Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Kisa kipi kilikufanya ujute sana?

Majuto mengine yanatokana na tamaa. Sielewi hata ile akili tuliitoa wapi, Ila mm na mwanangu Shedrack tulipanga tuibe nguruwe wa shule tukauze. Kipindi hicho tupo O level, kwenye shule ya kanisa (seminary).

Ili issue iende kirahisi, tukaona ni heri kuiba vinguruwe vitoto, kuliko wale wakubwa. Tulichora radar yetu vizuri, Ila kimbembe ilikua kuwakamata maana ziti kidogo lilikua Pana, alafu Lina partitions ambazo zinatuzuia tusikimbie vizuri.

Vile vinguruwe ma'amae vilitupeleka mchaka mchaka, maana tulikuwa hatutaki kuvikamia, visije kupiga kelele. Mpaka tunavidaka, tayari nlikuwa na hasira maana nilianguka zizini kama mara mbili.

Tutakota vizuri mle zizini, kila mmoja akiwa kambana nguruwe wake vizuri ili asitoe kelele, japo vilikuwa vinagugumia kwa sauti ambayo inakera. Kumbe Kuna Sister alishtukia mchezo, Ila either hakua na uhakika na alichoona au aliamua kuwa mpole maana alijua angetumia papara tungemzidi mbio alaf asingekutujua maana ilikua jioni.

Shadrak ndo alikua wa kwanza kumgundua sister kua anakuja uelekeo tuliokuwa tumejibanza. Sister baada ya kuona kimya kimezidi, akawa anaondoka, naona alihisi hisia zake hazikua sahihi. Wakati ashapiga hatua kama 5,kale kanguruwe nilikokashika kakaanza kupiga kelele ng'wiii ng'wii ng'wiii, nikakabana zaidi, nako kakaongeza nongwa ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Sister akaanza kurudi huku akisema tusimame, vinguruwe ndo kwanza vinakazana ng'wiii ng'wii ng'wiii. Tukaanza kukimbia huku tumeinama, namwambia Shadrak tuviachie tuamshe, jamaa akakataa.


Tukaishia zetu kwenye kimsitu, Sister akabaki anatuangalia kwa mbali tu, vinguruwe navyo viko busy ng'wiii ng'wii ng'wiii.

Tukavifikisha tulipokua tunavipeleka, then tukarudi. Kurudi shule tukakuta wengine walishahesabiwa na kukaguliwa. Na ishajulikana ambao hatukuwepo, Sister alishanitambua mm kutokana na mzula niliokua nimevaa ( ule mkoa unabaridi), Shadrak alijulikana baada ya roll call ya ghafla kipindi hatupo.

Tuliitwa ofisini. Sister akaongea na sisi kitafiki kabisa kwamba tulichofanya sio kitendo Cha kistaarabu. Na akatuomba tukaoneshe tulipowapeleka kabla Sister mkuu hajarudi, alafu ikawa msala zaidi. Kinyonge ikabidi tuwapeleke. Vinguruwe vikarudishwa, sisi tukaendelea na vipindi class. Ila baada ya siku mbili tukaitwa Tena ofisini, nashangaa kumuona mshua pale.

Then akabidhiwa barua ya mm kufukuzwa shule. Shadrak nae alitimuliwa. Safari ya kutoka shule mpaka tunafika home ilikua chungu Sana kwa upande wangu, maana kwanza ni ndefu kinyama, lakini mshua hakuninunulia chochote Cha kula mpaka tunafika home, maji ya kunywa niliyapata kwavile ndani ya bus waligawa.

Kilichofata baada ya kufika home, nilikielezea humu kwenye ile story ya maisha yangu.
Mkuu umenichekesha sana aisee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Tulichapwa bakora siku ya kumaliza necta form six

Siku hiyo sitosahau nilikula mijeledi kama yesu msalabani bila kosa ndo nikaamini sio kila anayeenda jela ana makosa

Ilikua hivi Nakumbuka ilikua Alhamisi ile tunamalizia mtihani wa mwisho msimamizi akatuambia mkimaliza mtihani muende uwanjani msiondoke kwanza tukasema poa, tulikua tunahisi sijui walimu wanakuja kutupongeza basi tukapiga pepa pale mpaka muda tunaambiwa pens down watu wakaanza kuvunja ruler wanatupa peni wengine wanachana mashati wanachana suruali kwa furaha ya kumaliza

Mimi sikupanga kuchana ila kuna jamaa tulikua tunamuita Mjita(mtu wa ukerewe)alikua amekaa nyuma yangu akachukua kiwembe akaanza kuchana shati langu mgongoni
Nilimuacha achane tu kwani halina kazi tena (Najuta kumuacha achane lile shati)

Basi msimamizi akakusanya mitihani na kuondoka zake lile darasa nililokuwepo watu hawakuchana sana uniform nilishangaa nilichokiona baada ya kutoka nje kuna darasa lingine hao walichana nguo sio poa unaweza sema ni machizi wameachiliwa kifungoni kila mtu kachana anavyojua basi(kumbuka mjita alichana shati langu mgongoni)

Basi tukakusanyika uwanjani kama tulivyoambiwa tunashangaa tunaambiwa tukae chini na wale mapolisi waliokuwa wanasimamia mitihani tukawa tunajiuliza nini kina endelea

Kumbe Jana yake kuna baadhi yaform six walichana magodoro na mashuka ya form five na hiyo taarifa ikamfikia mkuu wa shule ndo akawaambia wale form five waandike majina ya watu wanaowahisi kufanya hicho kitendo na majina yalipelekwa kwa mwalimu mkuu ndo akawaambia polisi hawa vijana wakimaliza mtihani kuna haya majina shughulika nayo hiyo ndo ilikua sababu ya kuitwa pale uwanjani

Basi Yale majina yakaitwa wakasimamishwa pembeni alafu yule afande akasema mbona naona watu wamechana uniform..dah akasema wote waliochana uniform na nyie simameni jiungeni na hawa waliochana mashuka maskinii mjita aliniponza na Mimi nikajumuishwa Kwenye msala.tulikua kama 25 hivi tukaambiwa pangeni mstari mmoja kuelekea ofisini.wale ambao hawakuchana uniform zao waliruhusiwa waondoke sisi tukabaki
Polisi akaanza kusema nyie ndo wahuni eeh basi tutaonyeshana uhuni niliogopa sana

Tukapelekwa mpaka assembly ground tukaanza kupigishwa kwata na wale mapolisi dah Mara headmaster akaja akasema Leo nawachapa nawaaga kwa kuwachapa dah niliona kama ndoto hivi nachapwa siku ya kumaliza Necta Moyoni mwangu naendelea kumlaumu mjita kwa kuniponza,tulijitetea kwamba sisi hatuhusiki na kuchana mashuka sisi tumechana nguo zetu tu majina yao si yapo hapo sisi hatuhusiki ila wale polisi hawakutaka kuelewa wakaona ni wale wale tu wachanaji magodoro na wachanaji uniform

Basi headmaster akaagiza mzigo wa fimbo ukaletwa akaanza kutupelekea moto afu anachapa fimbo za mgongoni na kiunoni lazima akuachie alama kama sio Kukutoa damu.dah tulipelekewa moto sana kwa bahati nzuri na mjita nae alichana nguo Kwahyo tulikua wote tunasulubiwa (ningeumia sana kama mjita asingekuwepo) basi nikiona mjita anakula mijeledi na Mimi nafarijika

Kumbuka hapo tushamaliza mtihani wa necta wale wasimamizi ndo wa nasubiri lile gari linalozunguka kusambaza na kufuata mitihani mashuleni lije kuwafuata kwahyo hapo pona yetu ni mpaka lile gari lifike dah basi headmaster akaendelea kutupiga mijeledi na walimu wengine wakaunga tela tulichakazwa haswaa alama kibao mgongoni na kiunoni mpaka lile gari linafika tulikua tupo juu ya Mawe(lawama zote ziende kwa mjita)

Tulikubali kusulubiwa japokua tulikua tumemaliza necta tungeweza kugoma kuchwapwa lakini hatukuwa na jeuri hiyo kwa sababu polisi walikuwepo dah Kwahyo ukigoma tu polisi wanakuchezeshea mikwaju na unaenda kulala kituoni dah ikabidi tuache tu headmaster atupelekee moto chini ya uangalizi wa polisi,baada ya kipindi cha muda mrefu hatimae gari la kukusanya mitihani likafika ndo wale polisi wakaondoka na headmaster akatuacha ila hakutucha hivi hivi aliandika majina yetu ili siku ya kuja kuchukua result slip tulipe magodoro dah ilikua siku ya kihistoria Magodoro sikuchana,nguo sikuchana kwa mikono yangu,na mijeledi nimesulubiwa

Mjita popote ulipo mataccor yakooo!
Mjita
 
kiukweli kuna mtu najuta mno kumfanya rafiki, sina wa kumsimulia kisa changu maana hii siri nitakufa nayo mwenyewe, lakini najuta mno kumfanya rafiki na sina namna ya kumuacha na kumuweka mbali lakini pia sina namna ya kumkimbia.

Mola wangu wa mbinguni nisamehe mimi siyapendi haya na yananigharimu mno kwenye maisha yangu.
Sema mkuu
 
Kupga threesome na mademu wenye ugwadu wa kufa mtu..niliwatoroka na kibukta kwa kupitia dirisha la chooni.
 
INAUMA niliua pasipo kujua kama ninaua hii kitu inaniuma sana maana hakuna aliejua zaidi yangu na hadi sasa sijui nitakuja kuitubia wapi hii dhambi maana hata Mimi mwenyewe sikujua kama ninaua, ila baada ya kifo kutokea ndio nikaunganisha dot nikagundua iam murder pasipokujua, Binadam ni watu wabaya sana na wanaweza kukutumia kuuwa then wakakudamp.
Pole sana, tatizo linakuja jambo likishakaa kichwani ni shida kutoka
 
kiukweli kuna mtu najuta mno kumfanya rafiki, sina wa kumsimulia kisa changu maana hii siri nitakufa nayo mwenyewe, lakini najuta mno kumfanya rafiki na sina namna ya kumuacha na kumuweka mbali lakini pia sina namna ya kumkimbia.

Mola wangu wa mbinguni nisamehe mimi siyapendi haya na yananigharimu mno kwenye maisha yangu.
Same story kwangu, najuta najuta najuta, imenigharimu zaidi ya sana mpaka kesho
 
Oya sasa kwanini hukutimua mlivyoitwa na maafande?

Ulihofia nini tena kama mitihani ulishamaliza?

Sisi tulikuwa tunaogopa kufukuzwa shule tu lakini baada ya mitihani walimu ndio walikuwa wanatembea watatu watatu kuepuka kichapo cha revenge katika miaka minne yote waliyotutesa
Ishu ukimbie
Afande akufukuze
Akunate hapo ndpo utaona mfipa alizngua
 
KAMWE SIWEZI SAHAU TUKIO HILI

2018 kipindi nimemaliza kidato cha nne, sa day moj nlikua na washkaj zang nliomaliza nao shule tupo home seblen tunachek porn kweny Tv
, hapo tumewek CD kweny dek,
Tumechek mzigoo weeeee, hapo stim zimepanda kila mtu katoa mashne yake anaipooza,
Kipnd hcho wazaz wapo job na madogo wengne wap shule..
Tukiwa bdo tunaendelea kuchek porno wenyew tunaita Tution[emoji1787]
Gafla umeme ukakatika na CD ipo ndan ya dek,,, wale jamaa zangu wakaondoka nkabaki mwenyew nasubir umeme urud ntoe CD,
ikafka saa kumi bado umme haujarudi, na ndo time ya mzee kuja, pia akifika hua atak mtu achezee TV
kipnd natafakali nkaskia honi getini, nkajua n mzee hyu,, nkachomoa dek chap nkaend ficha chooni kuna kile kimlango cha juu kweny gypsum kwa ajili ya fundi kwend kweny dali, nlivyomalz nkaend kufungua geti,
Mzee akaenda chumbani kwake baadae akaja seblen akaon deck haipo, akaniuliza nkasem imeharbka nmepeleka kwa fundi ntaifata umeme ukirud
bas nkaend nje na mamb yang, baadae umeme ukarud nashangaa naitwa ndani kufika sebkeni nakuta porn ipo LIVE aloooooh nusu nizimie, nkaulizwa hiki n nn?nkawa sina majibu aisee
Nlipgwa
Ruka kichurachura
Tembelea tumbo
Pushup,
yan nlipgwa kama gaidi bahat nzur mam alitokea ndo naachwa ,, nakumbuk nlichanika usoni kidgo.
Kumbe mzee alvyotk job aliingia choon akaon gypsum kam imebomok kidogo, ule unga wake umemwagika chini, akahis kun kitu juu, alvyopanda akakuta deki,, NYIEEEEEE Mpaka leo hii nkionana na mzee ananiuliza kam bad anaangalia ila kiukweli nmeacha.
Kuanzia 2018 had leo sjawai kuangalia XNXX[emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23] kuna aibu ndogo na kubwa lakini hii Ni kubwa..
 
Sitakuja kusahu aisee maana mie nilililelewa na mzazi mmoja bimkubwa, mshua enzi hizo mambo mengi hivyo bimkubwa akajitaa so mshua akaanzisha familia yake nyingine ambayo aliipa thamani kubwa halafu ukizingatia na mshiko mrefu wa dili zake za mbao.

Sasa bimkubwa akifight sana mpka nikamaliza chuo mwanzoni mwa 2000, mshua kule madogo walizingua wote kwenye elimu halafu kwetu hakuwa anahudumia chochote sio kwa kuambiwa ni kwa kuona kabisa, alikata networks baada ya muda mambo yakamuendea kombo hapo tayari nipo kwenye ajira.

Akaanza kunitafuta nimpe sapoti ya kiuchumi nilikuwa Nampa kimtindo bila kinyongo ila nguvu kubwa niliwekeza kwa bimkubwa, mshua akajua hilo akaenda kumkoromea bi mkubwa kuwa kwanini mie nampendelea sana yeye kuliko yeye mshua?

Hakika sintasau na hakika najutia maana hamaki niliyokuwa nayo nilienda kumuwakia mshua tena kwa facts aache kabisa kumzonga bi mkubwa ila baadae nilijutia sana maana mshua alikuwa mdogo sana hali hiyo ikapelea pressure kupanda ila Mungu ni mwema yupo poa ila alishakuwa mgonjwa mgonjwa ambapo moyoni najihisi hatia kuwa nahusika na ugonjwa wake.
Mnaona mambo yenu wanaume mnavokuwaga🤣🤣 ila wababa🤣 ila pole
 
Nilikua na mpenzi wangu tulipendana sana ila aliniboa siku 1 tukazinguana sana hasa mimi nilikasirka kupita maelezo,nikakaa baadae halmashauri yangu ya kichwa ikaniambia "huyu demu ni malaya muache"

basi nikawa namtafutia sababu nimuache,kuna siku nimekaa mahali nikaona anapita na mwanaume wanatembea mdogo mdogo kuelekea kwao,mimi nikainuka nikaunga tela kwanyuma nione wanaelekea wapi na watapitia wapi.

Basi wakaingia uchochoro flani kagiza kalikua kameingia wakasimama wakawa wanaagana kwa kuongea tu ila maongezi hayaishi,mimi uvumilivu wakufata nyuma kwa kujificha ficha ili wasinione kama bodyguard ukanishinda,Nikatokea Paap kama mzimu.

nikamwambia kwanza yule jamaa,Oya sepaaa Jamaa akaniogopa kweli akasepaa,nikabaki na dem,kwakua tulikua tumegombana akawa ananijibu shit,namuuliza huyu NANI ananiambia "haikuhusu" asee nilimzabua zabua,pga makofi.

Nikampokonya simu ili niende ikagua,nikamwambia leo kila mwanaume wako humu naenda kumuua,ngoja nikawatafute. Hapo nishampiga sanaaa.Huyoo nikasepa na simu yake.

Kufika home simu haikua na password, (haya ma pattern ma password yameanza kutumika hivi karbuni tu) zamani watu wengi simu hazkua na password.

Nikaanza kupekua, kweli mtoto wa kike kutongozwa n kawaida sana, basi nikakuta chatting za wanaume wakimtongoza,ila na yeye alikua akiwakataa tena kwa kuwambia ana mpenzi wake anampenda sana na akawa anawatajia jina kabisa.

Jina ni langu Movies Store convo ya kwanza,nikatoka nikaingia ya pili nikakuta mwingine dem msimamo n ule ule hata atokeee mwanaume gani chni ya jua hawezi muachanisha na Movies Store.

nikaingia na nyingine na nyingine,kuna moja ikanimaliza kabisa n msg ya Asubuhi tu,ya siku hyo nlompokonya simu, Alikua anachat na dada ake sijui rafiki anamwambia leo inaenda wiki Movies Store hatuongei tumegombana,nateseka mwenzako sijui nafanyaje jaman, Rafki ake huyo anamwambia usijali mtakua sawa Tu kesho nitakusaidia kuongea nae, Dem akamshukuru sio kawaida.

Nikaanza kujutia kwann nilimpga mtoto wa watu kumbe ananipenda hvyo,Basi nikaendelea ku search nikaingia sehemu ya NOTEBOOK ya simu nikakuta malengo yake kwangu,jamani dada alinipenda yule sio kwa niliyoyakuta. Plan zake za kuja nifanyia kitu kwenye birthday yangu ya huo mwaka,mambo ni mengi mengi.

Nilijiona mkosaji mkubwa nikifkiria kpgo nlichomshushia yule mpenzi wangu,wakati naendelea pekua pekua simu yake ikaita nikapokea kumbe ni yeye kapga, akaniambia Movies Store baki na hiyo simu milele siitaki tena wala sitaki kukuona na wewe.

Niliomba msamaha wa kila aina ila ndio tayari nilimpoteza yule dada kwao n mwanza nataman siku 1 nirudi mwanza nikamtafute walau nimsalimie nimuone tena. Nikikuta kaolewa sawa tuu ila kama n urofa maishani niliowahi ufanya ni kumpoteza yule binti kwa sababu zangu za kijinga jingaaaa.

Tangu na hiyo siku nikiwa na mpenzi wangu Hata asimame na mwanaume nitakaa pembeni waongee wamalize,sishiki simu yake,naheshimu watu anao wasiliana nao ki ufupi mpenzi wangu hata nikute kabebwa mgongoni na mwanaume mwingine mimi sitosema kitu,nitanyamaza ntamwambia "baby naomba twende nyumbani muda wa kucheza umeisha"
Kuna kitu cha kujifunza hapa mkuu
 
Back
Top Bottom