru mwoga kuepusha mbawa. Watu wa aina yake huwa smart sana. Hakuingizi kwenye mtego haraka. Anakujenga taratibu
Plato...
Nini ulikuwa mwisho wa huyu kijana?
Ningependa sana kujua.
 
KISA CHA ''MAGAIDI'' WAWILI: SHEIKH RAMADHANI RAJAB CHAMBUSO NA SHEIKH AHMADA KIDEGE

''Akauliza muulizaji katika kuwahoji kwa shutuma za ugaidi ni nani anawalipa kwa kazi hiyo ya kusomesha Qur'an.

Jibu likatoka kuwa hakuna anaewalipa ila wanaifanya kazi hiyo ili Allah awaridhie na kesho kiama awatie peponi.''

Charles Dickens ameandika kitabu maarufu, ''A Tale of Two Cities.''

Nimechukua jina la kitabu hiki kufanya ndiyo anuani ya hii makala ambayo kwa kweli nimeaindika mwaka wa 2016 lakini nimeona niiweke tena upya watu waisome kwa kuwa muda uliopita unaweza kutufunza mengi ya manufaa katika hili tatizo la Waislam wanaosomesha Qur'an kukamatwa na kufunguliwa kesi za ugaidi.

Kama ilivyokuwa kwa Masheikh wa Uamsho ushahidi haupatikani na baada ya watuhumiwa kuteseka gerezani huachiwa.

Vijana hawa wawili wote ni waalim wa Qur'an na vijana wazuri na wema wao unafahamika na kila mtu mjini Tanga wanapoishi na kufundisha Uislam.

Kwa sifa hizi zao walipokamatwa kwa vipindi tofauti kwa tuhuma za ugaidi watu walisema, ''Si bure kuna jambo Chambuso na Ahmada walezi na walimu wa wanetu hawawezi kuwa magaidi.''

Hili jambo ni lipi?

Mpenzi msomaji wangu makala hii inaweza kukutegulia kitendawili hiki.

Soma na tafakari na ukimaliza kutafakari waombee dua vijana wetu wanaoshughulika na kukisomesha kitabu cha Allah:

"Sheikh Rajab Ramadhani Chambuso ni katika vijana wadogo wa Tanga niliopata kusubiana naye kwa kipindi cha miaka 15 niliyoishi Tanga.

Nilifahamiana pia na mwenzake Ahmada Kidege ambao wote wakishughulika na kusomesha Uislam.

Sheikh Chambuso yeye ndiye alikuwa karibu na mimi zaidi.

Nilimjua kama mwalimu wa Islamic Knowledge akipita shule za sekondari akisomesha wanafunzi wa Kiislam elimu ya dini yao.

Kabla hatujafahamiana vizuri tulikuwa tukipishana alfajr tukifanya mazoezi ya kukimbia Barabara ya Bombo.

Nakumbuka kumuona akitembea kwa miguu shule moja baada ya nyingine jasho likimtoka kwenda kuwahi kipindi mimi nikiwa katika gari yangu na kiyoyozi kinaunguruma.

Wakati ule sikuwa sana karibu na yeye lakini nilipokuja kumzoea nikajafahamu kuwa anasomesha kote mjini na nje ya mji kwa kujitolea.

Haukupita muda alinunuliwa baiskeli na muhisani aliyeguswa na juhudi ile ya kijana mdogo kujitolea kuwasomesha watoto dini ya Allah bila ya malipo yoyote yeye akitegemea radhi za Allah.

Huu ukawa pia ni mwanzo wa uhusiano wangu na Sheikh Chambuso ikawa na mimi kwa namna yangu nasoma kwake kila tunapokuwa pamoja katika mazungumzo ya kawaida tu.

Ukiwa karibu ya waridi hukosi kunukia.

Sheikh Chambuso akanisoemsha historia ya Tanga na taasisi zake kubwa za Uislam kama Shamsiyya, Zahrau na Maawal Islam na baadae Shamsi Maarif ilipokuja kuanzishwa wakati mimi bado nipo Tanga.

Sheikh Chambuso ni kijana maarufu mjini kwa ile heshima yake ya kumtumika Allah na waja wake.

Waarabu wana msemo kuwa, "Anaewatumikia watu ndiye bwana wao."

Wanafunzi waliopita mikononi mwake kuwasomeshsa hawana idadi.

Kupitia Sheikh Chambuso na mimi rafiki na nduguye nikawa nasafiria nyota yake nikifahamika kama ‘’rafiki yake Chambuso.’’

Sheikh Chambuso hakutosheka na kuwa anapita kwenye shule kusomesha akawa sasa anaingia hadi kufanya ushauri kwa wanafunzi wa Kiislam katika wale aliokuwa akiwasomesha dini masomo gani wachukue kwa ajili ya mstakbali wao wa baadae.

Hapa ikawa sasa Sheikh Chambuso anaingia katika anga ambayo kwa hakika ilikuja kuwanufaisha vijana wengi na wengi wao wakafanikiwa.

Lakini kubwa lililokuja kunifurahisha ni pale alipoamua yeye na wenzake kuanzisha shule ya chekechea ya Kiislam na kuanza shule ya msingi.

Sasa tena Sheikh Chambuso akawa anaongeza ulezi juu ya kusomesha.

Madrasa yake na shule ya chekechea ikawa imejaa pomoni.

Mimi binafsi furaha yangu ilikuwa haina kifani.

Sheikh Chambuso akaongeza na ‘’idara,’’ nyingine siyo rasmi akawa anapita kwa Waislam kuwaomba kuwasomesha katika shule yake watoto mayatima na wale ambao wazazi wao Allah amewapa mtihani wa kipato.

Haikuwa ajabu kumuona Sheikh Chambuso amafatana na daktari kumpeleka katika nyumba ili amtie suna mwanafunzi wake ambae kwa shida za umasikini kapita umri wa kutiwa suna.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso.

Siku moja baada ya kutoka Tanga kwa kustaafu kazi nilirudi Tanga na nikenda kumtembelea Sheikh Chambuso shuleni kwake.

Ile kuniona tu na baada ya kusalimiana ghafla akasimamisha masomo katika madarasa yote akawatoa wanafunzi wote nje ya wakapanga mstari ili wanisalimie.

Sheikh Chambuso alikuwa anazugumza na ule mkusanyiko kwa Kiarabu.

Niliyoshuhudia pale niliinamisha kichwa changu chini sikuweza kujizuia.

Machozi yalinilengalenga.

Kumbe mambo haya yanawezekana…

Lakini kuutumikia Uislam kuna changamoto zake hasa nyakati hizi za ''siasa za ugaidi.''

Haukupita muda Sheikh Chambuso akakamatwa na kuwekwa rumande kwa kesi ya ‘’kushawishi mauaji,’’ akawekwa ndani rumande Handeni majuma mawili.

Kasafirishwa kafungwa kitambaa cheusi machoni chini ya ulinzi mkali.

Sheikh Chambuso hana sifa ya uovu mimi binafsi na kila aliyesikia habari hizi alisikitika na kushangaa.

Hii ilikuwa kesi ya kubambikizwa kama ilivyokuja kudhihirika hapo baadae.

Siku ya pili yake zilipopatikana taarifa kuwa Sheikh Chambuso kakamatwa mji mzima wa Tanga ulizizima kwani ni nani asiyemjua Sheikh Chambuso mwalimu na mlezi wa watoto wao?

Ule msururu wa ingia toka nyumbani kwake kuanzia alfajir kuna baadhi ya watu walidhani nyumbani kwake kuna msiba kafa mtu.

Sheikh Chambuso alihangaishwa sana na kesi hii ambayo alinifahamisha kuwa polisi wanaiita, ''kumfunga mtu paka mweusi shingoni.''

Sheikh Chambuso mwenyewe alikuja kunambia kuwa ile kesi imemfunza mengi na imemuongezea elimu ambayo asingeweza kuipata popote.

Kwangu mimi ikawa sasa Sheikh Chambuso kawa shule na mwalimu pia na mimi nasoma kwake na kujifunza.

Hii ilipelekea mimi kuandika mengi kuhusu madhila mengi yanayowakabili Waislam kiasi nilimkaribisha msikiti kwetu aje kuzungumza na Waislam na nilimwekea ukurasa makhsusi kwa ajili yake katika kipindi chote alichokuwa mahakamani kujibu tuhuma za ''kushawishi mauaji:''

Ukurasa huu wa Sheikh Chambuso ulisomwa na watu wengi sana na ulikuwa na taarifa nyingi za uchunguzi kwa kuhusu ukweli wa tuhuma za ugaidi dhidi ya Waislam.

Huwa kila akija Dar es Salaam basi Sheikh Chambuso atanipitia kwangu kunijulia hali na kunieleza shule inavyokwenda na taarifa nyingine za vijana wa Kiislam Mkoani Tanga.

Mara ya mwisho nilipokutananae nilimuuliza kuhusu mwanafunzi wake mmoja bint nillitaka kujua maendeleo yake.

Sheikh Chambuso akaniambia, ‘’Yule bint anamaliza shahada yake ya Udaktari.’’

Kama nilivyotahadharisha hapo awali.

Kabla hatujaagana Sheikh Chambuso akanifahamisha kuwa wamefungua shule ya ushoni kwa wasichana inayoongozwa na Sheikh Khamisi Shemtoi ambae yeye mwenyewe licha ya kuwa sheikh ni fundi cherahani bingwa.

Huwezi kummaliza Sheikh Chambuso na wenzake kila unapokutananao basi watakuwa na jema la kukueleza kukufurahisha.
Kubwa ninalofaidi kwa Shekh Chambuso ni kule kunifunza misemo ya Kiarabu ambayo imekuwa silaha yangu kubwa katika mijadala.
Mathalan siku moja tunazungumza jambo akanipa jibu kwanza kwa Kiarabu kisha akanifanyia tafasiri akasema, ''Ukiijua sababu inaondoa ajabu.''

Kuna mfano mmoja alinipa kueleza jambo lililovurugika na watu kujaribu kulirejesha kama lilivyokuwa hapa mwanzo.

Akanambia, ''Sheikh Mohamed chukua mfano wa kioo kishavunjika na wewe ukajaribu kukiunga, hakiwezi kuwa kama kilivyokuwa hapo mwanzoni.

Ukijitazama na kioo hicho utaiona tofauti.''

Sheikh Chambuso anasema yeye misemo hii kafundishwa na Sheikh wake Marehemu Sheikh Mohamed Ayub.

Siku moja tulikuwa katika gari yangu nikaweka CD ya Sheikh Mohamed Ayub anadarsisha tafsir ya Qur'an darsa za L'Asr Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Msomaji kasoma aya mbili tatu kamaliza Sheikh Mohamed Ayub anaanza kusomesha.
Nikamuona Sheikh Chambuso ghafla uso umembadilika kajiinamia akanambia, ''Sheikh Mohamed mimi hapo nipo sisi wanafunzi wadogo tuko safa ya nyuma mbele pale namuona sheikh mwenyewe kazungukwa na wanafunzi wake wakubwa ambao ndiyo walikuwa walimu wetu sisi, Sheikh Mohamed Bakari, Sharif Sayydid Hussein, Sheikh Zuher bin Ali bin Hemed bin Al Buhry...''

Sheikh Chambuso hakika ni kijana hazina kwa watu wa Tanga na umma wa Waislam wa Tanzania kwa usomi wake makini na jinsi amavyojibiidisha kuitumikia jamii.

Sheikh Ahmada Kidege hivi sasa yuko Gerezani kwa tuhuma za ugaidi na wakati anakamatwa alikuwa anasimamia ujenzi wa hospitali kwa ajili ya wanawake.

Picha: Sheikh Ramadhani Rajab Chambuso akigawa mashafu tafasiri ya Sheikh Ali Muhsin Barwani kwa wanafunzi wake St. Christina Secondary School Tanga
Picha ilipigwa 2006 wakati akiwa Sheikh na Mwalimu ''mtoto.''

Picha ya pili kulia ni Sheikh Chambuso na Sheikh Ahmada Kidege.

View attachment 1822295
Saint Christina!!,Shule ya kiislam!!
Huwa Kuna mstali mwembamba sana kati ya Islamic fundamentalism/radical islamic teachings na Islamic terrorism!
 
Saint Christina!!,Shule ya kiislam!!
Huwa Kuna mstali mwembamba sana kati ya Islamic fundamentalism/radical islamic teachings na Islamic terrorism!
Juan...
"Mstari."
Mimi nafaidi sana hapa kwa kuwa nazungumza kitu ambacho mie mwenyewe ni sehemu yake.

Unaweza ukatia kila aina ya maneno mfano wa hayo "Radical Islam," nk.

Lakini namfahamu Sheikh Chambuso yeye ni mwalimu kasomesha vijana wengi Qur'an na ni mwanafunzi wa TAMTA Tanga chuo kinafahamika na waalimu wake mimi nawafahamu.

Anawafunza wanafunzi wake ucha Mungu na tabia njema kama Uislam ulivyo.

Hayo yaliyozuliwa kwake hayapo na ndiyo maana mahakama ikamwacha huru na anasomesha Qur'an hadi leo.
 
Labda uzungumze kuhusu tanzania.
Duniani na Afrika kwa ujumla kote huko baadhi ya waislamu wanakamatwa kwa tuhuma za ugaidi wa kidini.

Unasikia kinacho endelea Nigeria Somalia, Kenya, Msumbiji nk.

Hivi kwa mawazo yako huko kote Waislamu wanaonewa kwa chuki za kidini ?

Abdalah Shakeu kule Nigeria mwislamu anatangaza hadharani kuwa yeye ni kiongozi wa Magaidi wa Boko Haram.
Moja ya tukio alilolifanya ni kuwateka wasichana wa secondari.

Naye anaonewa ?
Alshababu wa Somalia ni Waislamu wenyewe wanasema hivyo nao wanaonewa ?

Muhamedi ghailan mtanzania mwislamu Mahakama za Marekani zilithibitisha kuwa ni Gaidi na kuhusika kuulipua ubarozi wa Marekani naye alionewa ?

Tukio la Garisa Kenya Watanzania Waislamu walikamatwa live wakiwaua wanachuo kwa maslahi ya Al-Shababu nao walionewa ?

Au wanatakiwa wakamatwe nje ya nchi ndio watakuwa wanatendewa haki ?

Nani alikuwa anamjua Hamza Muhammedi (mwislamu) pamoja na upole wake na kuwa mwanachama wa CCM kuwa alikuwa na mafunzo ya Ugaidi hadi alipo amua kuua Polisi hadharani.

Matendo ya kigaidi ya Kibiti, Kilwa, Mkuranga Amboni Tanga, yote yalitokea kwanye Jamii ya Kiislamu. Magaidi wa kiislamu walijificha huko kwa mgongo wa Uislamu.

Ukweli ni kwamba hayo makundi ya kigaidi ya kiislamu yanawafuasi wake hapa Tanzania ambao ni waislamu.

Mwezi wa 10 mwaka 2022, Polisi huko Zanzibar ilitoa onyo la Vijana wa kizanzibari kuto kushawishiwa na vikundi vya kigaidi kwenda kuchukua mafunzo ya ugaidi baada ya vyanzo vya upeleleze kubaini ushawishi huo.

{Waislamu tengenezeni kizazi kinacho tambua kuwa watu wote wana haki sawa ya kuishi hapa duniani. Kama kuna madai ya kisiasa ziko njia sahihi za kudai ama kwa kutumia wawakilishi kama wabunge au kujiunga na vyama hivyo.

Hadi sasa mimi sioni umuhimu wa kauli za kujiandaa na vita vya Jihadi kunakofunshwa na baadhi ya Mashehe wa Kiislamu.
Jihadi dhidi ya nani ?

Hizi kauli za Waislamu kuonewa bila kitoa uonevu wenyewe ni moja ya vyanzo vya vita vya kulinda jamii flani ya kidini isionewe na ndio Ugaidi wenyewe}

Somesheni kizazi chenu kijikwamue na Ujinga wa kufikiria JIHADI katika hii dunia ya sayansi na technolojia.
Udhaifu mtupu ndo nauona, unawezaje kushangaa dunia nzima kuwa na chuki juu ta uislaam? IBLIS mwenyewe ameahidi kuwa atakuja kuwakalia Waislaam juu ya njia iliyo nyooka na kuwapoteza, hapo hakitaja watu wote maana anajua wasiowaislaam tiyali washapotea sasa awapoteze kwenda wapi tena. Ulimwengu mzima chini ya Kanisa katoriki na Macrusedors wanaendesha nadharia potofu juu ya Uislaam, kama kweli uislaam ni ugaidi mbona hayo matukio hayatokei Makka, Qatar au nchi za mamalaka zibazoongozwa kwa Quran tukifu? Isipokuwa nchi hizi za mchanaganyiko? Hii ni kwamba ni Uwongo unaoandaliwa na nyinyi na mfano mzuri ni wewe hapo unauchukuliaje uislaam kama uuchikulii kuw ni ugaidi,l. Hatutakai kujielezea sana ili mjue mnavyotuchukia kwakuwa tumeambiwa na Allah jkuwa

"𝙄𝙢𝙚𝙠𝙬𝙞𝙨𝙝𝙖 𝘿𝙝𝙞𝙝𝙞𝙧𝙞 𝙘𝙝𝙪𝙠𝙞 𝙮𝙖𝙤 𝙢𝙖𝙠𝙖𝙛𝙞𝙧𝙞 𝙠𝙖𝙩𝙞𝙠𝙖 𝙫𝙪𝙣𝙮𝙬𝙖 𝙫𝙮𝙖𝙤, 𝙣𝙖 𝙬𝙖𝙡𝙞𝙮𝙤𝙮𝙖𝙛𝙞𝙘𝙝𝙖 𝙠𝙖𝙩𝙞𝙠𝙖 𝙫𝙞𝙛𝙪𝙖 𝙫𝙮𝙖𝙤 𝙣𝙞 𝙈𝙖𝙠𝙪𝙗𝙬𝙖 𝙢𝙣𝙤"
Tunawajua wala hamshangazi ila Time will come Uislaam utatawala kila penye kupokea kuchomoza kwa jua.
 
Kama huyu anayejiita Gavana, anaongea kigaidi gaidi tu.
Huyu namtafuta lazima nimtie mkononi.
Nadhani ataisaidia sana Polisi katika mapambano dhidi ya Ugaidi wa kidini.
Unatafutwa na Jehanamu utamuweza anayetafutwa na Malaika Gabriel????

Umeambiw Usome acha kukurupuka Dunia ni fupi mno, there's a time u will return to your Creator. Leta hoja sio, matukio Created
 
Mkuu hao jamaa aya za kitabu chao ndio tatizo,kuna aya zinaruhusu kufanya uhalifu na uhalifu huo huwa kwao ni haki.Tanzania ipo misikiti inayohubiri hayo mambo tena bila kificho ajabu kuna upofu au makusudi fulani hivi ya kujifanya hayaonekani.
Umesahau zile za kuruhusu kunywa pombe ili upungukiwe akili? Umesahau zile za kupeana mkiwa ibadani,? Umesahau kauli ya kiongozi wenu kuruhusu ushoga? Afu akili yko ni ndogo sana, Madamu u katika ushirikina huwezi kuielewa Quran, kawaulize wasomi akina Prof. Amertus Keith Moore, ndo wanaijua Quran maan wanatumia akili sio ushawishi
 
Saudia arabia nchi ya kiisalmu ila anakitengo cha kuzuia ugaidi. sasa jiulize
 
Propaganda na labeling ya suala ugaidi ni gumu sana kwa mfano utasikia tuhuma kua waislamu hujifunza karate misikitini, lakini hawasemi wakatoliki waliojifunza skauti ikiwamo mbinu za kipelelezi na kivita kanisani, haya wakristo wa CAR( central africa republic) wanaowachinja waislamu kama kuku kamwe hutosikia wanaitwa magaidi, wataitwa waasi, M23 kule congo wanaitwa waasi na sio magaidi, lakini Boko haram na Alshabaab huitwa magaidi wakati shughuli zao wote ni sawa na zile za wakristo wanaoitwa waasi
 
Kuna mengi nyuma ya pazia kwa masuala ya uuaji kwa mfano ukiangalia madai ya Boko Haram ni kuitaka rasilimali ziwanifaishe wao pia na sio tofauti lakini sababu wenye maguvu duniani wana vyombo vya habari watapiga kelele na kuaminisha dunia kua habari zao ndio za kweli
 
Akili zenu zinafanana sana.
Nadhani wenyewe kwa wenyewe ndio mnaelewana vizuri.
 
Propaganda na labeling ya suala ugaidi ni gumu sana kwa mfano utasikia tuhuma kua waislamu hujifunza karate misikitini, lakini hawasemi wakatoliki waliojifunza skauti ikiwamo mbinu za kipelelezi na kivita kanisani, haya wakristo wa CAR( central africa republic) wanaowachinja waislamu kama kuku kamwe hutosikia wanaitwa magaidi, wataitwa waasi, M23 kule congo wanaitwa waasi na sio magaidi, lakini Boko haram na Alshabaab huitwa magaidi wakati shughuli zao wote ni sawa na zile za wakristo wanaoitwa waasi
Ninkweli kaka, lakini wnapangabna Mungu anapanga, naye ni mpangaji zaidi 𝘼𝙡 𝙖𝙣𝙛𝙖𝙖𝙡
 
Kwasbabu huna hoja, unajua ni ngumunmno kujadiliana na mkristo mmoja hasiye jua lolote kama wewe kuliko wachungaji melfu ambao walau kidogo wanajulua Biblia!
Mambo ya Biblia yametoka wapi kwenye hii Mada.
Akili zenu zinafanana sana
 
Planet...
Kesi ya ugaidi mahakamani na hukumu ikatoka kumuadhibu gaidi kwa kosa lake.
Nakutafutia ila naomba unijibu swali langu. Wale walioua polisi nane kule pwani na wakaiba silaha ni majambazi au magaidi?
 
Back
Top Bottom