Kisa kazi, mchumba wangu amenisaliti

Poleni na majumukumu.

Mimi ni kijana wa miaka 29. Miaka kadhaa yuma nilipata nafasi ya kwenda kusoma nchi fulani. Huko nikakutana na binti mmoja tukaanzisha mahusiano...
Kunguru hafugiki achana naye huyo hafai
 
Dogo sikia mwanamke moyo wake tunahitaji baunza pembeni yake, hivyo ww kkuwa mbali ilikuwa sababu, huyu Bibi usimwache kaa anayee umtengeneze utakuwa mke bomba, mke akiwa vacuum lazima hilo lijamaa lilitumia hiyo chance
 
Hivi kwa ushahidi wote huo toka kwa mhusika mwenyewe bado unafikiria mumsamehe? Wewe mtu wa namna gani ndugu? Mungu ashakuonesha huyo hakufai piga chini.
 
Dah aisee ni ngumu Sana kumrudia Mwanamke msaliti.Asee
 
Hii ni thread Bora Kwa mwaka huu.Naimani watu Wengi mmejifunza vitu vingi sana kama Mimi nilivyojifunza.

Ila nasema hivi.Msaliti dawa yake ni kumuacha.Kulia Lia kwako ni kutaka kufuta Aibu.Bro Wanawake wapo wengi Sana,Mwenye kukupenda hawezi kufanya Ujinga huu.
 
Bro Kuna kitabu nilisomaga ndani ya hicho kitabu kuna mahali kulikua na jamaa anampa ushauri aliyefunga ndoa na nukuu tu "Shida haipo kwenye kuipanda/kuikwea nguzo ya chuma iliyopakwa mafuta,shida ipo kwenye kuendelea kuwa juu kileleni kwa wakati wote wa mahusiano,Kupanda nguzo ni mara moja ila kwenye kuendelea kuwa juu kileleni ni swala jingine"
Hivyo Basi nakupa ushauri kwa namna ya kuuliza majibu utakayo pata utajua nini cha kufanya.

Ndani Kabisa ya moyo wako kuna mapenzi/upendo umebakia?

Je kama wewe ungekua kwenye situation yake ungeweza resist vishawishi ?

Sababu ya yeye kufanya hayo kusaliti ni nini?

Je, katika mahusiano yenu ya miaka mitano haujawahi kusaliti ?

Kuanzisha mahusiano na kumrekebisha huyo uliye naye toka kitambo ambaye nadhani mengi mliyajenga pamoja na mli plan?

Je, anaonyesha kujutia kitendo chake?

Je, anaweza akarudia tena alichokifanya kwenye future?

Mwisho
nataka nikwambie kuanzisha mahusiano mngine sio kitu kigumu lakini hautapata amani hata kwnye mahusiano mapya utakayo anza,Waswahili wanasema uking'atwa na nyoka hata ukiona jani unastuka,dhambi ya usaliti ya huyo mwanamke itakuathiri hata kwnye mahusiano mengine.Unaweza ukaamua kumpa physiological torture ambayo akiweza kuivumilia utaendelea nae.

But rafiki yangu wewe ndo unayemjua huyo mwanamke kuliko mtu mwingine sisi niwashauri tu!Mwisho wasiku wewe ndo ulikua nae!Pengine aliteleza na atajifunza na anaweza kuwa bora sana kuliko ukianza na mwingine ambae anaweza rudia hicho hicho .Mwenye maamuzi ya mwisho ni wewe,wewe unamjua zaidi kuliko mwingine yoyote fanya maamuzi kwa busara ila kumbuka wewe unaweza mtengeneza akawa bora​
 
Sikiliza moyo wako maana wewe ndio unaelewa unajihisi vipi kumuhusu bidada...
 
Sio kwamba nakubeza au nakudharau hapana ila nawaza inawezekana vipi Malaya kama huyo ukaendelea muita mchumba and so on...?mpige chini hiko ni kichaka cha wenye hamu.
 
Mle shoo kwanza zile za kibaharia kisha piga chini, ushahidi wa voicenote akikiri hilo la kuliwa papuchi usisahau, huyo ni aina ya mademu wanaoliwa na wengi maisha yao yote. Kuwa mrahisi hasa kuwaamini watu haraka sana na huruma iliopitiliza, huruma ni umalaya usiokikomo na imani ni kukosa selfu defense-thinking na decisions.
 

Utaishia kulipa mahari na kufunga ndoa ila mzigo itaendelea kuliwa na huyo njemba.

Miezi mitatu kwa matukio yote hayo? Kwa mtu uliye na malengo ya kufunga ndoa naye umsaliti kindezi hivyo tena na mtu asiye na cheo bali vitisho?!

Hapo hakuna mke. Ila wewe ndiye mwenye maamuzi.
 

Umeongea mengi ya msingi,lakini kama wewe ni Mwanamme Vaa uhusika wa mwenzetu huyo.Ki ukweli Mwanamke anayekupenda Kwa dhati hawezi kufanya Ujinga wa aina hiyo.Mwanamke msaliti ni Malaya tu,Tabia haina dawa,atamuoa ataliwa nje kama Mwanzoni kwenye uchumba.Matokeo Yake ni kuumizana tu.
Huyo ni kuachwa tu,Wanaume Huwa tunadanganyika Sana kirahisi na machozi ya Wanawake.Lakini ki ukweli Mwanamke chozi lake sio la kuliamini.
 
Utamuua ndugu yetu huyu kwa presha
 
Achana na huyo malaya wewe!
Mwanamke anayejielewa hawezi kutoa penzi on your absence.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…