Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #261
Kwanza mtu alieelimika hawezi kuendeshwa na mitazamo ya dini.
Msomi ni mtu aliehuru kutafakari kila hatua ya maisha na jamii yake.
Msomi anaeshiriki katika uharifu huyo kashiriki kwasababu ya "usomi" wake.
"Usomi/Ujuzi ndio kigezo kilichomfanya ashirikishwe kwenye uharifu husika.
Jamii ya sasa, jamii ya dunia kuwa kama kijiji kimoja hatutaraji kuona tabia za 'kipindi cha dini kushika hatamu'.
Kipindi ambacho viongozi wa dini walikuwa viongozi wa serikali pia. Kipindi ambacho dini na serikali zilifungamanishwa pamoja. Kipindi hiko, usingeliweza kuwa kiongozi wa serikali bila kuhusika katika uongozi wa dini.
Mataifa kama Afghanistan, Iraq, Iran ambayo bado mfumo wa uongozi wa serikali umefungamanishwa na dini.
Huyu mzee said, nilishampuuza kitambo. Na lolote limkute. Mzee mbinafsi sana, kwasababu familia yake haikuingizwa kwenye 'mfumo' baada ya Uhuru basi mfumo huo ni batili na haupaswi kuungwa mkono.
Sent from my SO-01J using JamiiForums mobile app
Msakaa...Kwanza mtu alieelimika hawezi kuendeshwa na mitazamo ya dini.

''Uhalifu'' si ''Uharifu.''
Maana ya kupuuza ni ''kuacha usishughulike.''
Ungekuwa umenipuuza usingenitaja hapa.
Ungekuwa kimya unaendelea na hamasini zako.
Si rahisi kunipuuza mimi.
Sababu ni kuwa nimekuja na elimu mpya ambayo kabla haikuwapo.
Elimu hii mpya katika historia ya Tanganyika imenifanya nialikwe kwenye vyuo vingi kuzungumza Afrika, Ulaya na Marekani.
Nimeshirikishwa katika uandishi wa vitabu kadhaa kuhusu historia ya Afrika tena na wachapaji wakubwa kama Oxford University Press, Nairobi na New York na wengine kutoka Afrika ya Mashariki.
Ndiyo nikakuambia si rahisi kunipuuza.
Wala mimi sizungumzi dini.
Nitakupa mfano.
Katika historia ya uhuru wa Kenya huwezi kuacha kuwataja Mau Mau kwa sababu ya mchango wao katika kupambana na ukoloni wa Waingereza.
Kuandika historia ya Mau Mau huwezi kuita ni ukabila.
Halikadhalika uhuru wa Tanganyika umechangiwa sana na Waislam.
Kuandika historia hii haiwezi kuwa udini.
Udini nio pale itakapo kataliwa kwa kuwa ni historia inayowahusu Waislam.