Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Aisee!!? Unajutia kwa mambo aliyojitakia mwenyewe?
Mkuu

Nachoona Jamaa ana weakness ya huruma kupita kiasi

Hili tatizo la absent fathers lipo kwa kila mtu mostly.

Na aliyopitia wamepitia wengi mostly dealing with useless absent fathers when they had time to take care of their kids

Hicho alichokipata baba yake ni natural feeback of what he supposedly hasnt done to his kids.

Reaction ya huyu jamaa ni very logical and proper kabisa...A grown up son can not let her mother be bullied yeye akiona...natural instincts can never allow that.

Mother ni biological extension of her sons,any pain she has is naturally extended to her sons.Sons will never allow their mother be pushed that way.

Situation yake ilikua ni lazima achague upande unaoonewa ambao ni wa mama,angechagua upande wa baba ambae ni bully sidhani kama angeweza kuishi na hiyo guilty consciousness,

Hii guilty anai-feel sasa ya upande wa baba ni lightweight kabisa na ninaona ni best choice he has done!
 
Habari wana jf,

Kuna mambo wakati mwingine huyaona ya kawaida ila ukifikiria kiundani unagundua kuna majuto ndani yake..

Niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja ana duka kkoo tunalingana umri lakini yeye aliolewa na mwanaume umri umeenda sanaa,
Tulianza kama masihara namuuzia bidhaa flani za mchongo, kuna kipindi akawa na upungufu wa wafanyakazi akaniomba niwe namsaidia siku akiwa na oda kubwa mwishowe akanihodhi mazima nkaacha biashara zangu (maduka ya mtaani yalikua vizuri tu) nilizokua nasimamia mwenyewe akasimamia mdogo angu kwa wazo nipige huku nae apige kule tukuze uchumi wa familia baadae, maana mshahara ulikua mzuri sana kipindi hicho kwangu.

Miezi kadhaa baada ya kunikabidhi duka moja akanitongoza nkajikuta nimeingia 18 zake, (ifahamike sikukubali sababu ya pesa zake bali uzuri wake na pesa hakua nazo maana kipindi naingia mimi wafanyakzi walishamfilisi kabaki mweupe maduka ma2 lkn mizigo hakuna) mapenzi yalikua moto moto kweli adi mitaa ya kazi kkoo walijua hilo, akanifosi nimuache mpenzi wangu tuliependana sana nkafanya hivyo (ila sasa ndio mke wangu baada ya kuachana miaka mi3) na alikua na wivu kupindukia, tulikua bize na mapenzi kuliko kazi, akiwashwa asubuhi mnaenda stoo, akiwashwa mchana mnaenda stoo akiwashwa mida ya jioni mnawahi kufunga kabla ya mda wa kawaida tunaenda gheto kwangu... Yaani ilikua ni vurugu tupu ndani ya miaka miwili lkn mimi sikusahau wajibu wangu nilipiga kazi ivoivo, nkamshauri afunge duka moja tukomae na moja akafanya hivyo, mi nawaza kazi ili nitoke kwenye umaskini yeye mda wote ni mapenzi tuuuu, ilipekea adi kufunga biashara zangu kwa kua mdogo angu nilimpa uhuru kama zake akafilisi.

Akanipa moyo tutafungua mengine tu,
Miaka mi3 inaishia hakuna la maana nililofanya zaidi ya kumjengea mama angu nyumba ya vyumba vi2 hapa dar,
Nkaanza harakati za kumkataa haikua kazi ndogo tuligombana sana adi ilifikia kipindi nkamshikia kisu aniache na maisha yangu ajabu akaenda kuwafata wazazi wangu kuwaeleza kilichotokea, niko gheto naskia gari inaingia uani kuchungulia kawabeba mama na baba, nkajiuliza hajui kama yeye ni mke wa mtu tena wa ndoa?
Nkajifungia wakaita weee nkawa kimya wakaondoka,

Tukaja yamaliza mambo yakaendelea,
Nkamtafuta zilipendwa wangu kama zali huyu hapa tukawekana sawa tukaendelea tulipoishia, mke wa mtu kuja kujua ikawa balaa tena tuligombana sana adi siku 2 hatukufungua duka akawa anatukanana na mpenzi wangu sana nae alishaambiwa niko na jimama lakini hakuniacha wakawa wanajibizana wenyewe kwa wenyewe.

Adi sasa hivi niko na huyo mke wangu mwaka wa kumi huu na kazi bado nafanya kwa huyo dada, kuna mambo yalitokea hadi ikwezekana kua hivyo sema siwezi yaweka hapa naeza fungua code maana huyo dada ni mtu maarufu eneo flani au hapa dar na stori zilijulikana sana.

Najutia kwa kua pengine ningekua na maisha mazuri zaidi ya niliyonayo sasa maana alinifanya nkawa napenda sana wanawake + nyota ya kupendwa kwa kua nilikua na kipato nilizalisha wanawake wengi sana ambao sasa hivi kipato nnachopata kinaishia kwenye kutunza baadhi na bado nna familia ya watoto wa4, pengine ningetulia na mke wangu tangu kipindi kile ningeendelea na displing niliyokua nayo ya kuheshimu hela na kufanya maendeleo lkn kupitia uhuru wa kuachiwa duka (tukiwa kwenye mahusiano hadi sasa) kulinifanya niwe na tabia ovu ambayo sikua nayo kabla sijaingia kwenye mahusiano na huyu dada.
 
I will never zalisha nje god forbid

Nimeona what happened to my dad,and he died uzeeni sababu ya pressure of watoto wa nje

Alijuta sana....

Nitavaa kondom mpaka **** ichubuke....
 
Tatizo pale kati patamu bwana
 
Mkuu

Still una soft spot for your father..which is okay....

Ila hiyo huruma uliyonayo kwake isije ikawa kwa gharama ya kumuumiza maza wako tena

Treat them separately as separate human beings....

Obviously bias ni kwa maza zaidi,which is okay obviously.

Tatizo unataka kumuona mtu huruma kwa kumuumiza maza wako eti sababu it happens anaitwa "baba"....your biological instincts will never allow that.

Cha ajabu una feel guilt kwa kufanya the right thing......hutakiwi ku feel any guilt mzee....I dont see any guilt anywhere

Sema labda kuna experience uliyoimiss ya kua na baba ndio maana you constantly looking for his approval,na hiyo inakufanya uone kama upo nae mbali na unaona guilt inakusumbua

As a grown man make decisions and live with them with their consequences!

No need kujikomba komba mzee!
 
Hii hali ipo sana kwenye African families zetu

Ndio maana wazungu wanatuzidi kwenye sekta hii ya familia.....

Tujifunze sana aisee
 
Kuna stori kama hii niliambiwa. Mshua alikuwa wa mkoa wa Mara
 
Mimi najuta kumdharau mtu..nimejifunza usimdharau mtu yoyote kwenye maisha yako. Maana huwezi kujua kesho yake. Wakati nipo mdogo, nilikuwa naishi na brother mkubwa, na mabraza wengine wanaomfatia. Sasa kwasababu yule braza mkubwa ndo alikuwa Sterling, hawa wengine wanaomfatia nilikuwa nawachukulia poa sana. Siku moja nilikosana na braza yangu mmoja, kwasababu alikuwa hana kitu nikamwambia huwezi niambia kitu maana hutokaa unisaidie kitu maishani. Aloo... Muda ukaenda yule braza yangu mkubwa niliekuwa namtegemea akafariki, halaf yule niliekuwa ninamdharau ndo akaja akapata hela ya maana na kunilea, kunisomesha na kila kitu..kweli hatujui kesho yetu, huyo bro ndo alikuja kuwa kila kitu. Siku moja aliwahi kunikumbusha kuwa uliwahi niambia siwezi kukusaidia kitu, nilibisha na kukataa sijawahi kusema maneno hayo, lakin moyoni nilipata aibu na fedheha kubwa sana. Lakin bro yeye hakuwa mtu wa visasi, alinisamehe na kuona kama ni utoto tu ulikuwa unanisumbua. Lakin nilipata funzo kubwa sana usimdharau mtu.. huwezi jua kesho yake
 
Kweli bana usimdharau mtu

Sent from my SM-G935T using JamiiForums mobile app
 
Braza kote sijacheka ila hapo umekaa chini kwenye zebra crossing. Dah yalikufika aisee
 
Braza kote sijacheka ila hapo umekaa chini kwenye zebra crossing. Dah yalikufika aisee
Noma mkuu hadithiwa tu hivi hivi ila yasikukute!

Kuna wakati fulani miaka ya nyuma kidogo huyu mwanamke aliyesababisha hili alikuwa akipiga tu simu hata kwa salamu ya kawaida nilikuwa nikiiwaza hii ishu najiuliza ni mimi kweli niliyefanya kile kitendo?
 
Dah sisemi...

Ila naikumbuka hiyo siku kama vile ni kila siku inajirudia.

Na kila nikiwaza napata mshituko kama sio pannick attack.

Imebadili maisha yangu kabisa kabisa. Na ubaya ni siwezi kuzungumza na mtu yoyote kuhusu hiyo siku hata awe wa karibu namna gani.

Kwa hiyo inanila tu moyoni. Ila sikati tamaa Mungu atarekebisha.
 
ni moja ya tukio kubwa kutokea shybush. tulisimuoiwa na waliokutana nalo hapa bush kipindi nasoma
 
Eti ulilia hahahaha

Wanaume tunazidi kupungua Kwa kasi
 
Alikuwa mchepuko hii ndo faida ya kuwa na mchepuko pindi inapotokea km hivi huwa wanasaidia sn huyu mchepuko alikuwa anajua wanangu kitambo hata watoto nilikuwa nawatuma kwake
Wewe ndo ulimuua mkeo kwa ajili ya sonona. Halafu bado unamringishia huko aliko amesoma text yako kwa uchungu sana. Atakuwa anatokwa na machozi tu...unaendelea kumuumiza na sasa unaona haitoshi unamringishia kabisa kuwa yule mchepuko mliyeshirikiana naye kumuua mkeo...umeamua kumuoa kabisa... We jamaa huna huruma..unaendelea kumtesa marehemu unataka aendelee kufa tu kila mara? Futa yale maneno yako ya kifedhuli na umwombe msamaha...anaweza akaamua kukujia kabisa.... Akueleze mmemfanyia unyama sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…