Nilikua na mpenzi wangu tulipendana sana ila aliniboa siku 1 tukazinguana sana hasa mimi nilikasirka kupita maelezo,nikakaa baadae halmashauri yangu ya kichwa ikaniambia "huyu demu ni malaya muache"
basi nikawa namtafutia sababu nimuache,kuna siku nimekaa mahali nikaona anapita na mwanaume wanatembea mdogo mdogo kuelekea kwao,mimi nikainuka nikaunga tela kwanyuma nione wanaelekea wapi na watapitia wapi.
Basi wakaingia uchochoro flani kagiza kalikua kameingia wakasimama wakawa wanaagana kwa kuongea tu ila maongezi hayaishi,mimi uvumilivu wakufata nyuma kwa kujificha ficha ili wasinione kama bodyguard ukanishinda,Nikatokea Paap kama mzimu.
nikamwambia kwanza yule jamaa,Oya sepaaa Jamaa akaniogopa kweli akasepaa,nikabaki na dem,kwakua tulikua tumegombana akawa ananijibu shit,namuuliza huyu NANI ananiambia "haikuhusu" asee nilimzabua zabua,pga makofi.
Nikampokonya simu ili niende ikagua,nikamwambia leo kila mwanaume wako humu naenda kumuua,ngoja nikawatafute. Hapo nishampiga sanaaa.Huyoo nikasepa na simu yake.
Kufika home simu haikua na password, (haya ma pattern ma password yameanza kutumika hivi karbuni tu) zamani watu wengi simu hazkua na password.
Nikaanza kupekua, kweli mtoto wa kike kutongozwa n kawaida sana, basi nikakuta chatting za wanaume wakimtongoza,ila na yeye alikua akiwakataa tena kwa kuwambia ana mpenzi wake anampenda sana na akawa anawatajia jina kabisa.
Jina ni langu
Movies Store convo ya kwanza,nikatoka nikaingia ya pili nikakuta mwingine dem msimamo n ule ule hata atokeee mwanaume gani chni ya jua hawezi muachanisha na
Movies Store.
nikaingia na nyingine na nyingine,kuna moja ikanimaliza kabisa n msg ya Asubuhi tu,ya siku hyo nlompokonya simu, Alikua anachat na dada ake sijui rafiki anamwambia leo inaenda wiki
Movies Store hatuongei tumegombana,nateseka mwenzako sijui nafanyaje jaman, Rafki ake huyo anamwambia usijali mtakua sawa Tu kesho nitakusaidia kuongea nae, Dem akamshukuru sio kawaida.
Nikaanza kujutia kwann nilimpga mtoto wa watu kumbe ananipenda hvyo,Basi nikaendelea ku search nikaingia sehemu ya NOTEBOOK ya simu nikakuta malengo yake kwangu,jamani dada alinipenda yule sio kwa niliyoyakuta. Plan zake za kuja nifanyia kitu kwenye birthday yangu ya huo mwaka,mambo ni mengi mengi.
Nilijiona mkosaji mkubwa nikifkiria kpgo nlichomshushia yule mpenzi wangu,wakati naendelea pekua pekua simu yake ikaita nikapokea kumbe ni yeye kapga, akaniambia
Movies Store baki na hiyo simu milele siitaki tena wala sitaki kukuona na wewe.
Niliomba msamaha wa kila aina ila ndio tayari nilimpoteza yule dada kwao n mwanza nataman siku 1 nirudi mwanza nikamtafute walau nimsalimie nimuone tena. Nikikuta kaolewa sawa tuu ila kama n urofa maishani niliowahi ufanya ni kumpoteza yule binti kwa sababu zangu za kijinga jingaaaa.
Tangu na hiyo siku nikiwa na mpenzi wangu Hata asimame na mwanaume nitakaa pembeni waongee wamalize,sishiki simu yake,naheshimu watu anao wasiliana nao ki ufupi mpenzi wangu hata nikute kabebwa mgongoni na mwanaume mwingine mimi sitosema kitu,nitanyamaza ntamwambia "baby naomba twende nyumbani muda wa kucheza umeisha"