Kisa cha Magufuli kushindwa kumuwajibisha Makonda, Ukweli uliofichika sasa hadharani

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
20,925
Reaction score
51,688
Tunaendelea na visa na viroja vya Rais mstaafu JPM.

Baada ya kisa cha kumtimua Balozi Ombeni Sefue usiku na kisa cha kumpa masharti Yahya Msigwa aliyekuwa Rais wa TUCTA kuwa atulie asimsumbue sababu anatumia jina la marehemu kwenye vyeti vyake vya kitaaluma, leo nawaletea kisa kingine toka korido za Ikulu kikimuhusisha Bwana Paul Makonda RC mstaafu wa DSM.

Yanasemwa mengi kuhoji uswahiba wa hawa watu wawili, wengine wakisema ni sababu wote ni home boys toka kanda ya ziwa ila wanasahau Dialo na Kitwanga pia ni home boys ila aliwatema peupe.

Wengine wanadai ni mambo ya kishirikina eti Makonda alimletea kikundi cha wachawi na waganga kuagua mashetani yaliyoachwa na mtangulizi wake Ikulu ya Magogoni hadi kushindwa kukalika.

Hizo zote ni nadharia ukweli huu hapa.

Itaendelea
 
Wengine wanadai ni mambo ya kishirikina eti Makonda alimletea kikundi cha wachawi na waganga kuagua mashetani yaliyoachwa na mtangulizi wake Ikulu ya magogoni hadi kushindwa kukalika.
hii si urongo, Bashite alileta wataalam toka Usumani kumzindika Mzee baba aka Jiwe, ila Bashite kujiwekea uzio akamwambia mganga awape dawa pamoja na Jiwe awaapishe kwamba ili dawa ifanye kazi basi wasitosane hadi uongozi wa Jiwe ukakapokoma - hapo ndipo ukawa mwanzo wa uswaiba mpya wa Bashite na Jiwe.

Ni kweli Bashite aliutaka Ubunge sababu alijua Jiwe hata akimpiga mkwara namna gani hawezi kuvunja mwiko wa mganga, Kweli Bashite akapigwa chini na Jiwe - na sasa Jiwe yupo wapi?
 
Mbongo mpe picha tu atakutungia story yote yeye mwenyewe.
 
hii si urongo, Bashite alileta wataalam toka Usumani kumzindika Mzee baba aka Jiwe, ila Bashite kujiwekea uzio akamwambia mganga awape dawa pamoja na Jiwe awaapishe kwamba ili dawa ifanye kazi basi wasitosane hadi uongozi wa Jiwe ukakapokoma - hapo ndipo ukawa mwanzo wa uswaiba mpya wa Bashite na Jiwe.

Ni kweli Bashite aliutaka Ubunge sababu alijua Jiwe hata akimpiga mkwara namna gani hawezi kuvunja mwiko wa mganga, Kweli Bashite akapigwa chini na Jiwe - na sasa Jiwe yupo wapi?
Kwani waganga walikuja kufukuza majini ya jk ama kuwaunganisha?

Maelezo yako hayaendani na ya mleta siredi.
 
Back
Top Bottom