Titicomb
JF-Expert Member
- Jan 27, 2012
- 12,823
- 21,210
Huyo mtuhumiwa ni dada yetu huku mtaani kwetu.Nadhani wewe utakuwa mchawi. Acheni mafisadi wanyooshwe
Hizi siasa zinaingizwa tu hata kama alimchangia Lissu yeye tayari alikuwa yupo kwenye makabrasha ya TAKUKURU.
Huyu dada yetu na mumewe wanatuhuma nyingi sana za kudhulumu watu kwenye kampuni yao kukopesha fedha na tuhuma zingine.
Wanaojua wanasema ulikuwa ukikopa kwao ukaweka nyumba ujue hutaweza kulipa deni hata iweje na mwisho unapoteza nyumba yako.
Hata akiondoka Magufuli huyu dada kesi yake na mumewe itawasakama tu. Hivyo akimchangia Lissu bado haitamsaidia.
Kiufupi kama hajafanya hayo anayotuhumiwa nayo tumuombee avuke salama kipindi hiki apate njia ya kujisafisha jina lake.
Hizi siasa wanazo ingiza ndio zitaofanya kesi yake iwe ngumu au serikali ipeleke hati ya kukamatwa kwake Interpol. Sky Eclat hapa haumsaidii dada yetu unachochea moto wa kusababisha akamatwe haraka na Interpol.