Wasaaalam wana jamvi
Miaka ya nyuma wakati nachukua masomo ya elimu ya juu nilipata msala mmoja ambao hadi kesho siji usahau.
Ulikuwa ni msimu wa test au CAT wengine wanaita. Hiyo week tulikuwa tunatest moja somo la afya kutoka college hiyo,hilo somo kwetu lilikuwa ni non core kutokana na field yangu nliosoma.
Hio test ilipangwa ifanyike siku ya jumatano, huku naendelea na maandaiizi ya hio test nikaamua nitoke nikapunge hewa nje.
Wakati niko huko nje mishe mishe ikaingia sms .... Test kesho probability kufanyika saa 8 mchana.. wakati huo hio test ya somo la afya ilikuwa ni saa 4 asububi.
La haulaaaa mie nlikosea tafsiri hio sms nliitafsiri kama ..... Test ya kesho uwezekano kufanyika saa 8 mchana.....
Sikuuliza mtu jion nikaendelea na kukaza kisomo, imefika saa 4 jamaa wakaenda , na next door nlikuwa nakaa na jamaa zangu wawili wote tuko programme moja na tuko kundi moja la kufanya kazi za darasa ,lakini siku ya kufa nyaní miti yote hukatikaaa , jamaa wakaenda kufanya paper bila kunicheki.
Kumbe ile sms kuna wadau walikuwa hawajafanya test ya Probability ndio walikuwa wanatakiwa wafanye huo muda.
Nimekaa nasoma mishale ya saa sita naona wadau wanatoka wanafatana na karatasi mkononi, ikabid niulize mnatoka wapi wakasema kwenye test,nikajibu anhaaa then nikavungaa kama hakuna issue wakaniuliza we vp hujafanya nikawajibu ndiyo sijisikii vyemaaa nimeomba ruhusa ilhali sikuwanayo.
Badae nikamcheki Cr nikampa full story nikasema nitazingizia ugonjwa, jamaa akasema powa atampanga madam, jamaa kumcheki madam ,madam anakaza anataka taarifa toka hospital na barua ya HOD kwann sijafanya test....
Nikaenda kwa HOD nikamwambia madam naumwa sijaweza fanya test, hivyo nimemcheki madam wa somo kasema nije kwako uniandikie barua ya kuomba fanya test yangu pekee yangu, HoD akagoma ye hausiki na angeweza nisaidia kama ningekuwa na uthibitisho toka kwa daktari siku hiyo husika....
NAKUMBUKA MADAM HOD alinambia nenda kamuombe msamaha mwalimu wako la sivyo UTADISCO, Daaah nlivosikiaa hivoo nlitamani kulia ,nikatoka nikamuaga pale madamu nikaenda zangu nawaza.
Badae nikakaa room nikawaambia wana mkasaa mzima, wako walionifariji wakisema huwa wanakaza hivohivo mwishowe wanakuwekea hata zero, wengine nao wakasema yaoo.
Nikamcheki madam wa somo hewan akapokea simu navomueleza feedbacks za hOd akakata simu, nikamtext sms WhatsApp ndefu sana nikiomba anisaidie na jinsi nilivyo mgonjwa plus kuweka mafomu ya hospital mbalimbali palee ma madawa nayo kunywaa[emoji1787][emoji1787], nlimsihi sana aniwekee hata zero asiache blank ambayo itasababisha system inikataee,
Madam hakujibu akaniblock WhatsApp, nikamtumia normal text akawa hanijibu,. Kuna siku nikamtext madam nakuja ofsini kwako nikuombe msamaha ,nikajiandaa fresh kesho nikazama kwake ofisin sikumkuta ,nikaulizia pale wakasema nimsurbi aje lakini hadi saa lapita hakutokeaa. Nikamtext madam nimekuja ofsin kwako sijakukuta ,hakunijibu.
Nikamcheki madama mwingine ambaye nae alifundisha hilo somo, i mean hilo somo lilifundishwa na walimu wa 2 ,alianza huyo nliomiss test yake akaja huyu nliemtafuta mwishoni, nikamueleza mkasa mzima ,ye akasema ingekuwa nimemiss test yake angenisaidia lkn hiyo ni test ya mwalimu mwingine, nikamshukuru pale ,ikaishaa hiyóo.
Ukafika wakati wa UE nikafanya mtihani kwa mawazo sana hadi namaliza, nimeenda nyumbani nlikuwa ni mtu wa maombi sana huku nikiendelea mtext yule madam pasi na kunijibu, hadi nikawa naulizwa mbona namawazo sana nikawa navunga no issue.
Nimeenda field sina raha nawaza tu kuhusu hilo somo, ukawadia wakati wa ku upload CW kwa portal, masomo yote yakawekwa likabakia somo la huyu madam ni wote hatukuwekewa CW za hilo somo.
Siku matokeo yametoka Naogopa kuangalia matokeo, nikajjikaza nikaangaliaaaa... Daaah sikuamini madam aliniwekea CW 16 lakini final UE lile somo nilipata A na ndolilikuwa somo pekee nililopata A kwa hiyo semester.
I was like wooow God is so wonderful ilikuwa ni furahaaa sanaaaa.
Daaah nikikumbuka huwa nacheka sana na kuogopaa.
Popote ulipo madam Dr. Gibore ulinitesa sana we madam