Sema wewe... ndo maana mwanzoni kabisa nami nikasema huo ni UONGO kwa sababu naifahamu Mafia vizuri sana! Home kwetu ukikaa dirishani unaona uwanja ambao Wahubiri wa Kikristo kibao walikuwa wanaenda pale wanatoa mahuburi ya Yesu ni Mungu lakini hawakuwahi kubughudhiwa hata siku moja!!Kiukweli Mafia mnayoisema mie siielewi ni ya wapi? Mie ni mkristo na nilipoenda mafia sikutegemea hata kitimoto ningeikuta Ila wazee Kuna pub na jamaa anatengeneza mbuzi katoliki safi sana na Kuna mangi mmoja anachoma mbuzi safi kabisa pale Mafia.
Haya mengine ni maneno ya kipuuzi ubaguzi huwa unakuwepo tu sababu ya kutozoea aina fulani ya maisha hata jamii ya kikristu huwabagua wengine sababu wanakuwa na Ile cultural shock ni Jambo la kawaida ambapo baada ya muda unakuja kuzoea tu.
Huu mchanganyiko wa jamii ndio husababisha watu kuzoeana na kuchukuliana na kuheshimiana Kama jamii iliyostaarabika ndio maana mzungu alipokuja alipewa maeneo na akakaribishwa akae wakajiweka kwenye maeneo yao kwa kuwa wenyeji wakiona Kama life ya wazungu ni tofauti.
Hata wahindi walipokuja nao walijitenga maeneo yao ya uhindini na wao kwa wao walijitenga unakuta wabohora Wana mtaa wao, jamatii Wana mtaa wao, waishamilia Wana mtaa wao, wasunni hivyohivyo basi ni ilikuwa wanaishi sababu ya kutozoea imani na maisha ya kila mwenzie.
Ila Mafia nguruwe nyama ipo Safi anayebisha aseme so huo ubaguzi wa kidini sijui na kama upo basi wa kawaida kwa familia na familia usigeneralize sheikh.
Na ule uwanja unapakana na Madrasa, kwahiyo wakati Wakristo wakiendelea na mahubiri yao, madogo upande wa pili wanasoma Quran lakini hakuna anayesumbuliwa!!
Pembeni tu mwa huo uwanja kuna Kanisa la KKKT, na limezungukwa na makazi ya Waislamu, lakini sijawahi kusikia wakibughudhiwa hata siku moja! Ukitoka hapo, ukashika barabara ya kwenda kwa akina Mzee Mwishehe, njia unakutana na baada, na inamilikiwa na Mkristo na ipo hatua chache tu kutoka ilipo Madrasa!
Ukifika pale kwa akina Mwishehe kwenyewe, kulia mzee Mwishehe, kushoto shemeji yake Idarous, kaskazini Mzee Idarous mwenyewe, na jirani yake wakati ule alikuwa Mama Mcaddam... wote hawa ni Waislamu lakini pembeni yao tu kulikuwa na baa!!!
Kwahiyo ni kiroja hasa kusikia mtu akisema eti Mafia kuna ubaguzi mkubwa wa kidini! Kwanza kama unataka kutaja maeneo yenye uvumilivu wa kidini Tanzania hii, Mafia inaweza kuwa among the top!!