Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mke mwema hutoka kwa Mungu. Hiyo no. 3 nimeona mashemeji zangu wakilia na wake zao wametoka wote kijiji kimoja. Ukitaka mke mwema shirikisha Mungu ila ukitumia akili zako unaweza pata balaa.Ushauri wangu Ni huu
1. Oa rafiki yako
2. Oa kutoka the same background
3. Oa mtu wa kwenu
4. Mkeo asikuzidi kipato
5. Epuka kuoa makabila usiyojua Mila na desturi zao. Wachaga wananielewa kwa hili
Unapigwa kipapai unatulia kama maji kwenye mtungiHuyo mwanamke hajakutana na chizi mimi. Mwambieni ana bahati sana kutoolewa na Soldier
Brother umemaliza kila kitu.Adui wa kwanza wa MWANAUME ni mwanamke, na hii watu wengi watasema ni ushirikina,sio kweli, kwa Wengi wenye wake wanalijua hili, girl friend au mke anataka kwanza kukuchunguza na kukujua kwa kila unachofanya na unakokwenda, baada ya hapo anaanza kukupangia anachotaka yeye, na ukikataa utaitwa mkorofi, ana mahawara,mnyanyasaji, anaharibu pesa,mbishi, na kuitiwa vikao, yote hayo ni kukuogopesha ili jamii na wewe mwenyewe ujione mkosaji na aibu, Ukishakubali hapo MWANAUME utakua mtumwa.
Suluhisho ni kuhakikisha anapanga mambo yake mwenye na kufukuzia goals zake za maisha, Pesa Yake aweke mwenyewe na apangie mwenyewe. akiona anaendelea na ubishi. amwache kwani Maisha yake ni bora kuliko huyo mwanamke.
Hapa ndio ataharibu ndugu wanaweza kufukuzwa au kuundiwa zengwe wakatengeneza ugomvi wa maisha wasiongee tena na jamaa. Na hapa wife atakuwa ameshindaUnawafahamu ndugu zake? washirikishe..
Hahahahahaaaaaaa sio mimi mzee babaUnapigwa kipapai unatulia kama maji kwenye mtungi
Inawezekana mke ana'blackmail' huyu jamaa! Mie nafikiri angejilipua tu ili aondokane na madhira hayo! Ukweli utamuweka huru!Dah,msaidie ndugu yako aseee,amefungwa hata kama kuna kupangiana mshahara si kwa staili hyo inamaana,labda tuseme labda kuna siri anamtunzia maana mambo ya family huwez jua lakini hata kama ni hivo basi hamna faida huo ni ukatili,asa kama ni hyo hela tu anapata vipi kuhusu ndugu zake
Ipo sana mkuu, nilishawahi fanyiwa hii kitu, usiombe ikutokee, kuna jamaa tuliyokuwa tumeoa kwenye hiyo familia, ukimuona utamhurumiaNajaribu kuingiza akilini hii ishu ila inagoma bwana wee.
[emoji16][emoji16][emoji16]Ndo maana mimi sitaoa Forever ushenzi gani huu tunafanyiwa na Madem.
[emoji16]Tastes like Tea.
It's probably Tea.....
Oh My! It is Tea!!
[emoji16][emoji16]Keep left then..!
[emoji16][emoji16][emoji16] Friedrich Nietzsche aliwahi kusema kwamba Wanawake Ni Kosa 2 la Mungu kutenda ktk uumbaji wakeMi naona baada tu ya Hawa kumwaribia Adam pale Bustanini Mungu angemrudishia tu Adam Ubavu wake aendelee kuwa na Wanyama maana huyu kiumbe(ke) bado anasumbua..
Nasema uongo ndugu zangu?
[emoji16][emoji16][emoji16] Yaani kasema kabisa??Kama huamini unajidanganya
Haya mambo yapoo tena sana
Huyo kalishwa limbwata
Kuna mama mtaani kwetu mpika chapati maarufu siku asubuhi wakati tunasubiri atoe chapati mumewe alikuwa amekaa pembeni
Huyo baba siku zote huwa namuona amekaa kibalazani kwake anasalimia watu tu
Huyu mama akamfokea aingie ndani au akatafute shughuli ya kufanya
Akatuambia wanangu msije mkampa mwanaume limbwata utamuathiri akili pia ona huyu wangu nilimpa anipende awahi kurudi nyumbani matokeo amezubaa mpaka amekua mzigo,kazi hana wala hajiangaishi
Nikajifunza kumbe limbwata ni mzigo badae [emoji848]
[emoji16][emoji16][emoji16] Yaani kasema kabisa??
DuuuKuna watu hapa duniani wanapitia maisha magumu kwenye ndoa.
(Samahani mimi sio mwandishi mzuri wa story)
Kuna mwenzangu tulisoma naye O level, mimi niliendelea A level na yeye akaenda DIT kipindi hicho ikiitwa Dar Tech, hatukuonana miaka mingi sana na sikujua yupo wapi. Kwa bahati tu nikawa nimepata uhamisho kwenda ofisi nyingine, nikamkuta jamaa pale ofisi na ana madaraka makubwa kuliko mimi.
Na wafanyakazi wa pale anawanyanyasa sana ila wakaona kwangu ni tofauti kabisa akiniona au akiwa anatoa majukumu kwangu huwa anakuja kuniomba labda kwakuwa najua kila kitu chake na najua uwezo wake kwenye fani ile maana tuna fani moja.
Nikaambiwa huyo bosi hana ushirikiano na wenzake hata michago ya kijamii hatoi, kwahiyo watu wanamwangalia tu ngoja apatwe na tatizo tutamkomesha haswa. Kusikia hivyo nilishtuka sana ila nikasema labda ni maneno ya watu kwakuwa ni mgeni.
Pia niliambiwa kuwa hawajawahi kumuona anakula chochote mpaka anatoka kazini.
Kuhusu chakula nikanza kwenda ofisi kwake kumwita kuwa twende tukanywe chai na chakula kwa muda wa wiki hivi akagomesha kuwa hanywi chai wa chakula kwenye restaurants za hapa kazini kuwa sio safi kumbe alikuwa anaogopa kununua.
Ikapita kama mwezi nikamwambia twende tutoke nje kuna sehemu nimeona chakula kizuri nitakununulia jamaa akakubali kwa shingo upande tukaenda tukala, kesho yake ikawa hivyo hivyo na kuendelea, mpaka ikafika muda akawa anakuja ofisini kwangu kuniambia twende kula ila yeye ni kuagiza tu kulipa ananiangalia mimi ndo nilipe ikaenda kama kwa muda wa miezi miwili na nusu kama sikosei kwa hali hiyo mpaka nikasema kumbe nilifanya kosa kumwambia siku ya kwanza nitakununulia chakula.
Ila nikajipa moyo kuwa mbona nyumbani nina watu wengi na sio watoto wangu ila wanakula na kushiba na wala sijafirisika, ngoja tuende hivyo hivyo pia muda wangu wa kukaa pale kazi ikuwa unaisha narudi kofisi za mwanzo ko isinipe tabu.
Kuna siku tukiwa tunafanya kazi moja nikaamua kumueleza jinsi wafanyakazi wenzake wanavyomsema kuhusu kuwanyanyasa na kutokuwa na ushirikiano katika mambo ya kijamii, alishtuka kiasi akasema kwa mshangao, "kumbe!''
Akawa kama mtu aliye changanyikiwa akaongeza sauti ya juu kuwa achana na wale hawana elimu niwajinga tu na hawanisaidii chochote.
Nikamwambia hapana kuna umuhimu wa kukaa vizuri na jamii maana unaweza ukapatwa na tatizo ikashindikana kusaidiwa, nikampa mfano itokee mtoto wako au mke wako amepungukiwa damu na wafanya kazi wenzako wakagoma kujitolea utajisikiaje?
Hapo akatulia kwa muda bila kuongea na mimi nikajifanya nipo busy na simu yangu.
Baada ya dakika kama tano hivi akanimbia wewe kweli ni rafiki mzuri umeongea jambo jema huku akionekana ubongo wake kama ame RESTORE TO FACTORY SETTINGS.
Akaniamia ngoja nikuambie rafiki, sio kuwa sipendi kushirikiana na wenzangu ila saivi sina pesa angalia hata uvaaji wangu sio ule ulionizoea.
Hapo nikashtuka tena huyu mtu anaongelea nini wakati mshahara wake umenizidi kama 500k kutokana na madaraka aliyonayo pia ana allowance nyingi kuzidi mimi? Ikabidi nicheke na kusema acha utani ndugu.
Akanza kujifikicha macho kama mtu anayejifuta machozi na sauti ikabadilika kuwa ya upole na kuanza kuniambia kuwa yeye hana madaraka na mshahara wake wala posho zake bali mke wake ambaye ni mama wa nyumbani yeye ndo ENGINEER wa mambo yote.
Akaendelea kusema kuwa yeye ana pewa elfu 45 tu kama nauli ya usafiri, na anaambiwa kuwa chakula akale home tu, akifika huwa ananushwa kama amekula huko nje na ikigundulika hapewi chakula siku hiyo nzima.
Pia akaniambia ndo maana kila akila nje lazima apige mswaki ili mke wake asijue maana hata akila muhindi tu ni shida. Na wakati mwingine huwa anatembea kwa mguu umbali wa lisaa na nusu akikosa nauli.
Nikampa mpole huku nikishangaa maisha anayopitia mtu anaye pata mshara wa 3M.
Nikamuliza una nyumba ngapi maana gari nilijua hana, kwa Ubahili huo na muda alio fanya kazi ni mrefu maana aliajiriwa akiwa na diploma ila alijiendeleza akiwa kazini.
Akanijibu bado amepanga ila gari alimnunulia mke wake na hairuhusiwi yeye kulitumia kwa shughuli yoyote ile labda mke wake ndo ampeleke na gari.
Akaniambia kuwa akifika nyumbani huwa hana amani pia anamuogopa mke wake kama yupo na simba nyumba moja, ndo maana huwa anachelewa kutoka kazini.
Nikamuliza unaishi vipi na mtu unaye muogopa? Akasema akiwa huku nje huwa hogopi na unakuta anapanga akilini mwake kuwa nikifika home nitaenda kufanya mapinduzi na kumfukuza mwanamke ila akifika tu home anakuwa mnyonge ila anakuwa na uelewa wa kwake kabisa ila anamuona mke wake kama simba.
Pia yeye akaniuliza sijui nifanyaje, ingawa siku hizi uwoga umeanza kupungua kiasi chake na anaweza kubishana naye ila kwa uwoga sio kama mwanzo ambapo kila kitu ni kuitikia kwa kichwa maana alikuwa anaogopa kutoa sauti asije pigwa na mke wake.
Tuliongea mengi na mwishowe nikabaki kuumpa pole tu nilishindwa kumpa ushauri wowote, na muda wangu wa kukaa hapa umekaribia kumalizika.
Sikuamini niliyo ambiwa ila kweli kuna watu wanapitia magumu katika ndoa. Muombe Mungu yasije kukukuta ya kupewa 45k out of 3m kwa mwezi.
Sasa huyo mama ana mloga mumewe na kuchukua mshahara wote wa mume na kuutumia hovyo mwisho watazeeka hawana hata kibanda, mwanamke tu kuwa mama wa nyumbani hauzi hata vitumbua Mimi naona ana tatizo kichwani, hivi siku huyo mume akiondoka duniani watoto si wataharibikiwa? Ni ujinga kumloga mwanaume ka kichwa Cha nyumba Kuna makabila sio ya kuoa ni wajinga Sana unalilia mshahara wa mume uutumie huanzishi hata biashara mfyuuu kabisaHiyo ndio faida ya kuoa mafundi vitatandani badala ya kufuata ushauri wa wazazi. Wazazi wanapokushauri huwa wanaangalia vitu vingi ktk familia husika unayotaka kuoa, mfano wanaangalia vichache vifuatavyo.
Uchawi ktk familia
Magonjwa ya kurithi
Uvivu ktk familia
Tabia za familia
Uchamungu wa familia
Mahusiano na jamii nk.
[emoji16][emoji16]Aisee mswahili Sana huyu mamaKashamchoka hapo akajikuta karopoka [emoji28][emoji28]
Nikabaki kushangaa
Ni kama miaka 10 imepita tulihama huo mtaa sijui kama bado wapo pamoja sija fatilia
Ukiwa na watoto wakiume inabidi uwaombee Sana ndo Mana mama dangote ni mkali KWA mwanawe na hivi ni maarufuUna uhakika na hili mkuu?? Ili niitunze kwa matumizi ya baadae kwa wanangu ikitokea wakafanyiww km rafiki wa mtoa mada